Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,532
Habari za wakati huu wakuu;

Leo nataka niwe BRIEF maana katika maoni ya wadau niliyopata ni kwamba nipunguze urefu wa maandiko yangu kwa sababu baadhi ya watu wana processing power ndogo na wakifika mwisho wa andiko wanakuwa wamesahau ujumbe wa msingi.SO nitakuwa BRIEF

WAZO LINAHUSU NINI?
Wazo linahusu uendeshaji wa FREE LANCE AGENCY lakini kwa mfumo tofauti na unavofanyika Sehemu nyingine

SEHEMU NYINGINE FREE LANCE INAFANYIKAJE?

Sehemu nyingine kuna kuwa na mtu kati(Free lance Agency )ambaye anawakutanisha Freelancers na Clients.Yeye anasajili wote na wakati wa malipo ela inapita kwa agency na agency inamlipa Free lancer

HAPA BONGO INAFANYIKAJE

Hapa bongo Free lance ni kama KIBARUA(Day workers) Ni issue maarufu sana katika makampuni na wanaita OUTSOURCE wakati mwingine.Lakini Pia wapo Vibarua mbao wanafanya kazi kwa pamoja kama vibaru wa ujenzi,udereva,Kilimo,n.k. Lakini Pia wapo wanaofanya kazi usafi majumbani,ulinzi,.Lakini Pia wapo Vibarua ambao wanafanya kazi za kitaalam kabisa kama Law,Accounting,Graphic Design,Software Design.N.K. Katika Mtazamo wa Free Lancing hawa wote ni Vibarua kama hawajawa organized kitaasisi na kibiashara na kama wanayo au hawana ofisi maalum au muda maalum wa kufanya kazi.Tofauti yao tu ni viwango vya utaalam na ubora wa kazi.

FURSA IKO WAPI?

Watu wengi wanaotumia vibarua wanafanya kazi nje ya mfumo Rasmi yaani hawalipi kodi,hawana bima za afya,hawatambuliki na taasisi za kifedha na wala hawako katika mifuko ya hifadhi ya jamii na wala hawapati hadhi na utambulisho katika kufanya kazi zao.Hawapati hata mafunzo ya kitaalamu na uzoefu

Sasa hebu Fikiria iwapo utakuwa na Free lance Agency ambayo inampa mtu hivyo vitu vyote na vingine zaidi.Je itakuwa na impact kiasi gani kwa uchumi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla?Jaribu kufikiria tu kwamba kuna binti wa kazi ambaye ana kitambulisho cha kazi cha kampuni na mkataba wa kazi wenye maslahi mazuri na anapata haki za msingi za mfanya kazi.Na hii yote ikawa inatolewa na Free lance Agency.

Kwa makadirio zaidi 70% ya watanzania hawako katika ajira rasmi hawa wote ukiweza kuwaingiza katika mfumo rasmi na kuwawezesha kufaidi matunda ya kuwa katika mfumo Rasmi unafikiri utakuwa umesaidia watu wangapi?

UNAWEZAJE KUITUMIA FURSA HII?

Kwanza lazima uangalie mfumo wetu wa kisheria Je hilo linawezekana?Pili tuangalie mfumo wetu wa kijamii Je linawezekana?Kisha unagalie Sekta za kuanza nazo,Mifumo ya ICT ambayo inaweza kusimamia hilo na vile vile gharama za uendeshaji na usimamizi na namna ambavyo zitasimamiwa.

HITIMISHO

Hili ni wazo tu ambalo bado ni changa linahitaji kutafitiwa na kuwekwa vizuri.Kama una maeneo ambayo unaweza kufanya maboresho basi huu ndio wakati wa kujadili.Iwapo ungependa kufahamu zaidi kuhusu huduma zetu tafdhali wasiliana nasi kwa Email:masokotz@yahoo.com au 0710323060

Tushirikiane katika kujenga Jamii yenye bidii maarifa na fursa
 
. . .freelancing ni moja ya mkombozi wa changamoto ya ajira kwa vijana, shida ni uelewa bado upo chini juu ya hii kitu, serikali haina sera nzuri ku support hili.
 
Na hapo ndipo ambapo FURSA ilipo.Serikali haina sera.Vijana hawana UELEWA so ukiwekeza katika kujenga uelewa na ukashiriki katika kutengeneza sera sahihi unakuwa umetengeneza fursa kwa ajili yako na kwa ajili ya wengine
 
Great idea, tatizo ni sera kisha utafiti wa kina kwa ajili ya kufanya kitu endelevu na cha kudumu
 
Habari za wakati huu wakuu;

Leo nataka niwe BRIEF maana katika maoni ya wadau niliyopata ni kwamba nipunguze urefu wa maandiko yangu kwa sababu baadhi ya watu wana processing power ndogo na wakifika mwisho wa andiko wanakuwa wamesahau ujumbe wa msingi.SO nitakuwa BRIEF

WAZO LINAHUSU NINI?
Wazo linahusu uendeshaji wa FREE LANCE AGENCY lakini kwa mfumo tofauti na unavofanyika Sehemu nyingine

SEHEMU NYINGINE FREE LANCE INAFANYIKAJE?

