We Condemn: Calling for A National Day of Mourning

We Condemn: Calling for A National Day of Mourning

Hakuna mtu asiyeliona tatizo la polisi lililotokana na mfumo mbaya wa sheria kandamizi, hili ni tatizo la upande mmoja LAKINI naona pia lazima tuliangalie pia tatizo la busara ya Chadema kung'ang'ania kufanya maandamano bila ya kujali athari zake ukizingatiwa kuwa kulikuwa bado na nafasi ya kufanya mkutano na kuyawasilisha yote yaliyotakiwa kuwasilishwa kwa umma mkutanoni bila tatizo lolote, kama wanatambua dhamana waliyonayo kwa wanachama wao iliwapasa kufanya uchambuzi wa faida na hasara ya kufanyika kwa maandamano hayo kabla ya kufikiwa kwa uamuzi huo.

Na kwa upande mwingine yatupasa pia tulione na kulikemea kosa la kauli ya Dr. Slaa kuwaagiza vijana kwenda katika kituo cha polisi baada ya mkutano kuwatoa kwa nguvu viongozi waliokamatwa na hivyo kupelekea vijana kupambana na polisi na kupelekea wengine kuuawa. Dr. Slaa anapaswa kujua kuwa kauli moja mbovu ya kiongozi wa kisiasa inaweza ikaleta madhara makubwa kwa nchi yake na kwa watu wanaomuamini na kumpenda sana, nategemea Dr. Slaa atajifunza katika hili.

Mwaihojo, japo nakubaliana wa wewe, lakini wanasiasa mahiri ulimwenguni kote, walipambana. Haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, inapiganiwa. Mandela aliandamana, Martin Luther King pia aliandamana, kina Kenyetta waliandamana, na wote hao walipigwa mabomu ya machozi na kuishia jela, ikiwepo loss of life, lakini mwisho wa siku, ukombozi utapatikana.

Hata Mungu alikuwa na uwezo wa kumkingia mwanaye Yesu Kristu na mateso yale, aliweza kuleta ukombozi bila kupitia mateso, lakini alimuacha ili kutoa somo kwa ulimwengu kuwa ukombozi, unakuja kwa njia ya mateso wakati wingine hadi kifo ili waliobaki waponywe.
Kwa kupigwa kwake, sisi tuluiponywa, ndivyo hivyo kwa kupigwa wana Chadema, Tanzania itaponywa!.

Aluta Continua!.
 
Mawazo yako ni duni, hawa raia wameuliwa (Mungu awalaze apendapo), kwa kusikiliza maneno ya viongozi wao, hususan maneno ya Silaa.

Kumbuka hawajapatwa maafa wakigombania matakwa ya wengi (majority).

Chadema (viongozi) wamekiuka amri ya polisi iliyowata wasifanye maandamano, wao waka kaidi na kuanzisha maandamano. Halfu leo unalete utumbo wa kusema iwe mourning day ya Taifa? Taifa lipi hilo? wewe ungekuwa na uchungu sana na taifa hili usingekimbia shida na dhiki za hapa nyumbani kwenda Merekani halafu unatuma viujumbe vyako vya uchokozi kila siku. Nini kinachokufanya usikae hapa na kuingia kwenye maandamano kama hao mnaowarubuni?

Kama ni rahisi ungeishi hapa na si kutokomea huko merekani na kutuletea fitna zako kila kukicha.

Naona Halmashauri yako ya ubongo haina ushirikiano.Unatumia sana personal attack kuliko hoja.
 
Jamani hapa tunapiga makelele tu, lakini ndo hivyo mafisadi wanalinda masilahi yao. kwa hiyo mtu yoyote anayedai haki nilazima atakiona. sababu nyingi zitatungwa ilmradi watu wapate kipigo waogope, hapo ni mwanzo tu, tutashuhudia mengi. hayo si matakwa ya said mwema, bali ni amri za mafisadi. mtasahau ajenda zingine kama dowans na richimond na katiba. hivi unadhani mkwele alifurahi kwa wabunge wachadema ku-walkout alimaindi sana na sasa ndo kisasi kwanza kimeanza.
 
