Western Propaganda Turns Mugabe into a Tyrant


kunakipindi nilisikia kwamba jongwe na mzee madiba picha zao haziendi. kama kuna ukweli basi hii inawezekana ni sababu iliyomfanya mzee madiba kusita kuzungumzia zimbabwe mapema kwani watu wanaweza husisha msimamo wake na "bifu" lao.

kuhusu kusemea uingereza hata mimi nashangaa, isipokuwa nakumbuka sana kwamba mzee madiba hakuhudhuria mazishi ya mwalimu kwani alikuwa uingereza. zinatolewa sababu lakini bahati mbaya mpaka leo sijazielewa.
 
Ni ukweli tu uliosema hapo. Anayebisha na aje na hoja ya kweli. Sidhani kama mwenye macho anasubiri kuambiwa angalia. Ni kweli commrade
 
Mimi katika uchaguzi wa 2005 hapa hapa Tanzania nilishuhudia kwa macho yangu wapenzi wa CCm wakishambulia wafuasi wa cuf waliokuwa katika msafara wao wa kampeni kwa nondo na tena bila aibu.
Kuliwa na ushahidi kabisa wa video na polisi walipewa lakini walinyamza kimya badala ya kuwafungulia mashitaka vijana wa ccm waliojeruhi watu.
Sasa kama ingetokea vifo tungesemaje?
Si mnakumbuka na ule uchaguzi kule Manyara?
Haya hapa tuseme ni wazungu pia?
 
Lini wameacha kuteteana? Kiongozi gani wa kiafrika ametoswa na wenzake?


kwani sasa ndio ameambiwa sadc wameacha kuteteana?

naamini ile move ilikuwa political blunder ambayo imechangia kuongezeka
kwa imani kwamba jamaa ni stooge. kama ambavyo mbio zake za kukimbilia
ubalozini hapo majuzi.
 
Hizi ni propaganda. Kama si kweli leta ushahidi hapa jamvini.
Propaganda kama hizi ndizo zimetufikisha hapa tulipo Tanzania. Baada ya miaka 40 na kitu bado tunaangaika na semi kwamba tuko hivi sababu ya wazungu/wakoloni. Hii si ni aibu? Ugonjwa wa kujitakia tu.
 

hivi tumejiuliza wazungu walicheza role gani katika kufanya mazungumzo
ya kugawa ardhi kutofanikiwa? haw jamaa walikuwa ni lobby group yenye nguvu kiasi cha kukwamisha zoezi hilo. bahati mbaya hawakuona kwamba nao wanajiseti kupata dhoruba ya kisiasa siku za usoni. na kweli muda ulipofika na suala la ardhi lilipokuwa turufu tosha ya kisiasa turufu hiyo ikatumika.
 
By ANGUS SHAW, Associated Press Writer
20 minutes ago



HARARE, Zimbabwe - President Robert Mugabe was sworn in for a sixth term Sunday, just hours after government officials said he overwhelmingly won a runoff that has been widely discredited. His main rival dismissed the inauguration as "an exercise in self-delusion."

Mugabe promised talks with the opposition, perhaps mindful that African leaders will pressure him to negotiate at a summit he was to attend Monday in Egypt.

As dignitaries watched under a red-carpeted tent at the State House complex, Mugabe held a Bible and stood before a red-robed, white-wigged judge to swear to uphold his nation's laws "so help me God." He then sat amid cheering to sign documents.

"The inauguration is meaningless," Morgan Tsvangirai, leader of the opposition Movement for Democratic Change, told Associated Press Television News. "The world has said so, Zimbabwe has said so. So it's an exercise in self-delusion."

Tsvangirai said he believed members of Mugabe's ZANU-PF party were ready for talks.

"I think that the reality has dawned on all the elites in ZANU-PF," Tsvangirai said. "Without negotiating with the MDC this is a dead-end."

The 84-year-old Mugabe, Zimbabwe's leader since independence from Britain in 1980, was expected to depart almost immediately for an African Union summit that opens Monday in Egypt.

In a speech following his swearing-in, Mugabe said: "Sooner or later, as diverse political parties, we shall start serious talks." He also had promised talks on the eve of the vote.

African and other world leaders have condemned Friday's election, in which Mugabe was the only candidate. Human rights groups said opposition supporters were the targets of brutal state-sponsored violence during the campaign, leaving more than 80 dead and forcing some 200,000 to flee their homes.

Residents said they were forced to vote by threats of violence or arson from Mugabe supporters who searched for anyone without an ink-stained finger — the telltale sign that they had cast a ballot.

Tsvangirai had withdrawn from the race because of the violence, though his name remained on the ballot and his supporters may have spoiled their ballots rather than vote for Mugabe.

The electoral commission said total results showed more than 2 million votes for Mugabe, and 233,000 for opposition candidate Morgan Tsvangirai. Turnout was put at about 42 percent, and 131,000 ballots had been defaced or otherwise spoiled, apparently as an act of protest. Neither candidate got credit for the spoiled ballots.

In the opposition stronghold of Bulawayo, official results showed Mugabe got 21,127 votes and opposition candidate Morgan Tsvangirai had 13,291, while 9,166 ballots were spoiled.

A high number of spoiled ballots had been noted earlier Sunday by Marwick Khumalo, a member of parliament from Swaziland who led a team of election observers from across the continent under the auspices of the AU-sponsored Pan-African Parliament.

Khumalo said some ballots were defaced with "unpalatable messages." He refused to elaborate, but left the impression the messages expressed hostility toward Mugabe, who has been accused of ruining Zimbabwe's economy and holding onto power through fraud and intimidation.

Tsvangirai won the most votes in the first round of presidential voting in March, but not enough for an outright victory. Official results were not released for more than a month after that vote.

In recent days, African mediators have been pushing for Mugabe and Tsvangirai to negotiate a power-sharing agreement.

Mugabe said on the eve of Friday's vote that he was open to talks but pressed ahead with the election, apparently hoping a victory would give him leverage at the negotiating table.

Khumalo, the observer, urged African and regional leaders to "engage the broader political leadership in Zimbabwe into a negotiated transitional settlement."

With the election discredited and attention turning to the possibility of negotiations, the role of Mugabe in any future government could be a sticking point.

Tsvangirai said in an interview with The Sunday Telegraph of Britain that Mugabe might be allowed to stay on as ceremonial president of a transitional government, with himself as executive prime minister.

"It's being considered within our structures," the paper quoted Tsvangirai as saying.

Mugabe, 84, was once hailed as a post-independence leader committed to development and reconciliation. But in recent years, he has been accused of ruining Zimbabwe's economy and holding onto power through fraud and intimidation.

The official inflation rate was put at 165,000 percent by the government in February, but independent estimates put the real figure closer to 4 million percent.

Since the first round of elections, shortages of basic goods have worsened, public services have come to virtual standstill, and power and water outages have continued daily.
 
Hata Mugabe alipoua watu 20,000 miaka ya 80, kina Nyerere walimpetesha. Kwa nini?

bongo aliwauwa wafungwa kwa marungu tena hadharani na mpaka leo
anadunda. au kwa vile walikuwa wafungwa? au tumesahau na hili?
 
Hivi Kibaki alipoapishwa kuna aliyekwenda kushuhudia uapisho au?

unadhani suala la kuapishwa siku hizi ni dili mkuu? mradi jaji mkuu yupo jamaa
anaapishwa. pia inategemea jongwe atamualika nani. je mwenyekiti wa au ataalikwa? mimi sijui.
 
Interesing Observer,

Mkuu labda bado hujanielewe..
Yaliyoandikwa na MDC ni kauli mbiu ambayo haiwezi kuchukuliwa kama ni ukweli wa sera na malengo ya chama hicho sawasawa na Mugabe na hiyo ZANU PF ambao waliichukua ardhi kwa kutumia sera kama au zinafanana na hizi za MDC lakini walichokifanya ZANU PF ktk utekelezaji wa azma hiyo ni tofauti kabisa....Ardhi imepewa viongozi na baadhi ya watu waliojulikana kama wapigania Uhuru. je, kuna ubaya kusema au kuona kwamba Morgan atawapa wazungu!.. Mugabe aliweza vipi ashindwe Morgan!
Hili ndio kosa la kimsingi tunalokubaliana sote kuhusu Mugabe kuwapa watu wake ardhi hiyo na hakuna sehemu nimesema Mugabe hakukosea au hakuwa na nia hiyo..Tuliomfahamu tulitegemea hili kutokea lakini bado haipotoshi ukweli kwamba ardhi ile ilitakiwa kupewa wananchi kwa kuunda sheria mpya ya umilikaji wa ardhi iliyokuwa koloni la kudumu la Muingereza..

