Wezi wa BoT - EPA warejesha bilioni 50 hadi leo

Ndugu, bongo

Hakuna mtu angependa kuwa na mashaka na JK kwa sasa, lkn kama yeye ni kiongozi anatamka nini kwa haya yanayo endelea? Kama unavyo onyesha upendo na kumshiba JK basi na kama uko jirani naye mwambie arekebishe haya mambo! Watendaji wake wanamharibia sana kama hawa kina Hosea, Chenge, Mustafa etc

festog naona hujaisoma post ya mbangaizaji hapo juu, naona ungali-isoma usingeuliza JK anatamka nini, naomba isome halafu utaona JK anatamka nini na hatua zipi alizochukua mpaka sasa.
 
festog naona hujaisoma post ya mbangaizaji hapo juu, naona ungali-isoma usingeuliza JK anatamka nini, naomba isome halafu utaona JK anatamka nini na hatua zipi alizochukua mpaka sasa.

Mbangaizaji amerocall EPA report tu!

Nauliza JK amesema nini juu ya Hosea, na maelezo kama haya ya Mkullo?
 
festog naona hujaisoma post ya mbangaizaji hapo juu, naona ungali-isoma usingeuliza JK anatamka nini, naomba isome halafu utaona JK anatamka nini na hatua zipi alizochukua mpaka sasa.

kuna kutamka na kutenda, majina ya wauza madawa kwani alipewa leo au mwaka huu?
 
Kitu kimoja hapa kipo wazi. Wizi mkubwa au kwa kimombo grand corruption iko embedded katika serikali/mfumo wa utawala. Kwa maneno mengine: tuna kitu inaitwa institutionalised corruption. Kama si hivyo, inakuwaje BOT chief anasema mafisadi wameanza kurudisha fedha kienyeji; na wananchi wanaona ni kitu cha kawaida tu?

Na hoja yangu hii inaweza kueleza vizuri, kwa nini pamoja na CCM/serikali kuonekana imechafuka sana, lakini bado kwenye uchaguzi inashinda na itaendelea kushinda. Mfumo wa kifisadi tulionao ndio unatuletea yote haya.
 
Ndugu zangu,

Hili kosa si la Kikwete wala si la serikali yake wala si la Chama chake cha CCM. Hili ni kosa letu na upumbavu wetu wa kukiweka chama hiki cha CCM (TANU/ASP) madarakani kwa miaka yote hii (1961-2008). Tunakubali kiini macho cha kubadilishiwa sura ya mtu kila baada ya miaka 10.

Asilaumiwe mtu wala kitu hapa. Ni sisi wenyewe na ujinga na uwoga wetu. Tunavuna tulichopanda.

Mapinduzi na mageuzi ya nchi yetu yataletwa na sisi wananchi wenyewe. Si CCM si CUF si CHADEMA si TPL si UDP si NCCR-Mageuzi ni Wananchi wenyewe, hizo ni platforms tu tunazoweza kuzitumia kujiletea Mapinduzi na Mageuzi.

Kama tumekasirika kikweli kweli, tu-organize na ku-moblize tufanye kweli 2010.

Hapa ndugu yangu nakuunga mkono 100%. Ila naongeza tu hatuhitaji kusubiri 2010 ili kupata majibu amabayo JK kwa kauli yake alituahidi Watanzania.
Watanzania tujifunze kujua mambo muhumu ya kitaifa na kuyachukulie hatua,ikiwa ni pamoja na ku-demand majibu,uwajibikaji kwa njia ya maandamano mazito.
AMA KWELI WAJINGA NDO WALIWAO( VYA WAJINGA NDO HULIWA)

mbangaizaji ahsante sana kwa kubandika hiyo post, watu wengine humu JF huwa wanabwabwaja tu. kwa wale wanaobwabwaja kama hampati jibu katika hiyo post ya mbangaizaji ndio muanze kuleta hoja, la sivyo fanyeni subra kazi inafanyika, muda wa tume ukiisha na kama hakuna action yeyote kutoka kwa waliokabidhiwa hiyo kazi na JK akikaa kimya tu, hapo ndio tuandamane, tuchukuwe sheria mkononi, tufanye kila tuwezalo kuhakikisha mambo yanakwisha kwa faida yetu walipa kodi, au mnasemaje?
.

