Jinsi ya Kupata Wazo la Biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,532
Habari za wakti huu;
Ni matumaini yangu kwamba mnaendelea vizuri katika jitihada zenu za kujenga taifa na kuifanya dunia kuwa salama na bora kwa kila mmoja wetu.

Kama ilivyo ada,leo nataka kuleta mjadala chokonozi ambao unalenga zaidi kuchokoza fikra zako na kukusisimua.Mjadala Utahusu "Jinsi ya Kupata wazo la Biashara" Kwa makusudi kabisa nimeacha neno zuri na pia sijataka kutumia neno fursa kwa sababu za msingi kabisa.

Wazo la biashara ni tofauti na fursa.Wazo ni hatua ya chini kabisa ya Biashara ni kama mbegu ambayo hata haijaoteshwa.Wazo linakuwa ndani ya kichwa chako,ndani ya fikra zako.Kila mtu anaweza kuwaza.Kuna ambao wanawaza mambo mazuri ya kujenga na wanaowaza mambo mabaya.Wazo la biashara linakuwa ndani ya kichwa chako.

Kabla sijaendelea niseme wazo kwamba FURSA ni wazo ambalo lipo tayari kufanyiwa kazi na linachohitaji ni rasilimali pesa na watu ili liweze kunyanyuka na kusonga mbele.Kama wazo lako halijafikia hatua ya fursa basi hilo bado ni wazo na sio wazo zuri.

Wazo linapokuwa ndani ya kichwa chako linakuwa kamili kabisa lenye faida na mafanikio kabisa.Kama ni wazo la kutoa huduma basi hiyo huduma itakuwa inapendwa na kila mtu ndani ya kichwa chako.Kama ni wazo la kuzalisha bidhaa basi hiyo bidhaa itakuwa bora kuliko zote na itapendwa na kila mtu ndani ya kichwa chako.Kama ni wazo la biashara basi hiyo biashara itakuwa kubwa kabisa.Na ndio kazi ya mawazo na ndivyo mawazo yanavyotakiwa yawe.Kama wazo lako la Biashara sio kubwa,kamili na la kipekee basi huna wazo.

Wazo la biashara huwa wazo zuri la biashara pale unapoligeuza na kulifanya liwe FURSA.Hivyo basi kichwa cha mada ningeweza kuandika JINSI ya kubadilisha wazo la Biashara liwe FURSA ya BIASHARA ila kwa sababu ya ufinyu nitaacha ibaki hivyo hivyo.

Katika Kujadili Jinsi ya Kupata wazo la biashara nitauweka mjadala katika SEKTA kubwa NNE AMBAZO ni:
  1. Sekta ya Uzalishaji,Mfano,Viwanda,Kilimo ufugaji n.k.
  2. Sekta ya Huduma
  3. Sekta ya Teknolojia
Ili kutengeneza wazo la biashara katika sekta husika lazima uamue na utambue kabisa kile ambacho unataka kufanya katika sekta husika na ni lazima KIWE KIKUBWA.Kama ni kulima Fikiria KULIMA KATIKA ESTATE,ni KUZALISHA FIKIRIA LARGE SCALE COMPLEX FACTORIES na kama ni KUFUGA fikiria KUFUGA LARGE SCALE K.V. RANCH.Unapokuwa na wazo lako kichwani hakikisha linakuwa kubwa kabisa.Hii ni kwa sababu katika ubongo wako hakuna LIMITS za mtaji,location,BEI,FAIDA,Gharama za UEndeshaji?Wateja?n.k.

Katika Ubongo wako Biashara ina faida kubwa sana na unaimudu kabisa so huna sababu ya KUJIBANA.Utajibana wakati wa utekelezaji.Kila changamoto kwenye ubongo inayo suluhisho so Project yako lazima ifanikiwe.

Vile vile usiogope kutafuta taarifa kuhusu sekta husika mfano watu au biashara zinazofanya vizuri,bei,utalamu na upekee,na taarifa nyingine unazohitaji.Ujaze Ubongo wako na taarifa za kina kuhusu sekta husika kiasi kwamba uanze kujihisi kuwa na wewe ni mtaalam wa sekta hiyo hata kama sio mtaalamu.

Zungumza na wasimamzi wa sekta,watoa leseni na vibali,wataalam na watu wengine walioko katika sekta husika.Hakikisha unapata taarif za kutosha kuhusu sekta husika.Unaweza kuona kwamba unapoteza muda ila tambua kwamba kadiri unavokuwa na taarifa nyingi ndivyo wazo lako linavyozidi kuwa bora.

Tembelea taasisi za fedha na uone namna ambavyo unaweza kufanya na kazi ikiwamo taratibu zao za kuendesha akaunti,gharama za mikopo aina za mikopo na huduma nyingine ambazo wanaweza kukupatia.Zingatia kwamba Taarifa hizi zitakupamwanga wa ni benki gani itafaa zaidi kwako.

Baada ya kulitengeneza wazo lako vizuri kichwani hatua inayofuata ni kuliweka ktika maandishi ukiwe taarifa zote za muhimu ila sasa wazo lako liwe na sura ya kuweza kuitwa FURSA.

Karibu tujadili mbinu mbalimbali ambazo unazitumia katika kupata wazo la biashara na namna ambavyo unalijenga na kulifanya liwe wazo BORA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom