We mwanamke inakuwaje unatandikiwa kitanda?

If I can put it this way,....nyumbani kwangu ni hoteli ndogo na baadhi ya watu wana kofia zaidi ya moja....

Does that satisfy you??

Sasa na wewe tueleze, tofauti ya wafanyakazi wa hotelini na nyumbani ni ipi?

Mind you, kuna nyumba zinaajiri wafanyakazi ambao wa wa taaluma ya kutunza nyumba (professional house keepers)!!

Babu DC!!

hii imekaa kinadharia zaidi ya vitendo mkuu!

yes! i know well and am aware of professional house keepers ,and they are good in what they are doing lakini still i cant compare my house na hotel...... nyumba yangu inaheshima yake na mahusiano yaliyopo nyumbani ni tofauti na ya hotelini( meaning client vs wahudumu) ,never the same and will never be the same.
 
Aisee umejieleza vizuri sana cacico nakubaliana na wewe kwa asilimia zote ila hapo mwisho tu ndio umenishangaza. Muwachwe mupumuwe kwakuwa mkitandika vitanda mnabanwa pumzi sio?

Kusaidiana sio tatizo kwakweli na ndio maana unaona hata mumeo ni yeye mwenyewe aliamua kukupumzisha baadhi ya majukumu pamoja na kwamba wewe mwenyewe hukuwa umekataa kufanya hivyo.Tatizo liko kwa hawa mnaojiita modern wife mnajaribu kila njia kubadili nyeusi kuwa nyeupe na hapo ndipo pagumu na mwanzo wa matatizo ya ndoa.

Btw, mumeo kumbe yuko gado kinoma, kila siku lazima atikise wavu 3-0!!!:smile::smile::smile:
kitanda twapeana zamu anayewahi kuamka, dada anaingia nikiwepo weekend na PAPA LAKE NAMPA MARA 4, HIYO NI RESOLUTION YANGU KWA MWAKA 2013, NO UBAHILI KWENYE AMANA YAKE, MUACHE ALEEEEEE MPAKA AKINAI!!

BEKI 3 ATAFANYA USAFI,. ILI NIWEZE KUWAJIBIKA PANAPO MTANANGE!! HAIHUUU KUWA UMECHOKA KLA UKIOMBWA GAME!!
 
hiyo nisawa na kuzuia mafuriko kwa beseni wangu! mimi sitaki kabisaaaaaaaa kujitoa roho wala kuumia MGONGO eti ni majukumu!! majukumu ambayo mwisho wa siku yanakuumiza we mwenyewe!! YE MWENYEWE YUPO SOOOO RELAXED, tena akiniona nimeinama huwa anagomba balaa, utasikia kwani dada ana kazi gani?? muite aje amalizie hapo, wewe kuja pande hii.......!! jamani wababa, kama ambavyo nyinyi huchoka mkitoka kwenye majukumu, na sisis ndio hivyo hivyo, muwe mnatuhurumia, ukilalamika isssue ndogo kama kutandika????? mbona kuna ya msingi ya kuongelea na kulalamika???

halafu kwa wale wenzangu na mimi tususuo tukichuchumaa, ukiwa mjamzito au umetoka kujifungua na beki tatu haingii rum kwako, si KUTAOZA HUKO NDANI??? nyie kazaneni kuonyesha mapenzi kwa kujiua migongo, wakati wenzenu wanashinda le chique kufanyiwa massage, akirudi mwepesiiiiiiii, we mgongo wakuuma, eti mapenzi NALINDA NDOA!! ZILINDENI SANA, tena wazungushieni nyaya za ULTIMATE SECURITY, haus gal akigusa anase!!

ndoa hazilindwi hivyo!!

Hapa sasa kazi inaanza,

But... kwa kweli nashindwa kuwaelewa watu wengi...at least nimemwelewa Nyamayao (ni jukumu lake), Mwita Maranya (analinda mila na pia anaogopa sudden attack za beki tatu..lol), King'asti (aethetic reasons), snowhite (mila za kwao) na baadhi ya wadau wengine...

Ila kusema kweli bado mie nawachukulia wasaidizi wa ndani kama wanangu...tunakula pamoja, tunapiga story pamoja na kwa hiyo tunasaidiana kazi zote!!

Hapo mie na bibi tunakosea wapi bandugu??

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
If I can put it this way,....nyumbani kwangu ni hoteli ndogo na baadhi ya watu wana kofia zaidi ya moja....

Does that satisfy you??