Anayebwabwaja ni JK ambaye hajui kati ya kile anachoahidi kukitenda na anachokitenda. Inakuwaje anawaogopa hawa majambazi kuliko siye wenye mali.kAPEWA MAJINA YA WAUZA UNGA KAONA SIRI.ANAJUA WEZI WA BOT ANAONA SIRI. Hivi ingelikuwa kapuku aloiba hivi ingekuwa siri kweli. Kifupi anajijengea dharau sana.
 
Hao wachukuliwe hatua za kisheria, mbona wezi wa kuku wamejazwa magerezani? Au tuchukue ushauri wa NdesaPesa( wanyongwe mpaka kufa)
 
Ndugu wanaJF.

Miezi sita iliyotolewa ilikuwa ni mkakati wa serikali kukusanya 133Billion kutoka kwenye vyanzo halali vya mapato ya serikali(Kodi za walala hoi) kuziingiza kwenye account na kusema mafisadi wamerudisha. Tegemea kama TRA wakitoa taarifa ya mapato utaona collection zimeshuka kwanzia January.

So tunapenda kuona Details za fedha zilizorudishwa. Ikumbukwe Tume ya BoT ilisema 70% ya hela zilipelekwa nje ya nchi hivyo tunapenda kujua Jina la Mrudishaji, account yake au Banker wake, Kiasi kilichorudishwa na account iliyotumika kupokea marejesho(tarehe, siku na saa ni muhimu)na 70% ya marejesho yatoke nje ya nchi. Kama hizi taarifa hazitawekwa hazarani kama mafisadi na wamiiliki wa makampuni walivyowekwa hadharani, basi JK, na serikali yake yoote iwajibishwe kama alivyofanywa Lowassa.Maana tunaamini fedha zaidi za walalahoi zinaidi kufujwa kufukia za mafisadi.

Transparency will set everyone free from suspicion, JK na watu wako kuweni wazi, usitetee ujinga ambao haunia mantiki

With down troden heart, naomba kuwakilisha
 
WanaJF muda huu Waziri wa Mipango na Fedha Mustapha Mkullo, sijui naye ni alhaj au vipi, anatangaza kuwa bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkullo anasema kuwa fedha za mwisho kufikisha kiasi hicho ziliingia leo asubuhi sana kutoka akaunti moja ya mwizi ambaye hata hivyo, kama kawaida, kwamba hana haja ya kumtaja kwa sasa.
Anasema hivi sasa kuwa fedha hizo zinazorejeshwa hazina riba. Kila mwizi anarejesha kama alivyochukua, bila kujali kama alizitumia kufanya biashara au vinginevyo.
Wakati akisema hivyo, wananchi nao, kama ilivyo kwa JF, wanataka kurejesha tu isiwe nongwa, wakamatwe na washitakiwe.

Bila kuwataja majina hawa waliorudisha pesa hizo na kupata uthibitisho wa kutoka bank iliyopokea pesa hizo wa kutuhakikishia pesa hizi zimeingia katika account namba gani na zimeingia lini na kiasi gani, basi huu utakuwa ni usanii wa aina nyingine. Tunataka independent party wakafanye uhakiki wa haya anayozungumza Mkulo, vinginevyo hatuna imani na wasanii na hao wanaorudisha pesa kwa nini hawasweki lupango? :confused:
 
Katika harakati za kupambana na rushwa yapo mambo mawili mengine ambayo tutayaangalia kwa karibu. La kwanza ni mikataba. Tutaangalia upya taratibu za mikataba mbalimbali inayoingiwa na Serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikaji. Mikataba ni mwanya mkubwa wa rushwa hasa zile kubwa kubwa za wanaotafuta utajiri.

Kadhalika, hatuna budi kuchukua hatua thabiti za kuzuia watumishi wa umma kutumia nafasi zao kujitajirisha na kujilimbikizia mali. Sisemi kwamba ni haramu mtu kuwa tajiri au kuwa na mali. Ninachosema mimi kuwa ni haramu ni kutumia nafasi yako ya utumishi au uongozi wa umma kujipatia manufaa ya kujitajirisha au kujilimbikizia mali.

Ninavyomjua mimi Kiongozi wetu ni Mjanja Sana na Less Talkative !!

Its true kesha anza kuipitia mikataba.. so Lets Give him Time. Sio Rahisi kama mnavyo fikilia awake tuuuu kama muuza dawa za panya... kapitia pale chuo cha diplomasia.. ikifika muda wa kuongea ataongea, Pipo kam dawn wanawane.

