cheupe sr
Senior Member
- Aug 18, 2012
- 102
- 34
Sawa cheupe sr,
Mbona sasa hujatueleza kwa nini hupendi house girl atandike kitanda chako?
Babu DC!!
Mimi kwa mtazamo wangu naona chumbani kwangu na mume wangu ni sehemu nyeti sana , na hasa ukiingaia sasa hivi mambo yameharibika sana ma HG wamekuwa hawaaminiki tena. so sitaki nimpe nafasi ya kunijua zaidi mpk chumbani kwangu. Nop. Na hata mume wangu anajua hilo. Nashukuru Mungu sijawahi pata emergence kali ya kusababisha akaingia otherwise labda kama mama anaumwa yuko ndani kitandani.. na hakuna mtu karibu.. ni lazima itabidi aingie. But that is special case.
Pia nadhani wanawake wengi saivi wamebadilika na ndo maana kama uatakumbuka nilikwambia jirani yangu yeye anatandika wkend kwa wkend ,that means, nao hawanautaratibu wa kumuachia HG..
But still nasisitiza kuwa wanaume muwe pia msaada, sasa kwa mfano mimi nimeamka saa 11 kasoro asbh tunatakiwa tuondoke saa 11 na nusu asubuh, natakiwa niangalie mambo ya mtoto kama yako sawa, nijiandae mwenyew , pia nirudi nikatandike tene mimi ndo nimewahi kuamka. wewe ukiamka ni kukimbilia bafuni tu na kutoka nje kuwahi kunipigia honi, i think that is not fair really..