Wenye nyumba kuweni waelewa

Wenye nyumba kuweni waelewa

Kuna muda wapangaji wenyewe wanazingua,nimempangisha dogo mmoja na mkewe wanajitafuta kimaisha.Maana hata sielewi wanachofanya,hajalipa Kodi yangu zaidi ya miezi minne sasa juzi naliuliza hela yangu vipi January hii lilivyokosa akili linanipandishia eti kuna wapangishaji wengine wanakaa hata miezi sita bila kusumbua nimeliambia ikifika tarehe 31 nisimuone.Hakuna asiyeelewa hali ya maisha ilivyo lakini ukishindwa kutimiza wajibu wako uwe hata na busara.
haaa sasa huyo kazingua mimi nimeomba wiki 3 kabla ya tarehe yangu
 
Wapangaji wengine wasumbufu.

Mfano, kodi inaisha tarehe 30, tareh 1 inabidi unilipe, inafika tareh 1 kimya, 2,kimya, 3,4,5 mpaka nakucheki mzee vipi kimya ndio anakwambia ooh, ana changamoto kidogo alikuwa anataka kukutafuta akueleze umvumilie, huyo utamuelewa kweli, kama umekwama we nipange mapemaa, tena ikiwezekana hata kabla ya tareh 30, kwenye 20+ huko niambie tu huelewi elewi, mie nakuwa najua kabisa kipi kinajiri. Sio ukae kimya tarehe 1 inafika na tena inavuka mpaka mie nikucheki.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wenye nyumba acheni usumbufu ebooo.
 
habari zenu,

wenye nyumba zenu mliopangisha na mpo humu, hebu kuweni waelewa muda mwingine jamani..

mtu anakulipa kodi siku zote on time bila maneno wala kelele, amekwama mwezi mmoja anaomba umvumlie hutaki kuelewa khaa.

hakuna mtu anapenda kudaiwa kila mpangaji anajua wajibu wake wa kulipa kodi ila kuna muda mipango sio matumizi muwe mnaelewa..

maisha hayapo hivyo jamani kuna kupata kuna kukosa mtu akikwama muwe mnawaskiliza..

wapangaji nao ni watu wanapaswa kusilizwa sio kuwanyanyasa…

msinichambe..
Hakuna cha kuelewa, zipo nyumba za bure za serikali. Nenda ustawi wa jamii.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wenye nyumba acheni usumbufu ebooo.
Kuna wapangaji wengine nao miyeyusho amini mimi maneno yangu.
Ukikwama toa tu taarifa mapema tu, kuna wengine mapemaa anasema mie mwezi huu hovyo, na tunaelewa sababu si wote tunahangaika na haya maisha kuna kipindi byee kuna kipindi ni tee kabisa.
 
Back
Top Bottom