We mwanamke inakuwaje unatandikiwa kitanda?

Kwann v2 vidogodogo vikusumbue, wat z wrng wit helpng ur blovd wife wit lito hh works! Dnt b self man. If u love ur wife u'l gve ha a helpng hand hasa pale wote mnafanyakazi na kurudi ucku. Dnt b stubborn. Love Love

Kwa mbaaaaaaaali naona kama ulikuwa na mibonge ya points...kwa nini usiandika mwandiko wetu ili sote tukuelewe??

Babu DC!!
 
Mfano mama yako akija na theory walizotumia kulelea watoto wao enzi hizo; za weka chumvi kwenye maji afu mpe mtoto (wa siku kadhaa) itamsaidia tatizo alonalo; utakubali?

Kwa nini mengine mnaona yamepitwa na wakati lakini hili la mwanaume aingii jikoni na bla bla bla mnaona haliwezi kupitwa na wakati?

Hizi dharau zetu kwa "mababu" zetu ndizo zimetufikisha hapa tulipo leo. Watoto wa mitaani wanazidi kuongezeka, talaka zinazidi kuongezeka na mifarakano ya ndoa/familia inazidi kuongezeka kwa sababu ya the so called kuishi kidigitali.

Kwa sake ya familia yangu sioni aibu kufuata misingi muhimu ya ndoa ya kianalogia kadri nilivyorithishwa na kufundishwa na wahenga kuliko kujifanya mdigitali na kuishia kuharibu familia yangu.
 
Sasa hapo Bro unajisifia uchafu...mkeo akisafiri basi wewe unajilaza kwenye shuka chafu...unaona madhara ya kuwa bossy na si husband?...utaja lala njaa kisa mimi MWANAUME. Nampa pole huyo wifi. Kibarua amepata.

Sijisifu wala sijisifii - "the bottom line" ni kuwa siwezi kutandika kitanda na mke wangu anaelewa na anakubali hivyo - BTW tuna miaka zaidi ya 18 ya "ndoa ya furaha"...!

Tatizo letu tunajaribu kuiga mambo ambayo "hayajengi" - Mwanamume anapoanza kutandika kitanda, anajaribu kuingilia "mambo ya ndani" ya wanawake ambayo kimantiki ndiyo "uhimarisha ndoa". Mwanaume inabidi unapoingia chumbani kwako kulala ni lazima hupendezwe na "mandhari" ya chumbani...! Ni wajibu wa mwanamke "pekee" kuandaa "mandhari" hayo...! (Full Stop)
 
yaani hizi ndoa hizi zina mambo, mtu yupo free kabisa kusema hayo maneno,kha, ni aibu kwa kweli, kwani mtu akimfulia mke wake chupi tabu kitu gani? mbona wao wanafuliwa?wanaume wengine mzigo kwa kweli, dizaini Baba E ni yule akiingia room sox kule, boxer chini ya uvungu, suruali kaivua kwa kuikanyagia na kaiacha hapo hapo chini, khaa, wuuuu wanawake tuna kazi kubwa.
 
Baada ya kusoma comments za mabinti na wanawake wengi juu ya hili ndo nimegundua ugumu uliopo juu ya kupata mwanamke mwenye elements nzuri kama walizonazo mama zetu. Si ajabu namba ya wanawake wasiopata waume inaongezeka.

Kweli FELIPE??

Wewe unatafuta mkwe mwenye elements kama za mama zetu??

Unadhani time ni static variable??

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Exactly kaka Mwita Maranya,

Na binti akishaishi chini ya paa langu tayari anakuwa kama mwanangu...that's why siwezi kumtamani...

Sasa inakuwaje house girl aonekane tishio kiasi hicho???

Babu DC!!

babu Dark City umenikuna....sijui uniwowe mke mdogo....(Asprin asione hii tafadhali)

mwanaume mzinzi mzinzi tu haijalishi nani anamfulia, anampikia wala kumtandikia kitanda......

Kiheshima haifai beki tatu atandike kitanda...... ila kati yenu meme na mke yoyote anaweza kutandika kutegemeana na mazingira...... Nimependa utaratibu wa Tuko ......

Last edited by a moderator:
Kwani watu wanaoa ili iweje? Kama ni kusaidia kazi si unaajiri hg tu? Kwa nini uingie kwenye life sentence eti kisa upikiwe na kufuliwa?

Weka hg...endelea kupiga mitaani.

