KERO Waziri wa UTUMISHI afanye ziara kama Waziri Mkuu, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri nyingi ni 'Miungu Watu'

KERO Waziri wa UTUMISHI afanye ziara kama Waziri Mkuu, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri nyingi ni 'Miungu Watu'

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tumeona ziara ya Waziri Mkuu ikitupa picha halisi juu ya uzembe na kutokuwa na uwajibikaji wa uwazi katika Ofisi za Umma.

Tunaomba pia Waziri wa UTUMISHI (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) angeanza ziara ya kupitia hususani katika Halmashauri zote kusikiliza kero na matatizo ya wafanyakazi, sababu naamini pia uzembe katika kazi huletwa pia na baadhi ya Watumishi kuminywa na kutotimiziwa malipo na madai yao ya msingi kwa wakati pasipo na sababu maalumu.

Inakipendeza pafanyike reforms katika Halmashauri zetu sababu baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wamekuwa Miungu watu wakihitaji kusujudiwa na kunyenyekewa ndio wakupe favor fulani na sio kuzingatia taaluma na experience za Watu husika.

Ujumbe huu umfikie pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe yeye na Wizara yake waangalie namba kuhusu utendaji wa Ofisi za Halmashauri pamoja na muundo wake.
 
Back
Top Bottom