What i have come to realize is that people have little knowledge about development studies, conlict is inherent in the nature of politics, na hakuna haki inayokuja kama lulu kwenye sahani, haki hupiganiwa, ingawa kupigana haimaanishi magonvi, kinachofanywa leo matunda yake yataonekana damu haikumwagika bure, Kwa hiyo watu kama selemani uelewa wao ni mdogo lakini bado wana nafasi ya kwenda shule waweze kuinterprete kinachofanyika leo.

Mataifa yaliyoendelea nayo yalipitia ujinga kama huu, lakini leo hii raia wake wanaheshimiana si kwa kuwa tu mungu alipenda hivyo,lakini pia damu ya mababu zao ilimwagika kwa manufaa ya vizazi vya wajukuu zao.
 
Mheshimiwa KNKU,
Nimekusoma nikaona labda ukisoma hapa unaweza pata picha...
Maswali ambayo yaliwashinda Mwema na Nahodha

Nahodha na Mwema walijibu baadhi ya maswali juu juu na kupuuza au kushindwa kujibu mengine, hasa yaliyohitaji majibu makini na ya kina.

Kwa mfano, Nahodha alipoulizwa kwanini serikali inataka mazungumzo baada ya watu kufa wakati ilipuuza ushauri huo huko nyuma, alisema: ”muda wa kufanya mazungumzo ya kina usingeweza kutosha.”
IGP Mwema alipoulizwa kwa nini polisi wanapeleka wananchi na viongozi wa CHADEMA mahakamani, huku wakikataa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani polisi walioua raia jijini Arusha, hakuweza kutoa jibu lolote. Badala yake, alirukia maswali mengine. Hata alipoulizwa swali hilo mara kadhaa, aliipuuza.

Alipoulizwa kwanini wafuasi wa CHADEMA na viongozi wao walipoandamana kwa takribani kilomita mbili hakuna fujo zilizotokea hadi polisi walipoanza kuwapiga, IGP Mwema alikwepa kabisa kujibu swali hilo. Badala yake aliendelea kusisitiza kwamba taarifa za kiitelijensia walizokuwa nazo zilionyesha kwamba kungekuwa na tishio la amani.

Mwema alidai kuwa matokeo ya kuchomwa moto kwa baadhi ya vibanda na nyumba mjini Arusha, ni ushahidi kuwa taarifa za kiitelijensi walizokuwa nazo zilikuwa sahihi. Lakini alipobanwa kwa maswali kwamba kwa nini uchomaji huo haukujitokeza mchana kabla ya polisi kukamata, kupiga na kuua watu, hakuweza kutoa majibu.
 
Kwanini viongozi wa Chadema walishinikiza wananchi waandamane wakati dola ya nchi ilipiga marufuku? Hebu jiulize hilo kwanza. Chadema leadership is responsible kwa kushinikiza wananchi to be involved in an illegal act. Tukubaliane hilo kwanza.

Kubaliana hilo na wajinga wenzio kina Makamba.
 
Mwaihojo, japo nakubaliana wa wewe, lakini wanasiasa mahiri ulimwenguni kote, walipambana. Haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, inapiganiwa. Mandela aliandamana, Martin Luther King pia aliandamana, kina Kenyetta waliandamana, na wote hao walipigwa mabomu ya machozi na kuishia jela, ikiwepo loss of life, lakini mwisho wa siku, ukombozi utapatikana.

Hata Mungu alikuwa na uwezo wa kumkingia mwanaye Yesu Kristu na mateso yale, aliweza kuleta ukombozi bila kupitia mateso, lakini alimuacha ili kutoa somo kwa ulimwengu kuwa ukombozi, unakuja kwa njia ya mateso wakati wingine hadi kifo ili waliobaki waponywe.
Kwa kupigwa kwake, sisi tuluiponywa, ndivyo hivyo kwa kupigwa wana Chadema, Tanzania itaponywa!.

Aluta Continua!.

I salute you
 
zomba acha umamuma na ukilaza...mungu akurehemu before u die..
 
