Naomba utoe mfano wa chanzo kimoja huru cha habari kilichoanisha kuwa Polisi walizidiwa "nguvu na raia". Naomba uweke kimoja tu na walizidiwa nguvu kabla ya kujaribu kuvunja maandamano au baada ya jaribio la kijinga la kuvunja maandamano halali?
Swali hili linaweza kuwa na hekima kidogo lakini ukiliangalia halizingatii ukweli. Watu 100 wenye manati wanalinganishwa vipi na mtu mmoja mwenye SMG? Je askari mia moja wenye SMG unaweza kulinganisha na wananchi 100 ambao hawana silaha?
Tatizo ni kuwa hawa wananchi hawakuwa hata na manati! Hakuna aliyekamatwa na kisu wala fimbo. Walikuwa mikono mitupu. Now u tell me kuna ulinganifu gani kati ya mikono mitupu na SMG, magari ya maji ya upupu, bastola, mabuti, virungu n.k? Really? Yaani unalinganisha wananchi wasio na silaha ya yote na jeshi la Polisi lenye udhaifu wa muda mrefu na silaha bwelele?
hapana hii si hoja ya msingi; kwani hakukuwepo na wenye manati! walikuwwepo watu wenye mikono mitupu. Sasa hiyo ni hoja ya msingi..
,
Yaani silaha zote hizo na unaniambia walizidiwa nguvu? Really, wangezidiwa nguvu maandamano yangefika mwisho. Polisi hawakuzidiwa nguvu bali waliwazidi nguvu wananchi wasio na silaha na kusababisha mauaji. Thats is a fact.
Nice try. Hakukuwa na fujo yoyote kabla ya jeshi la polisi lenye mwelekeo wa udhalimu lilipoamua kuingilia maandamano yaliyokuwa yanasonga mbele. Haki ya kulinda uhai unaita mtu yeyote anayeshambuliwa kujitetea hata ukishambuliwa na Polisi. Wananchi walikuwa wanaandamana vizuri tu hadi pale POlisi walipoona maandamano kweli yanafanikiwa wakaamua kuingilia kati. Hakuna vurugu yoyote kabla ya polisi kuingilia kati.
msisitizo wa neno lako ni "kama".
Nadhani ungetazama kinyume chake. Tusiruhusu watawala kutumia nguvu dhidi ya raia pale ambapo njia nyingine zingeweza kutumika. Tusiruhusu kwa kisingizio cha kuwaridhisha wanasiasa wa chama tawala Jeshi la POlisi linavunja haki za msingi za kiraia. Hiili tusiliruhusu.
Unachosahau ni kuwa huko kote POlisi hawakujipeleka kimbelembele kuzuia wananchi kufanya kazi zao za kisiasa. Huko kote jeshi la POlisi halikusitisha shughuli za Chadema kinyemela kama walivyofanya Arusha.
Hapana, kuna wakati wananchi wanapokosa imani na vyombo vyao vya dola wana haki ya kuwakataa watawala wao kwa njia mbalimbali za kiraia. Haki hii haiwezi kuondolewa kwa vitisho. Nyerere mwenyewe alisema vizuri kabis akuwa wananchii wanapokosa imani na serikali yao na serikali hiyo inapokuwa ya kibabe dhidi yao, basi wananchi wana haki ya kuiondoa serikali hiyo kwa nguvu. Lakini kabla ya kufika huko wananchi wana haki ya kuipinga serikali hiyo na kuikataa pale inapotishia haki zao za msingi. Hii ndiyo falsafa iliyosababisha tuunge mkono ANC, FRELIMO, n.k. Ni muhimu kuelewa dhana hii ya kisiasa.
Serikali haiwezikuwa juu ya wananchi wake na viongozi wake hawawezi kutenda with impunity kwa sababu ni "serikali". Ni lazima kutambua kuwa haki ya kutawala inatoka kwa wananchi sasa serikali can not hold its citizens hostage or in contempt as it seems the Tanzanian government is doing now.
Hapana, tatizo ur trying to create a moral equivalency kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wasio na silaha. You can not find that.
Usianze kunisingizia katika hilo; mimi ni muumini wa demokrasia na njia za kidemokrasia za kuwatumia ujumbe watawala. NInaamini kuwa hoja ndiyo njia ya kwanza kabisa ya kuwashawishi watawala. Lakini watawala wasiosikia la pili ni kuwapinga hadharani kwa njia halali za kiraia na kidemokrasia. Hizi ni njia za kisiasa, siyo makosa kama unavyoashiria. I'm proud to support the cause of democracy.
Lengo la maandamano lilikuwa kuipinga Serikali mkoani Arusha. Hayo mengine naona umekuja nayo tu. Maandamano yalikuwa ni ya kupinga serikali.
ajenda ilikuwa kupinga vitendo vya kuingilia uchaguzi wa meya wa Arusha na kupigwa kwa mbunge wa Arusha mjini. usisahau hilo.[/QUOT
Mzee Mwanakijiji!
Muda kwangu ni mchache na unanikwaza kujibu kila hoja lkn ninasema endeleni kuwahamasisha viongozi wa chadema watie watu mitaani kwa kila wasilokubaliana na serikali na waendelee kuwahamasisha watanzania kuandamana maana maandamano ndiyo mkakati mzuri wa kuleta mabadiliko.Mimi nalani kilichotokea Arusha na ninakubali kutokubaliana nawe kwenye hili kwani msimamo wangu pande zote mbili zina hisa juu ya kilichotokea Arusha.Mnaweza mkaspini mnavyoweza kwa kufikiri hatuelewi ni kwanini mlichagua maandamano badala ya mkutano na kwanini mlikubali hata watu watolewe kafara, Its all about media camera and attention deficit Disorder!