Sasa na wewe tueleze, tofauti ya wafanyakazi wa hotelini na nyumbani ni ipi?

Mind you, kuna nyumba zinaajiri wafanyakazi ambao wa wa taaluma ya kutunza nyumba (professional house keepers)!!

Babu DC!!

Mzee mzima hotelini kunafanyika biashara ya kuuza na kununua, kama nyumbani kwako nako ni hoteli ndogo bila shaka utaratibu ni ule ule wa kuuza na kununua.

Kwa kufafanua swali la mdau nani ni mteja hapo hoteli ndogo?
 
Aisee umejieleza vizuri sana cacico nakubaliana na wewe kwa asilimia zote ila hapo mwisho tu ndio umenishangaza. Muwachwe mupumuwe kwakuwa mkitandika vitanda mnabanwa pumzi sio?

Kusaidiana sio tatizo kwakweli na ndio maana unaona hata mumeo ni yeye mwenyewe aliamua kukupumzisha baadhi ya majukumu pamoja na kwamba wewe mwenyewe hukuwa umekataa kufanya hivyo.Tatizo liko kwa hawa mnaojiita modern wife mnajaribu kila njia kubadili nyeusi kuwa nyeupe na hapo ndipo pagumu na mwanzo wa matatizo ya ndoa.

Btw, mumeo kumbe yuko gado kinoma, kila siku lazima atikise wavu 3-0!!!:smile::smile::smile:

Hapa ni shule Poti,

Mtu akitoka hapa bila ku-upgrade au ku- make up ndo basi tena....

Nadhani sasa unaanza kuona kuwa kuna mazingira na mazingira kaka Mwita Maranya, ambayo yanaweza kumfanya msaidizi wa ndani afanya kazi zaidi ya matarajio ya wengi...!!

babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Mimi kwa kweli nitakuwa kinyume kidogo na wenzangu, kwa sababu siku ya kuingia ndani kwako, hasa chumbani unaambiwa hiyo ni sehemu takatifu haitakiwi mtu yoyote kuingia zaidi ya wewe na mumeo tu. Sasa Housegirl haruhusiwi kuingia sehemu hiyo , na kutandika kitanda na kufyagia chumba chako ukiwa kama mwanamke uliyeolewa ukapewa mafunzo huko kwenu ulikotoka.

Ninasema hivi kwa sababu, unajua pale kwenye uwanja wenu wa 6 x 6 ni mahala patakatifu ambapo Mungu alikuruhuru wewe na mumeo kula sakalamenti takatifu . Sasa linapokuja swala la kutandika, kuna mambo mengi kwa kweli wanawake wenzangu mnafahamu unaweza ukawa umesahau kile kitamb--- pale ambapo baba alipomaliza kula ukamf----.sasa house girl akiingia akakuta si niaibu kwako? kwa kweli tuwe waangalifu tusiwakomaze watoto wa wenzetu kabla ya muda

Pia unakaribisha ibilisi wewe mwenyewe, na kumpelekea mumeo aikaribie zinaa. hakuna dharau kubwa kama mumeo atembee na mwanamke mwingine katika kitanda chako cha ndoa.
Tujitahidi kudhibiti mianya midogo midogo kama hiyo.
 
Hapa sasa kazi inaanza,

But... kwa kweli nashindwa kuwaelewa watu wengi...at least nimemwelewa Nyamayao (ni jukumu lake), Mwita Maranya (analinda mila na pia anaogopa sudden attack za beki tatu..lol), King'asti (aethetic reasons), snowhite (mila za kwao) na baadhi ya wadau wengine...

Ila kusema kweli bado mie nawachukulia wasaidizi wa ndani kama wanangu...tunakula pamoja, tunapiga story pamoja na kwa hiyo tunasaidiana kazi zote!!

Hapo mie na bibi tunakosea wapi bandugu??

Babu DC!!
NASHANGA Babu DC!! NASHANGA mjukuu wako, hebu tuendelee kusikiliza labda tutaelewa! SIJICHOSHI KABISAAAAAAAAAA, ETI NAOGOPA BEKI 3!! atafanya usafi nikiwepo, si kumuachia chumba changu, hiyo nimekataa!! ila SIJIUMIZI PIA KWA KUWA ETI 'NIMEOLEWA'!!
 
Last edited by a moderator:
nimewaambia wanaolinda ndoa zao, WAWAZUNGUSHIE WAUME ZAO NYAYA ZA UMEME ZA ULTIMATE SECURITY, mabeki 3 wakigusa wanase wafe, kama kwa akili zao za kutandika kitanda ndio wanalinda! wenzao wanawagonga store wakati wa kutoa unga wa ngano, na kichapo hukohuko!!

Hapa sasa unataka kupotosha mjadala cacico. Kutandika kitanda kunamlazimisha beki tatu aingie chumbani kwenu. Baadhi ya watu nikiwemo mimi tunasema beki tatu haruhusiwi kuingia chumbani kwetu na tunazo sababu zetu za msingi.

La mume kuchukua beki tatu lina mambo mengi ndani yake si kutandika kitanda tu. Kama usipoweka mipaka ya kazi na majukumu kwenye nyumba yako uko katika nafasi nzuri sana ya kuharibikiwa. Sasa kama huamini kwamba wanaume ni dhaifu kwa wanawake basi we endelea tu kumuachia loose mumeo lakini siku yakikukuta usilaumu umodern wife, ukubali matokeo.
 
Last edited by a moderator:
Mzee mzima hotelini kunafanyika biashara ya kuuza na kununua, kama nyumbani kwako nako ni hoteli ndogo bila shaka utaratibu ni ule ule wa kuuza na kununua.

Kwa kufafanua swali la mdau nani ni mteja hapo hoteli ndogo?

Hivi Poti umezingatia context iliyotufikisha hapo??

Au umesahau ile kanuni yako kuwa huwezi kufanya hesabu zikapanda bila kuanza na lile neno tamu, assumption??

Mwisho wa siku, tunamtaka jamaa atueleze tofauti ya wafanyakazi wa nyumbani na hotelini??

Upo kaka??

Babu DC!!
 
NASHANGA Babu DC!! NASHANGA mjukuu wako, hebu tuendelee kusikiliza labda tutaelewa! SIJICHOSHI KABISAAAAAAAAAA, ETI NAOGOPA BEKI 3!! atafanya usafi nikiwepo, si kumuachia chumba changu, hiyo nimekataa!! ila SIJIUMIZI PIA KWA KUWA ETI 'NIMEOLEWA'!!

Unapojifungua unakuwa hauna njia nyingine ya kufanyia usafi chumba chenu zaidi ya kumtumia beki tatu?
 
mimi kwa kweli nitakuwa kinyume kidogo na wenzangu, kwa sababu siku ya kuingia ndani kwako, hasa chumbani unaambiwa hiyo ni sehemu takatifu haitakiwi mtu yoyote kuingia zaidi ya wewe na mumeo tu. Sasa housegirl haruhusiwi kuingia sehemu hiyo , na kutandika kitanda na kufyagia chumba chako ukiwa kama mwanamke uliyeolewa ukapewa mafunzo huko kwenu ulikotoka.

Ninasema hivi kwa sababu, unajua pale kwenye uwanja wenu wa 6 x 6 ni mahala patakatifu ambapo mungu alikuruhuru wewe na mumeo kula sakalamenti takatifu . Sasa linapokuja swala la kutandika, kuna mambo mengi kwa kweli wanawake wenzangu mnafahamu unaweza ukawa umesahau kile kitamb--- pale ambapo baba alipomaliza kula ukamf----.sasa house girl akiingia akakuta si niaibu kwako? Kwa kweli tuwe waangalifu tusiwakomaze watoto wa wenzetu kabla ya muda

pia unakaribisha ibilisi wewe mwenyewe, na kumpelekea mumeo aikaribie zinaa. Hakuna dharau kubwa kama mumeo atembee na mwanamke mwingine katika kitanda chako cha ndoa.
Tujitahidi kudhibiti mianya midogo midogo kama hiyo.
utasahauje kitambaa?? Moja, mbili kwani zimegeuka sprinkler kwamba hazinyonyeki ndani kunako papale!!! Tatu kwa case yangu, kabla hajaja hiyo jumamosi au jumapili kudeki, kwanini usihakikishe kila kilichopo cha siri kimewekwa sawa???? Tatu kitanda changu hagusi, twatandika wenyewe, ila usafi mwingine, hell no! Nimekataaa!
 
Mimi kwa kweli nitakuwa kinyume kidogo na wenzangu, kwa sababu siku ya kuingia ndani kwako, hasa chumbani unaambiwa hiyo ni sehemu takatifu haitakiwi mtu yoyote kuingia zaidi ya wewe na mumeo tu. Sasa Housegirl haruhusiwi kuingia sehemu hiyo , na kutandika kitanda na kufyagia chumba chako ukiwa kama mwanamke uliyeolewa ukapewa mafunzo huko kwenu ulikotoka.