Baada ya kusoma comments za mabinti na wanawake wengi juu ya hili ndo nimegundua ugumu uliopo juu ya kupata mwanamke mwenye elements nzuri kama walizonazo mama zetu. Si ajabu namba ya wanawake wasiopata waume inaongezeka.
 
Sijisifu wala sijisifii - "the bottom line" ni kuwa siwezi kutandika kitanda na mke wangu anaelewa na anakubali hivyo - BTW tuna miaka zaidi ya 18 ya "ndoa ya furaha"...!

Tatizo letu tunajaribu kuiga mambo ambayo "hayajengi" - Mwanamume anapoanza kutandika kitanda, anajaribu kuingilia "mambo ya ndani" ya wanawake ambayo kimantiki ndiyo "uhimarisha ndoa". Mwanaume inabidi unapoingia chumbani kwako kulala ni lazima hupendezwe na "mandhari" ya chumbani...! Ni wajibu wa mwanamke "pekee" kuandaa "mandhari" hayo...! (Full Stop)

sawa hatukatai, but hata akisafiri kwa muda mrefu kidogo maamuzi yako yatabaki hayo hayo?
 
kama kutandika kitanda
kupika chakula cha mume
kumuandalia maji ya kuoga mume(haijalishi kuna bath tubes na madijitali mengne ya bafuni basi japo niandae taulo tu la kujifuta)
kunawisha maji mume kabla ya kula
kuwa na special set up ya chakula ya baba tu hiyo
na kimsingi kufanya yale yote niliona mama yangu akimfanyia baba yangu ni ulocal wacha tu niwe wa kienyeji!
YANGU YANANINYOOKEA!basi! ucooperate ukiiingia mpka kwenye chini ya paa la nyumba yangu daaah!
mimi naamini hivo!

huyo ndiyo mama wa kiafrika aliyelelewa na baba na mama wa kiafrika ,period.

Wewe unaona ubwanyenye kuna wenzako wanafurahia na kama wewe unaona shida potezea kwani wako ambao wako tayari kuzifanya hizo kazi kama expression ya LOVE kwa waume zao na waume wana jinsi ya ku express LOVE kwa wake zao. Kwa sababu MMEKARIRI DEFINITION YA LOVE ndio maana unaona kumtandikia mumewo kitanda ni unyanyasaji.

Ndo maana hamjiulizi kwa nini ndoa nyingi za wanawake waliozaliwa kuanzia 1976 na kuendelea hazidumu. Badala ya couples kujadili jinsi ya kujenga familia na kujiletea maendeleo zinabaki kujadili NANI MWENYE HAKI KULIKO MWINGINE AU NANI AWE SUBMISSIVE NA NANI ASIWE. Why do nt we stick to the fundamental teachings za maneno ya Mungu badala ya kuleta mafundisho yasiyojenga ndoa? .

ushindani na kulipizana kwa kila jambo wanandoa walifanyalo na kelele za usawa zinatumaliza sana.

Nadahani ifike mahali wanawake mjitambue,swala la kulalama mara oooh wanatufanya maroboti,mara ooh kwanini nao wasifanye.........kuwa mjanja,hapa kuna wanawake wanatoa comments za kipuuzi kabisa,kisa kutaka usawa.Kusaidiana kupo ila isiwe ndio mazoea.

ndiyo nashangaa hizo haki bila wajibu mkuu......

Kwani mkiwa hotelini hizo taulo zenu huwa mnaziweka wapi??

Na huko hotelini huwa hampishi watu wakafanya usafi??

Naomba elimu yako Nyamayao..., hata ukitaka nilipe bill nitalipa!!

Babu DC!!

babu DC kulinganisha hotelini na nyumbani kwako siyo sahihi hata kidogo.

Kiukwel, utaratibu wa chumbani kwangu na wife, japo haujaandikwa ni kwamba wa mwisho kuamka kati yetu ndiye anayetandika kitanda.
Alafu tuna utani kuwa kila anayetandika, mwenzake akija anajitahidi kumkosoa kuwa hakutandika vizuri, anajifanya kutoa kasoro (jokes)
I just enjoy that?

good for you mkuu ,na huo ndiyo upendo wenyewe kama its ok with both of you sioni kama ni tatizo....... it need mutual respect and understanding
 
Furaha ni individual...unaweza sema mna furaha kumbe mkeo anakuvumilia na kupretend as if everything is okay kwa kuwa hana jinsi. Lol.

Sijisifu wala sijisifii - "the bottom line" ni kuwa siwezi kutandika kitanda na mke wangu anaelewa na anakubali hivyo - BTW tuna miaka zaidi ya 18 ya "ndoa ya furaha"...!