Pili baadhi ya watu washawajibika na wengine wakina Chenge wanakuja ... Tatu atachukua Hatua Thabiti ..

Yuko katika wakati mgumu sana wananchi kwani lazima apange na plan B unafikili rahisi kumuua Shetani.. whut if U miss Him ???

Lets Have little Faith ndani ya mioyo yetu... en he will do somethin for us tooo.

It wasnt easy for Him to call Edward pale kivukoni na kumwabia Ur FireD Huh !! ivi nyinyi mnamjua Edward mnamsikia....

So Bravo JK (kiongozi) that waz Smart of u naw I know whut Next.

Japo najua wewe pia ni binadamu but ya hawa binadamu wengine yamezidi.
 
So tunapenda kuona Details za fedha zilizorudishwa. Ikumbukwe Tume ya BoT ilisema 70% ya hela zilipelekwa nje ya nchi hivyo tunapenda kujua Jina la Mrudishaji, account yake au Banker wake, Kiasi kilichorudishwa na account iliyotumika kupokea marejesho(tarehe, siku na saa ni muhimu)na 70% ya marejesho yatoke nje ya nchi. Kama hizi taarifa hazitawekwa hazarani kama mafisadi na wamiiliki wa makampuni walivyowekwa hadharani, basi JK, na serikali yake yoote iwajibishwe kama alivyofanywa Lowassa.Maana tunaamini fedha zaidi za walalahoi zinaidi kufujwa kufukia za mafisadi.

Na baada ya hapo tuambiwe ni wangapi wapo segerea wanasubiri kufikishwa mahakamani....jamani mbona ili hamlitolei hoja,...tunataka kujua ni wangapi wako watakuwa segerea baada ya hiyo miezi sita...hivi hamkusikia china yule jamaa mkuu wa kitengo cha madawa alivyofanywa kama Saddam Hussein...bilion 130 zinatosheleza kuokoa maisha ya watoto wa kitanzania wanaofariki kila siku...zinatosha kugharimikia matibabu, chanjo, elimu na mengine mengi kwa takaribani miaka kama zaidi ya kumi (hapa naoengoelea watoto wadogo tu...ambao ndo wanapashwa kuitawala hii nchi muda mrefu...maana sisi wote hapa ni marehemu watarajiwa kati ya miaka 20 - 50 ijayo..ttukijua ilo nadhani hata ufisadi utaisha kabisa.... miaka 30 ijayo JK na EL wake watakuwa takribani 85 au 90 wakati anayezaliwa leo atakuwa 30..sasa nani anapaswa kupewa kipaumbele jamani...jamani JK...EL, na wengine fikirieni...Tanzania ya miaka 30 ijayo...kwani vyote vilivyochumwa kwa ufisadi mtaviacha hapa duniani ndugu zangu...acheni kutuletea kiwingu.....
 
Hii hotuba JK alisoma kama ilivyoandikwa,kwa hiyo yeye kama jk hakuandika hayo aliyoyasoma.ndio maana hata utekelezaji wake unakuwa wa shida sana, kama angejua kuwa itatuwa hivyo basi nafikiri angeruka baadhi ya maneno.


Ina maana JK ni mtu wa kusoma tu...lakini wakati wa kutoa taarifa uwa wanasema Rais JK amesema hivi..., sasa nasema kwamba maneno yalitoka kinywani mwake na ndo inabidi tutatumie kumbana ili afanye kazi kulingana na matarajio yetuy...jamani kumbukeni asilimia zaidi ya 80% si mchezo...lazima afenya kazi...kama ameshindwa aondoke awaachie wenye uwezo....
 
michkp.jpg
 
Kama wanaosema kuwa pesa zinarudishwa ndio wale wale waliosema kuwa hakuna wizi au upotevu wowote umefanyika in the first place basi inabidi uchukue muda kidogo kuamini maneno yao.


kusema ukweli ni kuzuri pale tu ukweli utakaposemwa utaleta faida kwa sehemu husika, lakini kama kusema ukweli kutaletea matatizo na machafuko, basi kusema ukweli si kuzuri, na kama kusema uongo kutaleta furaha au amani sehemu husika basi kusema uongo ni bora kuliko kusema ukweli.Mwandishi : Anon
 
