Time Bandit
JF-Expert Member
- May 22, 2013
- 615
- 321
Sioni tatizo hata kidogo katika kauli hii....Huu ni ukweli usiopingika kwamba the public sector hapa nyumbani ni kama imekufa.Bandari ya Dar-es-salaam ni gateway ya almost 90% ya biashara za Tanzani na inafanya clearance ya USD $ 15 billion kila mwaka(60% ya GDP YETU)...Strategically and Geographically bandari hii ina nafasi kubwa kuliko hata ya Mombasa kwa sababu inatoa huduma kwa nchi 6 ambazo ni landlocked(Malawi,Zambia,DRC,Rwanda,Burundi,Uganda)Lakini uzembe na ufisadi unakwamisha sana mchango wa bandari hii katika pato la taifa.Juzi hapa tumepata taarifa kwamba bandari hii ndo ya mwisho Afrika kimapato.Sasa sijui tukiambiwa ukweli tunalalamika nini.Mikataba mibovu kama ya TICCS,ufisadi,uzembe,ukiritimba usioa wa lazima,wizi na udokozi ndo vinafanya kitega uchumi hiki kishindwe kabisa kuchangia vizuri ktk pato la taifa.Leo hii bunge linakaa na kupitisha sh 1,000/= ktk kila line ya simu ilhali tuna vitega uchumi vingi tu.Ukweli unauma lakini wenye busara wakiambiwa ukweli wanajipanga na kujirekebisha.Tujirekebishe!