Zomba nakushangaa kumshambulia Mwanakijiji wewe na Selemani. Wewe umetumwa tu na kama kuna mtu ambaye hana akili basi ni wewe na siyo mwanakijiji. Sisi tunaomboleza vifo vya wenzetu 3 waliopigwa risasi na Polisi. kati ya waliojeruhiwa haswa raia hakuna aliyepigwa na CHADEMA. Waliotaka kuandamana hawakuwa na shida na mtu ila ku communicate ajenda zao kwa amani. Ni kuulize swali : NI KWA NINI POLISI WAZUIE MAANDAMANO YA AMANI. Hivi kwa sababu polisi wamesema hata kitu chenyewe kikiwa hakina maana basi watu wafuate tu. Era ya kukubaliana na kila utumbo wa watawala imwpita cha kuangalia ni kuepuka kuvunja sheria tu ila upuuzi wa kuambiwa acha hiki fanya hiki bila sababu hakuna mtanzania atakayeendekeza tena. Hivi leo huyo polisi akikujia akasema si ruksa kulala na wife kwa mwezi mzima kwa sababu za KIINTELIJENSIA basi na chumba utahama kwa sababu polisi wamesema? Lazima utakataa na kufanya unachoona ni sahihi . Na hiki ndicho CHADEMA walichofanya. Polisi hapa hawakupambana na CHADEMA kwa sababu wanavunja sheria bali kwa sababu eti wamekataa kusitisha maandamano kutokana amri isiyo na kichwa wala masikio. Hakuna atakayekubaliana na huo upuuzi, wewe endelea nao lakini sisi watanzania tunataka mabadiliko kama umezoea kudanganywa na pipi na alua za wakubwa endelea mwenyewe. Tunataka nchi inayojali watu wake na siyo viongozi wa kujilimbikizia huku wanyonge wakizidi kukosa huduma muhimu. Ni AIBU KUONGEA UNAYOSEMA WEWE NA SELEMANI KWANI MAWAZO YENU NI MGANDO
 
Mawazo yako ni duni, hawa raia wameuliwa (Mungu awalaze apendapo), kwa kusikiliza maneno ya viongozi wao, hususan maneno ya Silaa.

Kumbuka hawajapatwa maafa wakigombania matakwa ya wengi (majority).

Chadema (viongozi) wamekiuka amri ya polisi iliyowata wasifanye maandamano, wao waka kaidi na kuanzisha maandamano. Halfu leo unalete utumbo wa kusema iwe mourning day ya Taifa? Taifa lipi hilo? wewe ungekuwa na uchungu sana na taifa hili usingekimbia shida na dhiki za hapa nyumbani kwenda Merekani halafu unatuma viujumbe vyako vya uchokozi kila siku. Nini kinachokufanya usikae hapa na kuingia kwenye maandamano kama hao mnaowarubuni?

Kama ni rahisi ungeishi hapa na si kutokomea huko merekani na kutuletea fitna zako kila kukicha.

zomba
Nasukumwa kukujibu kutokana na ukweli kuwa una akili mgando na unajinufaisha na serikali dhalimu ya CCM. Kama una nia njema na nchi hii na una maanisha uyasemayo, naomba ujibu maswali yafuatayo:

1. Kulikuwa na sababu gani ya msingi ambayo polisi iliwalazimu kuzuia maandamano?

2. Ni kwanini polisi walitumia nguvu kubwa kiasi kile wakati maandamano yalikuwa ya amani?

3. Ni lini polisi wamewahi kuzuia mikutano/maandamano ya CCM na kwanini?
 
... the burden of proof lies with the prosecution kwa Chadema kuithibitishia mahakama 'beyond reasonable doubt' kuwa chanzo cha vurugu ni ile intarvention ya Jeshi la Polisi na sio wana Chadema, kwamba wao walikuwa wakiandamana kwa amani mpaka wapoingiliwa na jeshi la polisi ndipo vurugu zikafuatia.

