Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,056
- 10,596
Wakiweka website mnawachunguza sana, nondoz zao zote wanazoziweka mnazisoma kwa makini sana. Tangu Mwanakijiji awawashie moto Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, sidhani kama kuna wizara au idara ya serikali itakuwa inaanika nondo zake kwenye website yake, maana ni kama vile unajitakia kesi. Mtindo mpya wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ni kuweka percent za mikopo tu bila kuweka figures maana wameona ulaji wao unaweza kuyeyuka ivi ivi sababu ya uchunguzi wa akina Mwanakijiji!
Labda suala jingine la kujadili ni kuwa kwa nini tovuti nyingi za sirikali ziko kwa lugha ya kigeni? Je hii ni makusudi kuwanyima wasiojua lugha hii fursa ya kujua undani wa sirikali yao ama kuna agenda nyingine ya siri?
Naomba ufafanuzi tafadhali wana JF.