Ninasema hivi kwa sababu, unajua pale kwenye uwanja wenu wa 6 x 6 ni mahala patakatifu ambapo Mungu alikuruhuru wewe na mumeo kula sakalamenti takatifu . Sasa linapokuja swala la kutandika, kuna mambo mengi kwa kweli wanawake wenzangu mnafahamu unaweza ukawa umesahau kile kitamb--- pale ambapo baba alipomaliza kula ukamf----.sasa house girl akiingia akakuta si niaibu kwako? kwa kweli tuwe waangalifu tusiwakomaze watoto wa wenzetu kabla ya muda

Pia unakaribisha ibilisi wewe mwenyewe, na kumpelekea mumeo aikaribie zinaa. hakuna dharau kubwa kama mumeo atembee na mwanamke mwingine katika kitanda chako cha ndoa.
Tujitahidi kudhibiti mianya midogo midogo kama hiyo.
Huwa mnajificha wapi na pointi nzuri namna hii? Umefafanua vema kbs wajibu wa wenye kitanda. Mwenye masikio na asikie.
huwa sijapata kutoa ruksa beki tatu kugusa chumba changu.
 
Hapa sasa unataka kupotosha mjadala cacico. Kutandika kitanda kunamlazimisha beki tatu aingie chumbani kwenu. Baadhi ya watu nikiwemo mimi tunasema beki tatu haruhusiwi kuingia chumbani kwetu na tunazo sababu zetu za msingi.

La mume kuchukua beki tatu lina mambo mengi ndani yake si kutandika kitanda tu. Kama usipoweka mipaka ya kazi na majukumu kwenye nyumba yako uko katika nafasi nzuri sana ya kuharibikiwa. Sasa kama huamini kwamba wanaume ni dhaifu kwa wanawake basi we endelea tu kumuachia loose mumeo lakini siku yakikukuta usilaumu umodern wife, ukubali matokeo.

Mkuu naona hapa sas ume-tilt angle...

Mbona unataka kumtisha cacico??

Bwana wanaume ambao siyo dhaifu tupo, tena wengi sana (including wewe Poti)....May be ana uhakika kuwa mume wake siyo dhaifu....!!

Ahsante sana Lisa kwa uzoefu wako na weledi wako. Wewe ni mwanamke unayejitambua na kuitambua thamani ya ndoa yako.
 
Last edited by a moderator:
Kwani mkiwa hotelini hizo taulo zenu huwa mnaziweka wapi??

Na huko hotelini huwa hampishi watu wakafanya usafi??

Naomba elimu yako Nyamayao..., hata ukitaka nilipe bill nitalipa!!

Babu DC!!

Babu Hotel ni hotel,kwan hotelini kuna documents zako?zikiwepo si kwenye bag lako na sio makabati?pia hotel kuna may b nyaraka zako za siri,pay slip nk?
Nyumbani kwako,chumbani kwako kunapatikana vyote hivo,including makufuli yenu wote,so babu wewe unaona sawa house girl aje atizame makufuli yako?au tuseme house boy aje atizame chupi za bibi?bedroom kwako ndio the only place pa kujidai,na sio kila mtu kupita kama vile ni uchochoro!strictly my bed room will remain closed to all parties except me n my wife,and our kids bt with controlled movement!
 
Last edited by a moderator:
Emu pitia karatasi yako ya ruksa vizuri....hili kweli halimo?

Huwa mnajificha wapi na pointi nzuri namna hii? Umefafanua vema kbs wajibu wa wenye kitanda. Mwenye masikio na asikie.
huwa sijapata kutoa ruksa beki tatu kugusa chumba changu.
 
Mkuu naona hapa sas ume-tilt angle...

Mbona unataka kumtisha cacico??

Bwana wanaume ambao siyo dhaifu tupo, tena wengi sana (including wewe Poti)....May be ana uhakika kuwa mume wake siyo dhaifu....!!

Babu DC!!

Mkuu wala sijatilt na hata hivyo simtishi cacico, kwanza mtu mwenyewe nasikia hatishiki. lol
Mkuu Darck city huo udhaifu wa wanaume unaweza kukupelekea kumgegeda beki tatu juu ya kitanda unacholala na mkeo, huoni hiyo aibu inavyokuwa? beki tatu anamchukuliaje mama watoto wako kama anaweza kulala pale pale anapolala yeye?
 
