Kamanda
Senior Member
- Dec 5, 2007
- 150
- 176
WanaJF muda huu Waziri wa Mipango na Fedha Mustapha Mkullo, sijui naye ni alhaj au vipi, anatangaza kuwa bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkullo anasema kuwa fedha za mwisho kufikisha kiasi hicho ziliingia leo asubuhi sana kutoka akaunti moja ya mwizi ambaye hata hivyo, kama kawaida, kwamba hana haja ya kumtaja kwa sasa.
Anasema hivi sasa kuwa fedha hizo zinazorejeshwa hazina riba. Kila mwizi anarejesha kama alivyochukua, bila kujali kama alizitumia kufanya biashara au vinginevyo.
Wakati akisema hivyo, wananchi nao, kama ilivyo kwa JF, wanataka kurejesha tu isiwe nongwa, wakamatwe na washitakiwe.