WanaJF muda huu Waziri wa Mipango na Fedha Mustapha Mkullo, sijui naye ni alhaj au vipi, anatangaza kuwa bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkullo anasema kuwa fedha za mwisho kufikisha kiasi hicho ziliingia leo asubuhi sana kutoka akaunti moja ya mwizi ambaye hata hivyo, kama kawaida, kwamba hana haja ya kumtaja kwa sasa.
Anasema hivi sasa kuwa fedha hizo zinazorejeshwa hazina riba. Kila mwizi anarejesha kama alivyochukua, bila kujali kama alizitumia kufanya biashara au vinginevyo.
Wakati akisema hivyo, wananchi nao, kama ilivyo kwa JF, wanataka kurejesha tu isiwe nongwa, wakamatwe na washitakiwe.

Inakera,inachefusha moyo na kutapisha - hivi hawa viongozi walioko madarakani watatuchukulia sisi WTZ kama makondoo hadi lini?
 
Watanzania tulitegemea nini kutoka kwa Waziri wa fedha aliye Haramia na jambazi mzoefu wa fedha za wananchi?

Mustafa Mkullo amewekwa pale wizara ya Fedha ili kulinda wezi wote ndani ya SISIEMU.Hizi fedha si kweli kwamba zinarudishwa kutoka kwenye mifuko ya wezi ila ni fedha za serikali zinahamishwa kutoka mfuko mmoja kwenda mfuko ule ulio ibiwa.
Wezi walio Viongozi na wanachama wa SISIEMU kamwe hawawezi rudisha fedha kwa sababu imani yao haiwaruhusu kufanya hivyo na pia ukweli kwamba fedha hizo wamekwisha ziingiza katika miradi isiyoweza geuzwa fedha haraka na nyingine kuzitumbua kwa umalaya na ulimbukeni wa ukubwani.

Taarifa kwamba majmbazi wanarudisha fedha ni usanii mkubwa kuliko ule wa mwanzo wa kuiba fedha toka BOT.
Serikali ya SISIEMU wanatuibia kwa mara ya pili kwa kubangaiza fedha kutoka kila pembe ya mapato ya serikali ili tu MH Kikwete aonekane anafanya kazi.

Wanajidanganya wenyewe.

Sasa hivi wapambe wa rais wamejaa kila kona kumpigia debe kwamba anawajibika kuliko rais yeyote, wakati jamaa alisha fikia ukomo wa Vision yake siku nyingi zilizo pita na sasa tufani na vimbunga vya kashfa vinampeleka kule asiko jua. Wild Territory.

Kifupi ni kwamba rais wetu ana meno lakini ni plastic kwa hiyo hawezi uma badala yake anapulizia hata pale pasipo hitaji pulizwa.

Serikali ya SISIEMU imekiuka sheria za nchi kwa kuruhusu wezi na wauaji kuendelea kutanuwa mitaani na ma GX na VX yao huku wakiweka vifua vyao mbele kwa sababu wanajua sisi wananchi hatuna cha kuwafanya.

Hatua ya kutangaza kwamba majambazi wa uchumi wameanza kurudisha fedha ni Uhaini ambao ni felony tosha ya kuwapeleka SISIEMU kizimbani kujibu mashtaka.

SISIEMU wenyewe kama chama au genge la wahuni ndani ya chama chao wanahusika moja kwa moja na wizi wa fedha za BOT. Hatua ya kutangaza kwamba majambazi wa fedha za BOT wameanza kuzirejesha pia ina nia ya kujisafisha wao wenyewe kwa sababu fedha walizo iba zilitumika kupigia kampeni chafu ya kushinda kwa hila mwaka 2005.

SISIEMU hawawezi kujisafisha kwa kuendelea kujichafua. Hatua wanazochukua, ambazo ni kinyume na sheria za nchi, ni kuendelea kujichafua zaidi kukliko kujiosha.

Mtu, Taasisi au kampuni yeyote ile iliyo husika na wizi wa fedha BOT ni lazima ifikishwe Mahakamani kujibu mashitaka, kwa sabau wizi ni kosa la jinai, kosa la jinai haliamuliwi ndani ya kikao chochote cha chama au serikali. Kosa la jinai linaamuliwa Mhakamani kwa haki(sheria).

Onyo kwa seikali ya SISIEMU.
Ni rahisi sana kupindisha sheria ili kulinda watu wachache ndani ya mduara wenu. Lakini si rahisi hata kidogo kuyakabiri matokeo ya kupindisha sheria.