Last edited by a moderator:
utasahauje kitambaa?? Moja, mbili kwani zimegeuka sprinkler kwamba hazinyonyeki ndani kunako papale!!! Tatu kwa case yangu, kabla hajaja hiyo jumamosi au jumapili kudeki, kwanini usihakikishe kila kilichopo cha siri kimewekwa sawa???? Tatu kitanda changu hagusi, twatandika wenyewe, ila usafi mwingine, hell no! Nimekataaa!

Yaani wewe cacico ni kichwa...jembe kweli kweli...

Eti mtu anasema kuwa anaweza kusahau taulo za kujifutia?? How and why??

Kama mtu ni msahaulifu kiasi hicho basi huyo aendelee kujifanyia usafi...

Na kama mtu unajua kuwa unafungulia bomba kama wale jamaa zangu wa kanda ya Ziwa, kwa nini asitumie plastic sheets na akimaliza kazi akazitoa...then wasaidizi wanaweza kuendelea na majukumu yao??

Bado ntarudi hapa hapa, mbona hotelini hatufukuzi wafanyakazi wanaokuja kusafisha vyumba kwa sababu kama hizi?

Nasikitika kwamba watu wanaweza kuendekeza kupoteza muda (very precious time) kwa kazi ambazo siyo technical, wakati kuna mambo mengi ya muhimu yanawasubiri....

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Hapa sasa unataka kupotosha mjadala cacico. Kutandika kitanda kunamlazimisha beki tatu aingie chumbani kwenu. Baadhi ya watu nikiwemo mimi tunasema beki tatu haruhusiwi kuingia chumbani kwetu na tunazo sababu zetu za msingi.

La mume kuchukua beki tatu lina mambo mengi ndani yake si kutandika kitanda tu. Kama usipoweka mipaka ya kazi na majukumu kwenye nyumba yako uko katika nafasi nzuri sana ya kuharibikiwa. Sasa kama huamini kwamba wanaume ni dhaifu kwa wanawake basi we endelea tu kumuachia loose mumeo lakini siku yakikukuta usilaumu umodern wife, ukubali matokeo.
I TOUGHT UPO TOFAUTI!! UMENIPA MAWAZO!! WHY SHOULD ANY MARRIED MAN BE WEAK?? KWA HIYO NYINYI KUWA DHAIFU NI SAWA?? ILA KWA MWANAMKE NI CRIME?? HUU UBEPARI KUMBE UPO KWENYE VEINS ZENU! basi sina mengi ya kuongea ngoja nikae kimya! NAJUA WANGU YUPO WEAK, but NOT TO THIS EXTENT!!! MMMMHHHHHH!!
 
Na nikupe siri Bro...sisi wanawake uwa when it comes to marriage huwa tunaoneana wivu kwa kuwa na mume caring na si mume mwenye noti kwani kama ni noti hata wanawake siku hizi wanajua kuzichanga.

Mwanamke akiwa na mume anayefanya vitu ambavyo ni very rare utaona marafiki zake wanavyo comment kihisia wishing they could be on her position.

Nikiwa college mfano kuna prof mmoja alikuwa anabeba wanae kuwapeleka clinic...basi hiyo ilikuwa indentity ya ile familia...kila mtu anasema kuwa mkewe ana bahati.

Hivyo ukitaka kumpumbaza mkeo fanya vitu vidogo vidogo ambavyo wanaume wengi (mabossy) hawafanyi...jua hapo umemroga.

aksante sana dada yangu ,ila kumbuka care is sharing.....na siyo kila ukifanyacho basi na mimi nikulipizie au kila nikifanyacho lazima wewe ulipizie. tatizo la kuingiza mambo ya nipe nikupe ni balaa kabisa.

hela ni muhimu sana na ndiyo maana familia ikiyumba kiuchumi all the blame ni kwa mume na kupewa majina kibao like mwanaume suruali n.k.

kumsindikiza wife clinic au hospitali au hata mahakamani hiyo ni haki yake na mimi napaswa kutimiza wajibu hapo kadri ninavyopata muda.( kuna clinic moja(IPPM) ya specialist mmoja pale muhimbili kinamama wanawahi namba kuanzia saa 11 asubuhi ,halafu dokta anaanza kuwatibu saa tisa mchana ,kwahiyo hapo unashauri vp? huu ni mfano tu)

ninambinu zangu za kumuwin mwanamke lkn zimetofautiana na hizi ,lakini pia kuna vitu wanawake wakifanya ni lazima wataniwin tu......tumetofautiana.
 
Back
Top Bottom