Ni kwa sababu hii hii nasema kwamba hiyo kauli mbiu ya MDC haina ukweli wa kile wanachokusudia kukifanya...Na ushahidi ulikwisha tolewa siku nyingi na viongozi wa ISO ambao walipingana na MDC ktk swala la ardhi...
Wakuu nitarudia kusema maneno ya Mtu mzima huko nyuma kasema kwamba hata CCM wanasema MAISHA BORA kwa kila Mtanzania!...ni maneno ya kuvutia sana na yenye kila sifa, upendo kwa wananchi lakini Je kweli CCM wanafanya hayo?... Na kama hapana basi ndio sababu inayotupa sisi pumzi ya kuzungumza ubaya wa chama hiki. Ni empty promises za viongozi wa Kiafrika.
Morgan pamoja na chama chake cha MDC wanaelewa wazi kwamba Zimbabwe haiwezi kuinuka kiuchumi kama hawatarudisha ardhi hiyo.. Hizi zote ni siasa kama Mugabe alivyoitumia ardhi hiyo hiyo kuchukua tena ushindi wa kimbunga.

Kwa hiyo mkuu mimi hapa najaribu kutazama swala la ardhi kama ndio issue kubwa ya Mapinduzi ya Zimbabwe na nitawakumbusha kwamba chanzo cha haya yote ni Muingereza mtake msitake..

1. Katika makubaliano ya kusimamisha vita ambayo Ian Smith alikuwa akishindwa, ZANU, ZAPU na kile chama cha kina Sithole walikubaliana na Muingereza kusimamisha mapambano kwa ahadi ya kuigawa upya ardhi sawa kwa wananchi wake wakitumia kigezo tofauti iliyopo kutokana na rangi..
2. Utawala wa Ian Smith ulidai financial compensation kwa wananchi wake (wazungu) ambao wangepoteza ardhi hizo.. baada ya makubaliano haya kuwa ni reason of breach of title deed ambazo zinatambulika kisheria..
3. Muingereza alikubali kulipa ktk miaka 20 ifuatayo na hakutimiza ahadi hiyo hadi mwisho wa miaka 20.
4. Now, kwa mzungu bado anayo right ya ile ardhi kwa sababu compesation haikutokea - na Mweusi aliona haki yake ya kusimamisha vita imekufa.. kwa sababu hawakupigana kutafuta Uhuru kwa sababu ya kutawala nchi isipokuwa haki ya wananchi wote kumiliki ardhi.
5. Mugabe na baraza zima la bunge lao walipitisha kuchukuiliwa kwa ardhi hiyo toka kwa wazungu na kuwa chini ya serikali...

Toka hapo Zimbabwe ilianza kuwa na mgogoro wa kisiasa na kiuchumi. Ni Muingereza ambaye hakutimiza ahadi yake . kisha ni Muingereza huyu huyu baada ya uamuzi wa kuchukua ardhi aliyeshinikiza kuanzishwa kwa MDC dhidi ya ZANU PF....Morgan hakuwahi kuwa Politician hata siku moja, isipokuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi.. Mnakumbuka chama cha FORD Kenya kilichoanzishwa na kupewa misaada na Marekani?..
Mimi kama mkazi wa nchi magharibi naelewa fika siasa za nchi hizi kupandikiza mtu ama kikundi cha watu ktk nchi zenye viongozi wasiokubaliana na matakwa yao, na nilipoisoma ile report ya ISO Zimbabwe nilishtushwa sana. MDC waliwafukuza viongozi wote wa ISO kwa madai kuwa walikuwa wamekiuka taratibu na sheria za chama kutoa habari za ndani ya chama nje! MDC hawakukana malalamishi ya ISO na ndipo Mugabe alipodakia hoja hiyo na kuifanya issue kubwa ktk uchaguzi uliofuata.... sound familiar?.. siasa za kiafrika..

Kwa hiyo hata tukitazama vipi swala la Zimbabwe, bado Mugabe ni mshenzi mbovu kama viongozi wengine ambao hatutaki kabisa kuwatazama.. hao kina Morgan na MDC.. hakuna chunvi ktk maneno yangu na nitarudia kusema mtakuja nambia siku moja kuwa Mkandara alisema haya!..
Imani yangu nina hakika hata kusema kuwa Tulikosea sana - mtashindwa kwa sababu ndio utamaduni wa Mdanganyika..Utumwa wa akili bado ni kilema kikubwa kwetu.