Kumbukeni kwamba Tanzania siyo nchi mliyo rithishwa na bibi zenu kwa haki ya kuzaliwa, mmepewa dhamana tu kuiongoza Tanzania.

Ninyi SISIEMU mnafanya mambo yote yaliyo wahi kufanywa na vyama vilivyokaa madarakani kwa muda mrefu katika nchi nyingi duniani na sasa havipo kwa sababu vimeondolewa madarakani na walioviweka bila kujali utajiri na fedha kwa mlima za vyama hivyo.

Kuendelea kupindisha taratibu na sheria ni kuongeza kasi za kukimbia kuelekea dawati la umauti wa kisiasa.

Mmeweza kuwafanya Watanzania mazuzu kwa muda wa miaka 47 lakini haitakuwa rahisi hata kidogo kuendelea kuwadanganya watanzania hawa baada ya miaka 49 ya ununda wenu. U Know what I saying???
 
Unajua wazalendo wenzangu, of you who are familiar with the basic principles of the criminal law. Theft is taking the properrty of another with intention to permanently deprive the owner..

-physical element= is there, wameiba
- mental element is there= walifanya makusudi bank transfers and fraud do not happen by themselves

Kurudisha sio hoja, maana mwizi akiiba mkoba alafu aka kamatwa barabarani, mkoba unarudishwa alafu bado ana funguliwa MASHTAKA na ushahidi ukiwepo anafungwa.

-Serikali ya JK ikishindwa kuwashuhulikia WAHALIFU hawa then watakuwa wame demonstrate kuwa TANZANIA hakuna rule of LAW na nyimbo zao nyingine zote zitakuwa tantarira...

WEZI WASIPOshitakiwa, nakuadhibiwa, basi tanzania tumekwisha. Hicho ndio kitakua kipimo halisi cha uungwana wa huyu Rais wetu na serikali yake, sio richmond, Ballali, Lowassa etc.... Wote, waliohusika atakama ni usalama wa taifa basi wa chinjiwe baharini (tuwaone mahakamani) kinyume na hapo hamna ki2. Siwezi hata kupoteza pumzi yangu kujadili chochote saivi mpaka nione prosecution. Ambayo kisheria kutakua hakuna hatia ya kupprove maana by analogy wamerudisha hela, meaning wameiba. THUS WAFUngwe.. its only a plea of GUILTY and sentencing that is requied.

SAsa tuache kisheria, tuongee kisiasa, nidhahiri kwa mtu yeyote ambae anaakili timamu kuwa kuna uwezekano mkubwa (tena hapa nafikiria very conservatively bila jazba) CCM wanatumia fedha za wananchi kulipia uchaguzi wao.. Na kwa style hii, serikali nzima haifai... na JK na mawaziri wake wote ambao ni wanachama waandamizi wa CCM, ni uozo.. JE WANAWEZA KUKUBALI SERIKALI YAO IANGUKE?? EEH HAPANA HATA KWA DAWA. BASI chakufanya nikulipua richmond... kumpoteza EL and kuchanga karata (baraza) kidogo then kupeta kama kawa. After all wabongo mnataka nini. hela sizimerudi eeh.. TULIENI... Infact, mimi napinga na mtu yeyote humu ndani kama hawajamaa wasipochuniwa... MIMI KICHAA.. but anyway.. lets wait and see. Naomba Mungu JK aniprove wrong tu.
 
Ni kwa manufaa ya Taifa, fedha zetu kurudishwa alafu tuende mahakamani baadaye... otherwise tukianza mahakamani kesi zitachukuwa miaka saba... uliwahi lini kusikia jaji/hakimu anafunga mtu anayeiba kiasi hicho cha fedha?

Watanzania tulieni basi,,, hela irudishwe kwanza, wanaorudisha sisi twaendelea kupata vidhibitisho vya kuwapeleka mahakamani...chonde chonde Watanzania Angalieni Mbali zaidi ... achani kuangalia mita mbili mbele...
 
Ndulu na waziri wamesema majina na account details zitatolewa 'wakati muafaka' kupitia vyombo vya habari...go figure
 
Ndulu na waziri wamesema majina na account details zitatolewa 'wakati muafaka' kupitia vyombo vya habari...go figure
 
Back
Top Bottom