Unajua Wadanganyika mnacheklesha sana...
Nyerere alipokuwa akitumia siasa za UJAMAA alitupeleka karibu kuwa taifa lisilojiweza kiuchumi.. Hapo ni sisi tuliyefunga milango ya kiuchumi kwa nchi nyingine na tulifikia mahala tuanze kula nyama za watu....
Leo Mugabe kafungiwa yeye milango yua kiuchumi mnafikiri ataweza kufanya nini kama sisi ndani ya Ujamaa tulishindwa!..Nitarudia kusema hivi kila kitu kinachoweza kuota Zimbabwe bila mbegu ya mzungu...ardhi imekwisha haribika kwa hizo mbegu za maabala..
Kisha ebu jaribuni kufikiria kitu kimoja, leo hii Tanzania tufungiwe kila kitu kutoka nje... nambie huko madukani kutakuwa na nini... Hata unga wa ngano tunaagiza, mchele,... jamani siku hizi ktk kila chakula chetu kuna kitu kinatoka Ulaya hata mkate utahitaji amira kama huna mkate hauwezi kupikika..
Nitarudia kusema kwamba binafsi namlaani Mugabe kwa vitendo vyake lakini siwezi kusukumwa na mzungu kwa vigezo vyake!..
Swala la Zimbabwe ni kubwa kuliko Mugabe peke yake ingawa ni bora sana akitoweka lakini haiwezi kurudisha amani nchi hiyo hadi haki na ardhi ya mzungu imepatikana.
nachowaomba mnambie ni ushauri wenu kwa jinsi mnavyoiona Zimbabwe ya kesho... mathaln akitoka Mugabe mtazamo wenu ni nani atawale?...hapo nawaomba mzingatie tu ya kwamba Mugabe akiondolewa kwa mabavu, basi mjue Zimbabwe ni Somalia nyingine ambayo kwa miaka 17 haina serikali. Wamekwisha kufa watu zaidi la laki 5..
Je, hii ndio Zimbabwe mnayoiombea?..Kama sio basi nambieni kile mnachokiona nyie na mimi sikioni..
Interest za mzungu zinajulikana, tuwaache nje tuzungumze sisi kama waafrika! nipeni solution ambayo hata Membe anaweza kuipendekeza kwa Mugabe na serikali yake..
Nachosema mimi suluhu ya swala la Zimbabwe ni kumwomba Mugabe akae pembeni tu na mtu mwingine ndani ya ZANU PF ashike madaraka hali wakijua kabisa kuwa vikwazo havitaondoka..nje ya hapo mauaji yataendelea na pengine kuhatarisha zaidi usalama wa nchi zote kusini mwa jangwa!