Sehemu nyingine kuna kuwa na mtu kati(Free lance Agency )ambaye anawakutanisha Freelancers na Clients.Yeye anasajili wote na wakati wa malipo ela inapita kwa agency na agency inamlipa Free lancer

HAPA BONGO INAFANYIKAJE

Hapa bongo Free lance ni kama KIBARUA(Day workers) Ni issue maarufu sana katika makampuni na wanaita OUTSOURCE wakati mwingine.Lakini Pia wapo Vibarua mbao wanafanya kazi kwa pamoja kama vibaru wa ujenzi,udereva,Kilimo,n.k. Lakini Pia wapo wanaofanya kazi usafi majumbani,ulinzi,.Lakini Pia wapo Vibarua ambao wanafanya kazi za kitaalam kabisa kama Law,Accounting,Graphic Design,Software Design.N.K. Katika Mtazamo wa Free Lancing hawa wote ni Vibarua kama hawajawa organized kitaasisi na kibiashara na kama wanayo au hawana ofisi maalum au muda maalum wa kufanya kazi.Tofauti yao tu ni viwango vya utaalam na ubora wa kazi.

FURSA IKO WAPI?

Watu wengi wanaotumia vibarua wanafanya kazi nje ya mfumo Rasmi yaani hawalipi kodi,hawana bima za afya,hawatambuliki na taasisi za kifedha na wala hawako katika mifuko ya hifadhi ya jamii na wala hawapati hadhi na utambulisho katika kufanya kazi zao.Hawapati hata mafunzo ya kitaalamu na uzoefu

Sasa hebu Fikiria iwapo utakuwa na Free lance Agency ambayo inampa mtu hivyo vitu vyote na vingine zaidi.Je itakuwa na impact kiasi gani kwa uchumi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla?Jaribu kufikiria tu kwamba kuna binti wa kazi ambaye ana kitambulisho cha kazi cha kampuni na mkataba wa kazi wenye maslahi mazuri na anapata haki za msingi za mfanya kazi.Na hii yote ikawa inatolewa na Free lance Agency.

Kwa makadirio zaidi 70% ya watanzania hawako katika ajira rasmi hawa wote ukiweza kuwaingiza katika mfumo rasmi na kuwawezesha kufaidi matunda ya kuwa katika mfumo Rasmi unafikiri utakuwa umesaidia watu wangapi?

UNAWEZAJE KUITUMIA FURSA HII?

Kwanza lazima uangalie mfumo wetu wa kisheria Je hilo linawezekana?Pili tuangalie mfumo wetu wa kijamii Je linawezekana?Kisha unagalie Sekta za kuanza nazo,Mifumo ya ICT ambayo inaweza kusimamia hilo na vile vile gharama za uendeshaji na usimamizi na namna ambavyo zitasimamiwa.

HITIMISHO

Hili ni wazo tu ambalo bado ni changa linahitaji kutafitiwa na kuwekwa vizuri.Kama una maeneo ambayo unaweza kufanya maboresho basi huu ndio wakati wa kujadili.Iwapo ungependa kufahamu zaidi kuhusu huduma zetu tafdhali wasiliana nasi kwa Email:masokotz@yahoo.com au 0710323060

Tushirikiane katika kujenga Jamii yenye bidii maarifa na fursa
Masokotz habari, unatoa nondo zilizoenda deep. Mie nina wazo langu mfano mm ni freelancer tour guide. Naomba unipe ushauri nawezaje kupambania fani yangu ya tour guide, na naweza kuifanya kama sehemu ya opportunities kwa kuwa organizer freelancer na kuwaingiza kwenye kampuni na kufanya nao kazi?
 
Mkuu inawezekana kabisa,Jamo la Muhimu,umeshatambua soko loko,Kama uko serious na una nia ya kuwekeza katika hilo eneo na unayo mawasiliano yangu basi nicheck kwa mesage ili tuangalie needs zako hasa na eneo ambalo upo maana mwisho wa siku biashara lazima ifanyika kibiashara na ninaamini kwamba kuna fursa umeiona.

Hata hivuo kwa kuanzia unahitaji kuwa na contact za wamiliki wa TOUR COMPANIES,Uwasiliane na Wamilii labda wa MAGARI na MAwasiliano ya Makampuni ya TOURS kisha mengine naamini yanawezekana kama unayo NIA ya kuchangamsha hili eneo.

Karibu SANA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom