Mzee mzima kweli leo kazi ipo kama na wewe umegeuka kuwa denti.
Chumbani kwangu na mke wangu ni mahali petu pa binafsi/maalum (private) kufanyia mambo yetu, huko tunajiachia. Chochote kinachofanyika huko ni chetu wawili mimi na mama rhobi tu ndo tunajua na tunaopaswa kujua. Mzee mzima chumbani kwako ndio mahali pa kujifunga khanga. Tatizo ninyi waswahili wenzangu mnafunga khanga mnatoka nazo kwenda sokoni hapa mtanishangaa.
Si kila unachokifanya kinakuwa ni kwa ajili ya "public consumption" hapa nakusudia public ya familia yako, lile mnalodhani kwamba linaweza kufikishwa kwa wengine ndo mnalitoa. Kama mna jambo lenu huko ndo mnaweka cabinet na kulidadavua, huko ndiko mnakaliana bila wasiwasi wowote manake mko wenyewe (hapa najua wengine wanajifanya wameendelea wanadandiana hata sebuleni mbele ya ndugu jamaa na marafiki)
Na la mwisho, siri yenu wewe na mkeo inakuwa siri ikiwa ni yenu wawili tu lakini mkishamruhusu mtu mwingine kuingia chumba chenu cha siri basi hakuna tena usalama hapo. Tena hawa mabeki tatu tunaowaokota tu mitaani wameshaleta mabalaa kwenye ndoa/familia za watu. Hapa kuna mambo mchanganyiko kama vile mabeki tatu kuwatia kwenye kumi na nane zao wanaume, kuibiwa, kuvujisha siri za familia na mambo mengine kama hayo. Sasa kwa kulitambua hilo ndipo wahenga wetu wakatufundisha kutoruhusu watu wengine kukizoea chumba changu na mke wangu.