We Condemn: Calling for A National Day of Mourning

We Condemn: Calling for A National Day of Mourning

Tatizo ni kuwa kwako wewe umefumba macho hutaki kuona makosa ya serikali; kwa kufumba kwako macho uko tayari kuacha serikali ifanye lolote kwa mtu yoyote si kwa sababu ni haki au ni sawa bali ni kwa sababu ni serikali. Wakati wa utawala wa ...makaburu kulikuwa na watu waliotaka ANC wasiupinge utawala huo na kuwasihi wakubaliane nao au wauelewe. Ndicho ninachokiona unachokifanya. Kwako wewe, serikali haiwezi kufanya jambo baya. Mawazo yangu yaweza kuwa ni ya unafiki, lakini msimamo wako ni wa hatari kwa taifa letu na ni wajibu wa watu wenye dhamira zao kuwapinga.[/QUOTE
Mzee Mwanakijiji!
Hakuna hata siku moja ambayo sijaona makosa ya serikali au kufumbia macho makosa hayo lkn kukosoa serikali ni kwa njia ya maandamano tu ambayo hatima yake ni kupoteza maisha ya binadamu wenzetu?Hivi unataka kuniambia hakuna njia ambazo zinaweza kutumika zaidi ya maandamano kuishinikiza serikali iliyopo madarakani kutekeleza yale umma wa Tanzania wanayoyataka? tumeona hivi karibuni moto wa kutoka ndani ya bunge kwa amani umeweza kufanikisha mjadala wa katiba kupata muelekeo mpya.Tusilazimishe lile tunalolitaka ndiyo lifanyike hata kama linahatarisha maisha ya binadamu wenzetu,Maisha ya binadamu yanapopotea hamna anayeweza kuyarudisha hivyo pale tunapoweza kuepusha upotevu wa maisha ya binaadamu au kupoteza amani ni bora tukazingatia hilo na kutafuta taratibu mbadala za kutupeleka salama.Mfano wa Afrika ya kusini na hali ya Tanzania tuliyonayo sasa nitofauti kabisa na hali iliyokuwa sauzi haijafikia hata robo ya uhuru wa watanzania walionao ktk nyanja mbali mbali.tusishabikie machafuko ktk nchi tunayoipenda kwa jina la kuleta mabadiliko naamini busara inapotumika mabadiliko tutayapata kwa njia salama na kuyafaidi mabadiliko hayo kwa amani bila ya madhara.

You fool n coward. Can u give as an example of a country that got change without risking the life of patriot? Who gona give it to you peacefully? That is just a token there is a lot more to come if you realy want change. Is either you risk your life to be free or stay silent to become slave in your own mother land.
 
Mliambiwa msiandamane mkajifanya pasua kichwa! Na mtakufa wengi msipo angalia!

Halloo wewe? Unahatari kweli. Kweli jina lako linashabihana nawe! Yata kukuta sikumooja na utatamani kumeza hilo gundu lako ulilo kunya hapa.
Shame on u.
 
Kwanini viongozi wa Chadema walishinikiza wananchi waandamane wakati dola ya nchi ilipiga marufuku? Hebu jiulize hilo kwanza. Chadema leadership is responsible kwa kushinikiza wananchi to be involved in an illegal act. Tukubaliane hilo kwanza.
Hiyo dola ikikuamuru wewe leo hii umlawiti mama yako mzazi utatii kwa sababu ni dola imekuamuru?
 
Mzee Mwanakijiji!
Muda kwangu ni mchache na unanikwaza kujibu kila hoja lkn ninasema endeleni kuwahamasisha viongozi wa chadema watie watu mitaani kwa kila wasilokubaliana na serikali na waendelee kuwahamasisha watanzania kuandamana maana maandamano ndiyo mkakati mzuri wa kuleta mabadiliko.Mimi nalani kilichotokea Arusha na ninakubali kutokubaliana nawe kwenye hili kwani msimamo wangu pande zote mbili zina hisa juu ya kilichotokea Arusha.Mnaweza mkaspini mnavyoweza kwa kufikiri hatuelewi ni kwanini mlichagua maandamano badala ya mkutano na kwanini mlikubali hata watu watolewe kafara, Its all about media camera and attention deficit Disorder!

Hadi hivi sasa rekodi hapa inaonesha kuwa unatatizwa na wananchi kutumia haki yao ya kuipinga na kuandamana dhidi ya serikali kuliko vitendo vya kimabavu vya serikali dhidi ya wananchi wasio na silaha ambavyo vimesababisha mauaji ya watu wa tatu mikononi mwa polisi. Unajaribu kuhalalisha vitendo hivi vya kinyama kwa kusingizia "kwanini waliandamana". Hili ni wazo la kusikitisha.
 
Pasco!
Tatizo limesababishwa na pande zote mbili na hili sijalifumbia macho lkn kuwapa polisi walioko underground lawama wakiwa na wao walikuwa wanajihami kupoteza maisha yao vile vile si busara.Kwanini Mh. Dr Slaa ktk hali tata kama hiyo aliamua kuingiza watu wenye hasira mtaani na kibaya zaidi kwenda kituo cha polisi kutaka kutumia nguvu kuwatoa wenzao hivi kama wangefanya mkutano baadae wakaenda kuwatoa kwa njia zinazokubalika kiutaratibu kusingeepusha haya yaliyotokea.Mara nyingine matakwa na matamanio ya kutimiza malengo yao wanasiasa yanakwanza utumikaji wa busara ktk kufanikisha hio na yanatoa mwanya kwa udhaifu wa maamuzi kuchukua mkondo na kilichotokea Arusha kimesababishwa na hili.

Kwa hiyo wataka kuniambia kujihami kwao ilikuwa ni kuua raia wasiokuwa na hatia! Kujihami ilikuwa ni kuwaachia viongozi wa CHADEMA. Ni wapi uliona haki inaletwa kwenye sahani? Ukipigania haki hakuna kurudi nyuma hata kumwaga damu ikiwa huamini hivo jiandae kuwa mtumwa. What do you expect if people are pushed to their limit?
Raila wakati wameanza serikali ya Muungano alimwambia Kibaki hapa nilipofika siwezi kurudi nyuma umenisukuma mpaka utani sasa jiandae manake nitarudi katikati kwa nguvu ya ukuta. Inafika mahali hakuna kurudi nyuma. Wamechakachua kura ya urais, wamechakachua kura ya umeya, wamewapiga watu na kukamata viongozi. Hapo bado unataka tuwachekee kwa njia nyingine zaidi ya kuwaonyesha kuwa tumechoka kama mapambano tuanze? Tatizo la Tanzania ndio hili na ndio maana polisi na viongozi wa chama dhalimu CCM wanatuonea. Inafika mahala sasa tuseme basi. Kama mapambano wajiandae make hawawezi kutoa haki kwa amani.
Dr. Slaa kaibiwa kura na ushindi kugeuzwa amekuwa mstaarabu nchi iwe na amani nado wanaendelea na udhalimu wao. Unategemea wataacha lini bila kupinga ukandamizi huo kwa kupambana nao iwe kwa maandamano au kupambana nao? Think critically u coward.
 
Mzee Mwanakijiji Umeongea Hongera! IGP na RPC Arusha na wapambe wao ni lazima wasimame mahakamani. SAA YA UKOMBOZI NI SASA!
 
Mawazo yako ni duni, hawa raia wameuliwa (Mungu awalaze apendapo), kwa kusikiliza maneno ya viongozi wao, hususan maneno ya Silaa.

Kumbuka hawajapatwa maafa wakigombania matakwa ya wengi (majority).

Chadema (viongozi) wamekiuka amri ya polisi iliyowata wasifanye maandamano, wao waka kaidi na kuanzisha maandamano. Halfu leo unalete utumbo wa kusema iwe mourning day ya Taifa? Taifa lipi hilo? wewe ungekuwa na uchungu sana na taifa hili usingekimbia shida na dhiki za hapa nyumbani kwenda Merekani halafu unatuma viujumbe vyako vya uchokozi kila siku. Nini kinachokufanya usikae hapa na kuingia kwenye maandamano kama hao mnaowarubuni?

Kama ni rahisi ungeishi hapa na si kutokomea huko merekani na kutuletea fitna zako kila kukicha.






Not all dogs will wake up when thieves are around the streets, some of your types will excute non-humanity nature!!!!!!!!!!
 
tufikiri kwa makini katika kila jambo, somalia na kwingineko iliaanza hivi hivi.
jk kumbuka kila siku unawapeleka askari ndugu zetu kulinda amani sehemu mbalimbali, je wataka siku moja waje walinde amani tanzania.

kila binadamu ana kiwango chake cha kuvumilia, itakuja siku watanzania hawa watapata support toka mataifa katili. Watalishwa sumu, hatutakaa hapa.

ninaumia sana kuona watu wanaongea kwenye vyombo vya habari kana kwamba hawajakua kifikra. Hawa waliofiwa wanafidiwa kitu gani na serikali?


tukumbuke september 11, mamia ya watu walipoteza maisha, lakini tumesahau kwamba lazime umnyanyase sana raia ndipo anapowaza kutenda unyama ambao hautasahaulika.

siasa chafu ndizo chanzo cha maafa na vifo.

sasa tunapotembea barabarani tukisikia king'ora cha polisi watu twa kaa pembeni kupisha wakubwa wapite je, hiyo ndio inawasahaulisha na kutuona hatuna haki? Mwataka ifike siku tuache kuwapisha?







najitolea kulia mwezi mzima nikiomboleza msiba huu, inauma sana
 
Hadi hivi sasa rekodi hapa inaonesha kuwa unatatizwa na wananchi kutumia haki yao ya kuipinga na kuandamana dhidi ya serikali kuliko vitendo vya kimabavu vya serikali dhidi ya wananchi wasio na silaha ambavyo vimesababisha mauaji ya watu wa tatu mikononi mwa polisi. Unajaribu kuhalalisha vitendo hivi vya kinyama kwa kusingizia "kwanini waliandamana". Hili ni wazo la kusikitisha.
Mwanakijiji hawa hawakosi katika jumuiya. Hata nyakati za wakina Mandela watu wa aina hii walikuwepo. Weusi tii waliokuwa wako tayari kuendelea kula makombo ya weupe.
Leo katika vinchi vyetu ambavyo sasa tuna wakoloni weusi badala ya weupe usione ajabu watu wa jinsi hiyo hiyo wapo. Waoga maana hawawatendei watanzania haki na wanaogopa utawala mwingine ukija, wamekwisha. Hawa tunao hata huku mitaani kwetu.
 
Siku ya Jumatano ndiyo siku ya maombolezo, lakini hawajatupa muda kukaa kimya kuwakumbua Marehemu.
 
Back
Top Bottom