Hata yule Kilema wa miguu mara nyingi hatakiwi kuitazama ajali iliyosababisha ulemavu wake lakini hapa nashangaa kabisa watu wanapotetea kuwa ni lazima ukubali ulemavu wako na kushindwa kwako kuruka mfereji hautokani na ajali ile...Kama wewe ni kilema nani alikwambia uruke mfereji even if it is the only way through!..
That's why mjadala huu umesimama tu kumtazama kilema mbishi Mugabe akijaribu kuruka mfereji wakati mimi nazungumzia kuwa sii tu ni kilema isipokuwa hawezi kuruka mrefeji huo kilema chake ni kikubwa kilitokana na ajali blaa blaaa blaaa!..
 
Fundi Mchundo,

..huyo Mandela alikuwa wapi siku zote anakuja kusema leo? alikuwa wapi wakati wa-Congo milioni 3 wanakufa? ni hilo disco analopigiwa huko London ndiyo limemfanya aseme?

..nimeuliza kule inakuwaje Mugabe ambaye aliweza kuendesha uchumi ukakua hata kwa double digits leo hii agueze nchi kuwa mufilisi?

..pia inakuwaje nchi ambayo inakabiliwa na janga la njaa ikawekewa vikwazo na vyombo vya fedha, na zaidi ikalazimishwa kulipa madeni yake on time?

..kuna ripoti zinazomnukuu Mtanzania Peter Ngumbula, aliyekuwa head wa African desk IMF, akilalamika kwamba Zimbabwe imenyimwa fedha za budjet support kwasababu za kisiasa.

..sikumsikia Mandela, Askofu Desmond Tutu, Askofu Sentamu,...wakilaani ukatili huo wa vyombo vya fedha vya kimataifa. ndiyo maana wengine tunaona hawa wamekuwa kama vibaraka.

..kwa yeyote yule ambaye amejisumbua kufuatilia historia ya Zimbabwe, lazima ataelekeza lawama kwa wote[Mugabe,Tsivangarai,Tony Blair,ZANU,MDC,Labor Party] wanaohusika na mgogoro huu kwa kutufikisha hapa tulipofika.

..ni uhuni kwa chama cha Upinzani kupiga kampeni kwa wafadhili ili serikali iliyoko madarakani ikatiwe misaada, kwa nia ya kuifanya ichukiwe na wapiga kura, ili kukiwezesha chama cha upinzani kuingia madarakani. hicho ndicho walichofanya MDC for more than 10 yrs.

..NAOMBA NIMALIZE KWA KUSEMA KWAMBA HALI YA KISIASA IMECHAFUKA MNO ZIMBABWE KWA SASA HIVI. ZANU NA MDC WANAHUSIKA MOJA KWA MOJA KWA SIASA CHAFU ZA KUWAGAWA WANANCHI.

..KWA MAONI YANGU NI BORA JESHI LITWAE MADARAKA ZIMBABWE. SHUGHULI ZA SIASA ZISIMAMISHWE, NA BADALA YAKE SERIKALI YA MPITO IJIELEKEZE KTK KUTATUA MATATIZO YA KIUCHUMI YA ZIMBABWE.
 
..KWA MAONI YANGU NI BORA JESHI LITWAE MADARAKA ZIMBABWE. SHUGHULI ZA SIASA ZISIMAMISHWE, NA BADALA YAKE SERIKALI YA MPITO IJIELEKEZE KTK KUTATUA MATATIZO YA KIUCHUMI YA ZIMBABWE.

..hilo jeshi ndio chanzo cha mugabe kung'ang'ania madaraka.

..halafu hayo matatizo ya uchumi yatatatuliwaje ikiwa hali ni kama ulivyoisema.
 
naamini ile move ilikuwa political blunder ambayo imechangia kuongezeka
kwa imani kwamba jamaa ni stooge. kama ambavyo mbio zake za kukimbilia
ubalozini hapo majuzi
.

..wako viongozi wengi ambao ni stooge,tena wengi wao wako madarakani. wanatofautiana mabwana wanaojipendekeza kwao tu.

..ungekuwa wewe ungekimbilia wapi?
 
Dar Si Lamu,

..ikiwekwa serikali ya mpito ya ZANU-MDC basi wataishia kupika siasa kwa ajili ya uchaguzi unaokuja.

..huu mgogoro umegeuka kuwa personal kati ya Mugabe na Tsivangarai na ndiyo maana naona wakae pembeni.

..hata kama jeshi litachukua madaraka nategemea halitahusisha yeyote aliyekuwa black-listed na nchi za magharibi.