Tatizo letu tunajaribu kuiga mambo ambayo "hayajengi" - Mwanamume anapoanza kutandika kitanda, anajaribu kuingilia "mambo ya ndani" ya wanawake ambayo kimantiki ndiyo "uhimarisha ndoa". Mwanaume inabidi unapoingia chumbani kwako kulala ni lazima hupendezwe na "mandhari" ya chumbani...! Ni wajibu wa mwanamke "pekee" kuandaa "mandhari" hayo...! (Full Stop)
 
babu Dark City umenikuna....sijui uniwowe mke mdogo....(Asprin asione hii tafadhali)

mwanaume mzinzi mzinzi tu haijalishi nani anamfulia, anampikia wala kumtandikia kitanda......

Kiheshima haifai beki tatu atandike kitanda...... ila kati yenu meme na mke yoyote anaweza kutandika kutegemeana na mazingira...... Nimependa utaratibu wa Tuko ......

Hahahahaha,

Unajua nini BADILI TABIA, 2015 nina mpango wa ku-mutate ....

Utafikiriwa tu kama washindani hawatakuwa wengi...

Hapo red pia ungekamilisha kwa kusema kuwa, kiheshima, kama wakubwa hawapo, mtoto au msaidizi wa kazi anaweza kufanya usafi wa chumba ikiwemo kubadilisha mashuka.....hili lina ugumu gani??

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
huyo ndiyo mama wa kiafrika aliyelelewa na baba na mama wa kiafrika ,period.

ushindani na kulipizana kwa kila jambo wanandoa walifanyalo na kelele za usawa zinatumaliza sana.

ndiyo nashangaa hizo haki bila wajibu mkuu......

babu DC kulinganisha hotelini na nyumbani kwako siyo sahihi hata kidogo.

good for you mkuu ,na huo ndiyo upendo wenyewe kama its ok with both of you sioni kama ni tatizo....... it need mutual respect and understanding

Tofauti ya hotelini na nyumbani kwa muktadha wa mtu aliyeajiriwa ni ipi?

Kwani hotelini wanalipwa Diamond na nyumbani tunalipa copper??

Babu DC!!
 
Afu utakuta hawa wanaojua ku deligate kazi wanakuwaga wasafi....

Mtu atajidai nafanya kila kitu mwenyewe ukute chumba kinadekiwa once a week....tatizo nini hasa kulala chumba kisafi au nani kasafisha?

Hahahahaha,

Unajua nini BADILI TABIA, 2015 nina mpango wa ku-mutate ....

Utafikiriwa tu kama washindani hawatakuwa wengi...

Hapo red pia ungekamilisha kwa kusema kuwa, kiheshima, kama wakubwa hawapo, mtoto au msaidizi wa kazi anaweza kufanya usafi wa chumba ikiwemo kubadilisha mashuka.....hili lina ugumu gani??

Babu DC!!
 
Umeona eeh...utasikia mi siri chakula alichopika hg wakati kazini anakula chakula cha mama ntilie hakina hata TBS.
Raha ya watu kama hao ni kuona mke anatoka jasho...

Tofauti ya hotelini na nyumbani kwa muktadha wa mtu aliyeajiriwa ni ipi?

Kwani hotelini wanalipwa Diamond na nyumbani tunalipa copper??

Babu DC!!
 
Furaha ni individual...unaweza sema mna furaha kumbe mkeo anakuvumilia na kupretend as if everything is okay kwa kuwa hana jinsi. Lol.

Ku-pretend miaka 19? Nadhani unamkosea heshima mke wangu?

Hii "notion" ya "kusaidiana" sijui imetoka wapi? Au ni matokeo ya "uvivu" wa kizazi hiki? Kutandika kitandaa na mambo mengine yanayofanana na hilo yanachukua muda wako kiasi gani kwa siku? Mmeo anapokuwa anatandika kitanda wewe unakuwa unafanya nini - if I may ask?

Kwa mfano, saa 11 ya alfajiri wote mmeondoka nyumbani kuelekea kwenye kusaka pesa, saa mbili au tatu ya usiku wote mmerudi nyumbani... na bahati nzuri house-girl anakuwa ameshafanya kazi zoooote (except "kutandika" - haruhusiwi kuingia chumbani): kuanzia kupika, kuwaogesha watoto, kupiga pasi e.t.c... Sasa hata "kuandaa" chumba mnataka "kusaidiwa"? - SHAME...!
 
Hahahahaha,

Unajua nini BADILI TABIA, 2015 nina mpango wa ku-mutate ....

Utafikiriwa tu kama washindani hawatakuwa wengi...

Hapo red pia ungekamilisha kwa kusema kuwa, kiheshima, kama wakubwa hawapo, mtoto au msaidizi wa kazi anaweza kufanya usafi wa chumba ikiwemo kubadilisha mashuka.....hili lina ugumu gani??

Babu DC!!

DC, hicho unachotaka ujibiwe uridhike hutakipata, hili jambo lina ishu/maono tofauti kutokana na mtu na mtu, kama mie hiyo ya "heshima" imeniacha solemba, "heshima" ipi hapo? hiyo ni kwa mujibu wa BADILI TABIA, kwangu mie huo ni "WAJIBU" wangu, umeona? bado atakuja mwingine na maono tofauti, sasa kama wewe h'gal kufanya unaona poa, na pia kwetu ona poa basi.:confused2:
 
Hahahahaha,

Unajua nini BADILI TABIA, 2015 nina mpango wa ku-mutate ....

Utafikiriwa tu kama washindani hawatakuwa wengi...

Hapo red pia ungekamilisha kwa kusema kuwa, kiheshima, kama wakubwa hawapo, mtoto au msaidizi wa kazi anaweza kufanya usafi wa chumba ikiwemo kubadilisha mashuka.....hili lina ugumu gani??

Babu DC!!

heshima ya ndoa kama mke na mume......

Heshima binafsi ya mke, na ya mume..........

Heshima kwa hg wenu......

Ulinzi na usalama wa chumba chenu, beki tatu wa siku hizi utashtukia kakomba vijiakiba mpaka hati ya nyumba....
 
Last edited by a moderator:
Ku-pretend miaka 19? Nadhani unamkosea heshima mke wangu?

Hii "notion" ya "kusaidiana" sijui imetoka wapi? Au ni matokeo ya "uvivu" wa kizazi hiki? Kutandika kitandaa na mambo mengine yanayofanana na hilo yanachukua muda wako kiasi gani kwa siku? Mmeo anapokuwa anatandika kitanda wewe unakuwa unafanya nini - if I may ask?

Kwa mfano, saa 11 ya alfajiri wote mmeondoka nyumbani kuelekea kwenye kusaka pesa, saa mbili au tatu ya usiku wote mmerudi nyumbani... na bahati nzuri house-girl anakuwa ameshafanya kazi zoooote (except "kutandika" - haruhusiwi kuingia chumbani): kuanzia kupika, kuwaogesha watoto, kupiga pasi e.t.c... Sasa hata "kuandaa" chumba mnataka "kusaidiwa"? - SHAME...!

huyu baba nae anazeeka vibaya, sawa umeeleweka but swali lingine ni kwamba je akiwa mabli kwa muda mrefu kidogo bado msimamo wako utakuwa huo huo?
 
Kwann v2 vidogodogo vikusumbue, wat z wrng wit helpng ur blovd wife wit lito hh works! Dnt b self man. If u love ur wife u'l gve ha a helpng hand hasa pale wote mnafanyakazi na kurudi ucku. Dnt b stubborn. Love Love

i will do because i like and i am into IT,and not because my wife cant do or i am not satsfied with her doings.....na ili vitu vidogo vidogo visinisumbue i wont even bother asking about it......hutanisikia kamwe nikicomplain mbona chakula kibichi au nyumba ni chafu.

kama wote tunafanya kazi ni jukumu lake kuset standards za domestic issues na kuzisimamia kuhakikisha zinafikia matarajio yake na kwa kuishi naye natumaini atakuwa ameshanisoma mumewe matarajio yangu ,kwahiyo atakuwa hapo nyumbani kulinda interest zangu kama my wife kwenye domestic issues......( to me hapo nitajifeel nina mtetea ndani na jogoo lazima nilete kwere mtetea wangu akiguswa tu au kuudhiwa/kerwa)....HAKUNA KITU KITAMU SANA NA HULETA HISIA ZA UPENDO SANA KAMA MWANAMKE WAKO MPENDWA/WIFE TO HAVE YOUR BACK.IT FEELS VERY GREAT.
 
Sawa mwanaume ni mvivu, lakini haitajustfy kumuingiza hausigelo chumbani kwangu aisee. Ever since naanza kujitegemea, sijawahi tandikiwa kitanda na hgelo wala kufanyiwa usafi naye.
Hongera, kama kwenu kuna mabinti/wadada itabidi tujitambulishe(I hope wana tabia kama zako)
 
Back
Top Bottom