Ila na viongozi wa Chadema, next time, don't try patience ya serikali vichaa!, wewe umeshaijua serikali yako, inaongozwa na viongozi wenye vichaa, totally insane!, unamuona kichaa mbele yako kashika rungu anatishia kukupiga nalo!, wewe kama una akili timamu, si utamuepuka!.
Wewe ndio kwanza unaendelea kumfuata huku ukimwambia jaribu tuone!...
Kasheshe kubwa halikuwa wakati wa kuzuia maadamano; pamoja na kukamatwa viongozi wa Chadema, bali ni pale watu walipoamua kuandamana kuelekea Central na wahanga wengi wa fujo hizi ndipo walipotokea.

Dr Slaa ameingia kwenye kundi hilo kwani anaposema hataki damu ya watanzania imwagike ni maneno mazuri na yenye busara lkn anapowaongoza watanzania waende kituo cha polisi ili wakawatoe baadhi ya wanachama ambao wametiwa mbaroni na jeshi la polisi.
Kwanini asifuate njia za kisheria kwenda kuwatoa kama kuwachukulia dhamana na baadae waiachie mahakama ifanye kazi ya kuona uhalali wa kukamatwa kwao na kama kisheria wana hatia au laah.

Hii ilikuwa suicide mission!
Pamoja na viongozi wa Chadema kukamatwa, hakuna hata mmoja wao aliyeumia katika vurugu hizo, mie naona wananchi wa kawaida tunatolewa kama kafara kutafutia mtaji wa kisiasa.
Na katika hili Chadema wamefanikiwa kwani serikali wanaelekea kukubali kurejea mezani kuzungumzia uchaguzi wa u-Meya wa Arusha.
 
Mawazo yako ni duni, hawa raia wameuliwa (Mungu awalaze apendapo), kwa kusikiliza maneno ya viongozi wao, hususan maneno ya Silaa.

Kumbuka hawajapatwa maafa wakigombania matakwa ya wengi (majority).

Chadema (viongozi) wamekiuka amri ya polisi iliyowata wasifanye maandamano, wao waka kaidi na kuanzisha maandamano. Halfu leo unalete utumbo wa kusema iwe mourning day ya Taifa? Taifa lipi hilo? wewe ungekuwa na uchungu sana na taifa hili usingekimbia shida na dhiki za hapa nyumbani kwenda Merekani halafu unatuma viujumbe vyako vya uchokozi kila siku. Nini kinachokufanya usikae hapa na kuingia kwenye maandamano kama hao mnaowarubuni?

Kama ni rahisi ungeishi hapa na si kutokomea huko merekani na kutuletea fitna zako kila kukicha.

Zomba (CCM huiiiiiiiiiiiiiiiiiiii)

Umechemsha kaa kimya, nadhani hukua na nafasi kwenye jukwaa, wewe ni dictactor na unanufaika na ufisadi au madalaka. Polisi kazi yao sio kukandamiza upinzani, CHADEMA wanakiliohalali na nihaki yao kukiwasilisha kwa jamii kwa njia waliochagua wao kwamba inafaa, nayo ni maandamano ya amani.

Kumshambulia Mwanakijiji hiyo ni personal sio issue tunayoijadili hapa acha jazba.
 
huyu ***** zomba anaonekana kabisa hajui hata anachoongea maana hata kiswahili chake chenyewe shida. Unafaidika na nini wewe mbwiga?
 
163893_475471016155_687191155_6563333_7552055_n.jpg

There was no justification whatsoever of the brutal use of force against innocent and unarmed demonstrators in Arusha on January 5th, 2011 which lead to the killing reportedly of 2 civilians and injuring a score of other demonstrators. What happened in Arusha is inexcusable and indefensible.

We have to understand that you can not have a political opposition without actual opposition. It is like having a car but denied the right to drive it while others things are all constant. What the Tanzanian government shown through its police force yesterday is an ability and willingness to thwart any strong dissent when that is dissent is paired with other means of civil disobedience such as the demonstrations.

What I still don’t understand is the fact that if there was anytime the government could have used force was the time when people were waiting for results after the much contested elections last year. During that time the political situation in Tanzania was dramatically transformed and there was a credible fear that things could have gone out of hand. But the police and other security organs remained calm, composed and restrained. They did not use force in Arusha, Mwanza, or Mbeya and when they did in fact use force it was restrained and in a relative measure to the political opposition of the time.

