kusema ukweli ni kuzuri pale tu ukweli utakaposemwa utaleta faida kwa sehemu husika, lakini kama kusema ukweli kutaletea matatizo na machafuko, basi kusema ukweli si kuzuri, na kama kusema uongo kutaleta furaha au amani sehemu husika basi kusema uongo ni bora kuliko kusema ukweli.Mwandishi : Anon
Nacho jua mimi ni kwamba walio chukua pesa za EPA na zinginezo ni wale wachache ambao wamesha jihesabu kama wenye Nchi .Utakuja hata JK yumo na mashikaji wake zote so is hard to leave them naked na ndiyo maana usanii unafanyika .Lakini hili jambo ni kubwa na la hatari sana.
"Baada ya kuipitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na ya Mkaguzi wa Nje, yaani, Kampuni ya Ernst and Young, Mhe. Rais amesikitishwa na kukasirishwa na taarifa ya kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje vilivyofanywa katika taasisi muhimu na nyeti kama vile Benki Kuu. Kwa hiyo, ameamua kuwa hatua za kisheria na kiutawala zichukuliwe dhidi ya makampuni na watu waliohusika na vitendo hivyo viovu.
Kwa ajili hiyo Rais ameamua yafuatayo:-
1. Ametengua uteuzi wa Dkt. Daudi A. Balali kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
2. Ameagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ikutane mara moja kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya Maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara hii kwa taifa.
4. Rais amewaagiza; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kuchunguza na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kwa makampuni na watu waliohusika na uhalifu huu. Rais amewataka watumie ipasavyo mamlaka na madaraka waliyo nayo kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka wakamilishe kazi hiyo katika kipindi cha miezi sita. Amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe kiongozi wa kazi hii. Amewataka wahakikishe kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.
Kwani Warudishe Au Wasirudishe Zitatusaidia Nini Au Zitaongeza Kitu Gani Mimi Naona Nyimbo Ni Zile Zile Tu Miaka Nenda Rudi Mpaka Roho Zitakapoacha Miili
Kama Ingekuwa Serikali Yangu, Na Ili Kuonyesha Kweli Nimekichukia Kitendo Hiki, Nisingeangalia Mambo Ya Haki Za Binadamu Wala Nini Ningewatoa Hadharani Tena Ningealika Vyombo Vya Habari Itv Tvt Dtv Live. Nakata Kichwa Mmoja Mmoja Ili Iwe Fundisho Kwa Wengine Na Najua Wananchi Wangenishangilia Hatuwezi Kuwa Tunaendekeza Mambo Ya Kupuuzi Tu Kila Siku Ni Longo Tuu Hadithi Ni Zile Zile Mbona Alipoiba Kasusura Tena Dola M 2 Tu Mlitaka Kumtoa Korodani Na Kosa Kosa Lakini Jela Miaka Kibao Yaani Sawa Na Kumuua Maana Kwa Umri Alio Nao Na Miaka Mli Yomfunga Ni Sawa Na Mmemuua. Ina Maana Hawa Ni Nani Na Kasusura Ni Nani
JK anakwepa mada, jana ameongelea mambo ya misaada tu ktk hotuba yake. Omba omba kwa Bushi na kusolve mgogolo wa kenya mambo ya ndani yaliyo na madhara kabisa hajagusa hata chembe. Anaogopa nini kama yeye hakuwemo ktk madudu haya.
Mafisadi wa BoT warudisha bilioni 50/-
Faraja Mgwabati
Daily News; Friday,February 29, 2008 @06:10
Tumekamata mali nyingi tu na nyingine zilikuwa nje, alisema Mkullo na kuongeza kuwa, lengo na matarajio ya Serikali itafanikiwa kurejesha asilimia 80 ya fedha zote zilizoibwa, yaani Sh bilioni 106.4.