..kuna hatari ya war veterans kuchukua silaha and make the county un-governable ikiwa MDC watachukua madaraka.

..pamoja na hayo yote Zimbabwe inahitaji msaada wa dharura wa fedha ili kupooza makali ya uchumi.

NB:

..hivi wakina Gordon Brown wanaopendekeza Mugabe aondolewe kwa nguvu za kimataifa za kijeshi wanatarajia nani ataongoza badala yake?

..au wataweka Transition Authority kama ile ya Ambassador Paul Bremer kule Iraq?
 


..sidhani,kinachoonekana ni mugabe kushindana na west ili kuwaonyesha yeye bado ni kidume,at the expense ya wananchi.

..haliwezi. halafu lenyewe ndio chochezi wa mambo haya yote.

..war vets hawana nguvu yeyote kama hawapati msaada wa jeshi au polisi. pili,under current settings mdc hawawezi kuongoza nchi wenyewe. tatizo ni jeshi and company.

..sijui.

..labda,kama sadc na au watakubali. but,it's not necessary.
 
Nimeanza kuamini kabisa kuwa pengine wengi wa wachangiaji hawamfahamu Robert Mugabe. Upepo wa mabadilko ulipoifikia Rhodesia, Joshua Mqabuko Nyongolo Nkomo alianzisha chama cha NDP mwaka wa 1960 kudai uhuru na baadaye akaungwa mkono na Robert Mugabe. NDP ilipopigwa marufuku Nkomo na Mugabe wakaanzisha ZAPU mwaka 1962. Mwaka 1964 Nkomo pamoja na Ndabaningi Sithole, Edgar Tekere, Maurice Nyagumbo na Robert Mugabe walitiwa kizuizini na serikali ya Ian Douglas Smith.

Baada ya kuachiliwa mwaka 1974 kulitokea mfarakano uliomfanya Sithole na Mwanasheria Herbert Chitepo, kuanzisha ZANU. Wakati wa vita vya ukombozi viliyojulikana kama "Rhodesia Bush War" ZAPU ilifanya mashambulizi kutoka Zambia na ZANU kutoka Msumbiji. Chitepo alipouwawa mwaka 1975, Robert Mugabe alijitwalia uongozi wa ZANU. Sithole alikuja kujiunga na serikali ya mseto kati ya Ian Smith na Bishop Muzorewa mwaka 1979 baada ya uchaguzi ambao haukutambuliwa na nchi yoyote zaidi ya Afrika Kusini.

Mfarakano kati ya ZAPU na ZANU ulitokana na mambo makubwa mawili. La kwanza lilikuwa ni namna ya kupambana na mokoloni. Nkomo hakutaka kamwe kuwe na suluhu yoyote na Wazungu lakini Mugabe kama ilivyokuja kutokea baadaye aliwakumbatia kwa kiwango fulani. Inasemekana Kuna mazungumzo ya siri yaliyofanyika kati ya Mugabe na Smith ambayo hadi leo hakuna anayejua kilichozungumzwa. La pili lilisababishwa kwa kiasi na tofauti kati ya makundi mawili makubwa ndani ya Zimbabwe - Watebele walio wachache na Washona ambao ni wengi. Mugabe aliweza kumshinda Mkomo kwa kuungwa mkono na Washona.

Nkomo was appointed to the cabinet, but in 1982 was accused of plotting a coup d'état after South African double agents in Zimbabwe's Central Intelligence Organization, attempting to cause distrust between ZAPU and ZANU, planted arms on ZAPU owned farms, and then tipped Mugabe off to their existence.

In a public statement Mugabe said, "ZAPU and its leader, Dr. Joshua Nkomo, are like a cobra in a house. The only way to deal effectively with a snake is to strike and destroy its head."[4]

He unleashed the Fifth Brigade upon Nkomo's Matabeleland homeland. More than 20,000 Ndebele civilians were killed by Mugabe's North-Korean trained 5th Brigade during the Gukurahundi (“the early rain that washes away the chaff”) ethnic massacres.Their leader was Perence Shiri who called himself 'Black Jesus'. Mugabe is said to fear prosecution for this massacre, with bills calling for inquiries into the incident sometimes introduced into Parliament. The opposition Movement for Democratic Change has said that if it comes to power, it will call for an international trial of the massacre. Most of the 20,000 killed were innocent civilians.
 

Tanzania na Afrika walisimama wapi kuhusu hili, miaka hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…