Kwanini wenye nyumba wanalazimisha wapangaji walipe Kodi kwanzia miezi 6?

Kijana LOGICS

Senior Member
Dec 16, 2023
140
525
Kumetokea wimbi la wenye nyumba kutaka Kodi ya miezi 6 kwa mkupuo wengine wanataka hadi ya mwaka mzima

Mfano Mimi nalipia Kodi 150,000 mwenye nyumba huaa hapokei Kodi ya mwezi mmoja anasema Kodi lazima nilipe miezi 6 au mwaka mmoja

Ukiangalia ulipwaji WA fedha/Kodi haumpi mpangaji guarantee ya fedha Anayolipa

Mfano mpangaji akipata dharura akitaka Kuhama mkoa hakuna kipengele Cha kurudisha Kodi.

Mpangaji akifariki kama hakua na MTU WA Karibu wakati WA kusain mikataba hizo fedha zinapotea .

Nishauri Wenye nyumba waruhusu wapangaji waamue ulipwaji wakodi ili haki itendeke.
 
Huu mtindo wa kulipia miezi mingi ya mbeleni si mzuri kwa mpangaji. Saa yoyote unaweza kughairi kuendelea kupanga nyumba hiyo kama itatokea vitu vya kukera au dharura yeyote ile, unakuta unaacha hela nyingi kwa mwenye nyumba.

Hii ni hasara, bora kulipa mwezi mmoja mmoja tu, ukiona mazingira hayaridhishi unaondoka. Kulipia pango miezi mingi ni utapeli tu
 
Ni ujinga kulipia miezi ambayo huna uhakika wa kuishi kwenye hiyo nyumba.

Wizara yenye dhamana inapaswa kuliangalia hili upya, hata kumlipa dalali mwezi mmoja ni wizi.

Kama inawezekana kukodi chombo cha usafiri kwa kupitia Application kama bolt imeshindikana nini wenye nyumba kulazimishwa kutangaza nyumba zao kupitia mitandao rasmi na wateja wapatikane huko na kodi ya Serikali ilipwe?

Kuna kodi inapotea, Madalali hawalipi kodi ukimpa laki 1 yake anaenda kulewa tu hiyo kazi kazi amefanya lakini Serikali haijakusanya kodi.
 
Ni ujinga kulipia miezi ambayo huna uhakika wa kuishi kwenye hiyo nyumba.

Wizara yenye dhamana inapaswa kuliangalia hili upya, hata kumlipa dalali mwezi mmoja ni wizi...
Hapa utasikia wanakuambia "kuna watu wanalisha familia kupitia hizo kazi za udalali sasa zikipigwa marufuku waende wapi", yani mwanaume mzima anaacha kutafuta kazi ya kueleweka analilia kula hela za wanaume wenzie burebure tu, kama mtu hajawahi kukutana na utapeli wa madalali anaweza akawatetea hao watu
 
Maoni yangu

1.Suala la kulipa Kodi eidha kwa mwezi/miezi 6 au Mwaka 1 liwe hiari ya mpangaji mwenyewe,lisiwe suala la lazima kwa wamiliki wa nyumba!.

2.Madalali hawakwepeki kwasababu wanasaidia sana,lakini suala la dalali kulipwa liwe chini ya mwenye nyumba kwasababu yeye ndiye anamtafutia mteja hivyo mwenye nyumba ndiye anapaswa au awajibike kumlipa!.

3.Hayo mambo mawili yanapaswa kuwekewa mkazo na sheria kali!.

Bado sijajua serikali yetu inawasaidiaje wananchi wake kwasababu zimebaki porojo na siasa tu!.

Mengineyo!

1.Unakuta mpangaji akinunua umeme anakatwa ile kodi ya Jengo (Ilikuwa 1000 lakini sasa hivi ni 1500)

Hii kodi wenye nyumba nyingi hawahusiki nayo tena wakati majengo ni yao,huu mzigo unaenda kwa mpangaji ambaye nyumba si yake,anaponunua umeme anakatwa juu kwa juu sheria ilipaswa ipitishwe na iwe kali ya kwamba,hiyo kodi iwe ndani ya ile kodi ya mpangaji na mwenye nyumba ailipe yeye au kama mpangaji akiilipa basi mwenye nyumba amrudishie!.

Unakuta Mwenye nyumba anaishi mbali na hivyo mpangaji anaona kuanza kumtafuta kisa 1500 ni kero,anaona bora ailipe tu kuondoa usumbufu na kero!

Watanzania wengi wanapata mateso sana kwasababu serikali yao niyakisenge sana!
 
Nikupangishe mwezi mmoja kwa 150,000 au 300,000 ukitoka ushaharibu vitu kadhaa,mwingine akiingia lazima ufanye marrkebisho madogo.

Hio 150k yako si itaishia kwenye marekebisho? Sasa hio si biashara kichaa?

Sheria ya serikali haitakiwi kuzidi miezi mitatu, miezi 6+ inaleta utulivu kwa mpangaji na mwenye nyumba.
 
Mkuu mara nyinyi wenye nyumba hufanya hivo ili wasisumbuane na mpangaji kila mwezi kodi kodi hata wew kuna unafuu ukishalipa kodi una relax kdg kufatilia mambo mengn

Welcome to capitalism, nyumba yake, sheria zake...

Wewe kama hutaki hizo sheria, jipange ujenge mjengo wako...
Issues sio capitalism tunataka haki itendeke
 
Nikupangishe mwezi mmoja kwa 150,000 au 300,000 ukitoka ushaharibu vitu kadhaa,mwingine akiingia lazima ufanye marrkebisho madogo
Hio 150k yako si itaishia kwenye marekebisho? Sasa hio si biashara kichaa?
Sheria ya serikali haitakiwi kuzidi miezi mitatu, miezi 6+ inaleta utulivu kwa mpangaji na mwenye nyumba.
Hiyo ni nadharia nyumba inaharibika VP
 
Exa
Maoni yangu

1.Suala la kulipa Kodi eidha kwa mwezi/miezi 6 au Mwaka 1 liwe hiari ya mpangaji mwenyewe,lisiwe suala la lazima kwa wamiliki wa nyumba!.

2.Madalali hawakwepeki kwasababu wanasaidia sana,lakini suala la dalali kulipwa liwe chini ya mwenye nyumba kwasababu yeye ndiye anamtafutia mteja hivyo mwenye nyumba ndiye anapaswa au awajibike kumlipa!.

3.Hayo mambo mawili yanapaswa kuwekewa mkazo na sheria kali!.

Bado sijajua serikali yetu inawasaidiaje wananchi wake kwasababu zimebaki porojo na siasa tu!.

Mengineyo!

1.Unakuta mpangaji akinunua umeme anakatwa ile kodi ya Jengo (Ilikuwa 1000 lakini sasa hivi ni 1500)

Hii kodi wenye nyumba nyingi hawahusiki nayo tena wakati majengo ni yao,huu mzigo unaenda kwa mpangaji ambaye nyumba si yake,sheria ilipaswa ipitishwe na iwe kali ya kwamba,hiyo kodi iwe ndani ya ile kodi ya mpangaji na mwenye nyumba ailipe yeye au kama mpangaji akiilipa basi mwenye nyumba amrudishie!.

Watanzania wengi wanapata mateso sana kwasababu serikali yao niyakisenge sana!
Exactly well said
 
Unakuta mpangaji akinunua umeme anakatwa ile kodi ya Jengo (Ilikuwa 1000 lakini sasa hivi ni 1500)

Hii kodi wenye nyumba nyingi hawahusiki nayo tena wakati majengo ni yao,huu mzigo unaenda kwa mpangaji
Mnamuendekeza faza/ maza house wenu.. yan mmekosa lugha ya kumpa? Hehee

Wa kwetu anailipa ya mwaka mzima. Na anailipa kwa kutununulia umeme
 
Inategemea na mwenye nyumba, Nina rafiko yangu aliachiwa nyumba ya urithi eneo potential kinoma Lina fremu zimezunguka zipo zaidi ya 30, huyu jamaa hataki stress ye ni mtu wa kula bia tu....

Kinachonichekesha jamaa anapokea Kodi ya mwezi mmoja mmoja tu, yaani hata umuue hawezi kukubali umlipe zaidi ya mwezi, alafu wapangaji tarehe zinapishana yaani karibu Kila siku anapitia maokoto tu... Niliwahi kumuuliza akadai mambo ya kupewa hela miezi sijui 6 zikiisha unaweza kupauka kweli mpaka mzigo uje tena
 
Bora tz unalipia 6months unarelax, nchi zingine ambazo wanalipa kila mwezi lazima mwanzo kuna safety deposit depending na finishing ya nyumba unaweza lipia deposit kodi ya 6months halafu ndo unaanza mmoja mmoja. Hii yetu ni nzuri na ukifikiria mwenye nyumba ndo anabeba risk kubwa kwa system ya kodi miezi 6.
 
Mnamuendekeza faza/ maza house wenu.. yan mmekosa lugha ya kumpa? Hehee

Wa kwetu anailipa ya mwaka mzima. Na anailipa kwa kutununulia umeme

Mkuu mimi nina kwangu nimejenga,nilichokiandika hapo ni maisha ya marafiki,ndugu na jamaa zangu wanachopitia,na ukiacha hivyo hata mimi nimewahi kuwa mpangaji hivyo yote yapo kama yalivyo!
 
Back
Top Bottom