Ziara ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba huko Nsimbo, Katavi

Ziara ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba huko Nsimbo, Katavi

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,714
Reaction score
2,745
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba amefanya ziara mkoani Katavi kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa mkoani humo ikiwemo ujenzi wa shule na hospitali na kuelezea mafanikio yaliyofanyika katika kipindi cha uongozi wa awamu ya sita.

  • Waziri Mkuu ameonya tabia ya vituo vya afya kuwaagiza wanaanchi wakanunue dawa nje ingali nchi una utoshelevu wa dawa katika maeneo ya kutolea huduma za afya. Mwigulu amehoji duka la dawa linaweza kupata wapi dawa ambazo serikali haina?
  • Mwigulu ameonya pia mwenendo wa kulimbikiza migogoro jambo linalopelekea kwa kua migogoro hiyo inatishia undugu wetu kama Watanzania. Ameeleza kuwa wakati mwingine wanaosababisha migogoro hiyo ni watu walioamaniwa.
  • Ameagiza pia wakandarasi wote waliolipwa fedha zao zote kisha wao hawawalipi mafundi (sub contractors) wasakwe, wawekwe ndani hadi wazitapike hizo fedha kwani jambo hilo linaichafua serikali kwa kuonekana kuwa hawalipi fedha za miradi kwa wakati jambo ambalo amesema si sawa.
  • Amesisitiza pia kuwa ziara hizo hazitakuwa za mara moja na watapita mikoa yote na kwa maeneo ambayo wameshapita wanafuatilia utekelezaji wa maagizo waliyoacha

View: https://www.youtube.com/live/-1ITpYS5V1c
 
Back
Top Bottom