That was not so in Arusha yesterday. The demonstrators wanted to demonstrated going to an open space area for a political rally. It was purely a political event charged with political rhetoric. I for one expected that the police force will be there to ensure a peaceful demonstrations and safety of other non-involved people. The demonstrations was well organized and there was nothing whatsoever that signaled trouble before the main event day. None whatsoever.

But abusing their authority the police force decided to cancel the demonstrations and by doing so assaulting the right of individuals to assemble and the right of citizens to air the political grievances. This was indeed an assault on democracy and the principles that govern it.

The deaths of the two individuals can not go unrecognized. Once again our country has seen blood in the hands of the State. We have seen this during the Mwembechai killings, we have seen it in Pemba and it has happened before elsewhere (in other incidents). The police force in Tanzania has this proclivity to use brutal force against citizens not just in such political settings but as we all know during civil issues. It looks like the police force is not well trained in understanding and dealing with the modern world of political plurality and the dynamism of political dissent.

I believe Mr. Said Mwema the current IGP has lost the credibility to lead this force at this juncture of our history. And so has Mr. Andengenye the current Regional Police Commander of Arusha. These two individual bear full responsibility for what happened in Arusha yesterday and they must be sacked immediately. The individual police officers who obeyed an illegal order knowing fully that obeying an illegal order is not a criminal defense they have to be brought to justice and pay the price of the illegal killings of Tanzanians.

As we continue to forge ahead with the cause of democracy and as we continue pushing for the new constitution before 2015 we stand together with all political activists in the country as well as the human rights activists who have come out to condemn the brutal attack on civilians who were protesting their government. I urge Chadema to call for A Day of Mourning to remember our comrades and to show solidarity with each other at this time.

We have to take a stand, for in the presence of evil there is no neutrality.

My friends, if we don’t stand together to oppose the rise of political tyranny in our country then we will surely see our country falling into tyranny. We can choose to stand together or they will find a way to silence us individually. Whatever they (the government, ruling party and their puppets) do we can not retreat or surrender for a brighter future for Tanzania under new people centered Constitution is possible. Yes, a new Tanzania without CCM at the helm of power is coming we just have to hasten it.

By. M. M. Mwanakijiji (BGM).

The future of Tanzania is in the hands of people,,,,not the rulers we have right now,,,,,and the voice of the people is the voice of God!
 
Mawazo yako ni duni, hawa raia wameuliwa (Mungu awalaze apendapo), kwa kusikiliza maneno ya viongozi wao, hususan maneno ya Silaa.

Kumbuka hawajapatwa maafa wakigombania matakwa ya wengi (majority).

Chadema (viongozi) wamekiuka amri ya polisi iliyowata wasifanye maandamano, wao waka kaidi na kuanzisha maandamano. Halfu leo unalete utumbo wa kusema iwe mourning day ya Taifa? Taifa lipi hilo? wewe ungekuwa na uchungu sana na taifa hili usingekimbia shida na dhiki za hapa nyumbani kwenda Merekani halafu unatuma viujumbe vyako vya uchokozi kila siku. Nini kinachokufanya usikae hapa na kuingia kwenye maandamano kama hao mnaowarubuni?

Kama ni rahisi ungeishi hapa na si kutokomea huko merekani na kutuletea fitna zako kila kukicha.
duh kazi ipo kweli ni heri uwe maskini wa fedha kuliko wa fikra.ukila ukashiba ukawa na uwezo wa ku access internetbasi unauwezo wa kutoa pumba tu! duh lakini tutafika changes will change you weather you like or not.weather you use stupidor insult language time will tell
 
Ukweli unabakia jinsi ulivyo; POlisi wanatakiwa kuwajibika moja kwa moja kwa yale yaliyotokea Arusha. Mwema na Andeng'enye ndio wahusika wakubwa. Hawawezi kusimamia mauaji ya wananchi halafu kesho wakabakia kujiita ni viongozi wa "usalama wa raia na mali zao"
 
Tatizo ni kuwa kwako wewe umefumba macho hutaki kuona makosa ya serikali; kwa kufumba kwako macho uko tayari kuacha serikali ifanye lolote kwa mtu yoyote si kwa sababu ni haki au ni sawa bali ni kwa sababu ni serikali. Wakati wa utawala wa ...makaburu kulikuwa na watu waliotaka ANC wasiupinge utawala huo na kuwasihi wakubaliane nao au wauelewe. Ndicho ninachokiona unachokifanya. Kwako wewe, serikali haiwezi kufanya jambo baya. Mawazo yangu yaweza kuwa ni ya unafiki, lakini msimamo wako ni wa hatari kwa taifa letu na ni wajibu wa watu wenye dhamira zao kuwapinga.[/QUOTE
Mzee Mwanakijiji!
Hakuna hata siku moja ambayo sijaona makosa ya serikali au kufumbia macho makosa hayo lkn kukosoa serikali ni kwa njia ya maandamano tu ambayo hatima yake ni kupoteza maisha ya binadamu wenzetu?Hivi unataka kuniambia hakuna njia ambazo zinaweza kutumika zaidi ya maandamano kuishinikiza serikali iliyopo madarakani kutekeleza yale umma wa Tanzania wanayoyataka? tumeona hivi karibuni moto wa kutoka ndani ya bunge kwa amani umeweza kufanikisha mjadala wa katiba kupata muelekeo mpya.Tusilazimishe lile tunalolitaka ndiyo lifanyike hata kama linahatarisha maisha ya binadamu wenzetu,Maisha ya binadamu yanapopotea hamna anayeweza kuyarudisha hivyo pale tunapoweza kuepusha upotevu wa maisha ya binaadamu au kupoteza amani ni bora tukazingatia hilo na kutafuta taratibu mbadala za kutupeleka salama.Mfano wa Afrika ya kusini na hali ya Tanzania tuliyonayo sasa nitofauti kabisa na hali iliyokuwa sauzi haijafikia hata robo ya uhuru wa watanzania walionao ktk nyanja mbali mbali.tusishabikie machafuko ktk nchi tunayoipenda kwa jina la kuleta mabadiliko naamini busara inapotumika mabadiliko tutayapata kwa njia salama na kuyafaidi mabadiliko hayo kwa amani bila ya madhara.
 
Mheshimiwa KNKU,
Nimekusoma nikaona labda ukisoma hapa unaweza pata picha...
Maswali ambayo yaliwashinda Mwema na Nahodha
Shopa!
Mimi siwezi kuwajibia wao kushindwa kujibu maswali kwani mimi ningekuwa ktk nafasi zao au hata nafasi za viongozi wa chadema tusingefika hapo walipotufikisha chadema na jeshi la polisi ktk hili.Waliowahi kupitia jeshi au kufanya kazi ktk majeshi wanaelewa amri za kijeshi zinavyotolewa kuwatupia lawama polisi waliokuwa underground wakati wanasiasa wanaamrisha watu wenye hasira waandamane wakapambane na polisi kwa jina la kuwatoa wenzao sidhani ni sahihi na hapo ndipo Mh. Dr Slaa alipoonyesha udhaifu wa maamuzi juu ya hili.Kwani kwa hao viongozi wa jeshi la polisi si mara ya kwanza kutoa amri za aina hiyo iliyosababisha maafa hivyo kwa upande wao sishangai lkn kwa mwanasiasa ambaye aliahidi kuhakikisha hali kama hii haitokei hilo ndiyo limenishangaza kidogo.
 
Samahani nilimaanisha Shapu na si Shopa!
 
Kwanini polisi wameanza tabia mbaya ya kukataa kila ombi la maandamano? Au mpaka tuandamane kuipongeza serikali kwa kilimo kwanza?
Serikali ili ikae salama lazima ijifunze kusimamia vema sheria. Udikteta hautasaidia sana specially now.

Kwa sababu wanajuwa kuwa hayo maandamano ni ya uvunjaji sheria na hayana cha maana zaidi ya kutafuta fujo.
 
Back
Top Bottom