From:
Cartels a threat to efficiency at port, JKIA, says Kamau - News - nation.co.ke 9/7/2013
Transport and Infrastructure Cabinet Secretary Michael Kamau gestures during a meeting with the Senate Committee on Energy and Transport at the Kenyatta International Conference Centre (KICC) July 9, 2013. On the left is Infrastructure Principal Secretary John Mosonik. ANN KAMONI
Waziri wa Usafirishaji na Miundo Mbinu wa Kenya Bwana Michael Kamau, leo ametoa kauli ya dharau kwa Tanzania kwenye kikao cha Kamati ya Seneti ya Wizara hiyo ya Usafirishaji na Miundombinu. Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa Kenyatta International Conference Center.
Wakati wa kikao hicho, pamoja na mambo mengine Bwana Kamau alisema: "iwapo watanzania wasingekuwa watu wa namna walivyo, bandari ya Mombasa ingekuwa imekufa kitambo. Kwa bahati nzuri, kwa mawazo yao ya kijamaa, hawawezi kupeleka vitu haraka"
If the Tanzanians were not people that they are; Mombasa would have died a long time ago. Fortunately, with their Ujamaa thinking, they are not able to develop things very fast,.
Maneno haya si maneno mazuri kutoka kwa Waziri wa nchi ambayo tunapanga kuingia nayo katika ushirikiano wa karibu katika Jumuiya ya Africa Mashariki.
Watanzania tunataka viongozi wetu wasimame imara na kuturudishia heshima mbele ya nchi za jirani na katika jumuiya ya kimataifa.
Ikumbukwe hivi karibuni tumesikia kauli za kejeli toka kwa Rais wa Rwanda, sasa hii nayo toka kwa Waziri wa Kenya na zingine zitafuata...
Watanzania wenzangu naomba maoni yenu.
Sioni ubaya wa maneno hayo. Kwani mlitegemea kiukweli kabisa wakenya wangependelea tz iwapiku? Ukweli ni kwamba, kama nchi, kenya kama zilivyo nchi zingine majirani, ni adui/mpinzani wa tz, na kamwe hawawezi furahia kusoma namba za nyuma za tz! Kenya ingependelea kubaki keleleni mwa EAC kiuchumi milele!
Hayo yaliyosemwa tuyapokee kama changamoto tukijua kuwa tunapaswa kuchangamka na tuache ubinafsi unaoididimiza nchi yetu.
sio swala la viongozi pekee yao bali ni la kila mtz, kwani viongozi wanatoka miongoni mwetu. Hebu jichukulie ww mwenyewe jichunguze unachangiaje ktk hali tuliyonayo nchini! Unafika ofisini kwa muda? unatimiza wajibu wako kikamilifu? Hebu fikiria usumbufu usio wa lazima uliopo bandarini kwetu. Fikiria hao watoa huduma ambao kimsingi wamesaini mikataba ya ajira na wanajua majukumu yao kabisa...lakini unakuta anapotezea muda na hela watu wengi sana. Huyo akipandishwa cheo anaendeleza mchezo huo huo...badala ya kupeleka mambo haraka haraka ktk kufanya maboresho ya bandari, fungu linakuwa 'diverged' sehemu kusiko, badala yake miundombinu inazidi kuchoka, na huduma zinazidi kudolola! Watu kama hawa wanao acha majukumu yao na kuweka 'bureaucracy' ndio wanaotutukanisha na kutudharaulisha! Hao wanaoiba vipuri na bidhaa bandarini, wanaochelewesha miundombinu isiboreshwe kwa wakati ndio wanaoinufaisha bandari ya mombasa, na kama hasira wao ndio wakuelekezewa. Na ukishawanyooshea kidole kimoja, vingine vinakusuta ww mwenyewe ktk sehemu yako ya kazi. Jawabu ni kutanguliza utaifa kabla ya ubinafsi wetu.
Ni muda muafaka kwetu kupokea chanamoto kama hizi na kuzifanyia kazi badala ya kuleta utetezi usio na tija. Heshima gani inayodaiwa kupotezwa kwenye ukweli? Hapo ni sawa na kukata kuwa uko uchi wakati kiukweli hujavaa nguo! Kama hatutaki kuyasikia maneno kama haya, solution ni moja tu...tutimize wajibu wetu kwa kuweka tz mbele na ubinafsi nyuma.
Haijarishi kenya ipo mbele au nyuma yetu, kama tukihakikisha utaifa kwanza, na kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu...tutaboresha maisha ya wananchi watz...na kwa mapenzi ya Mungu...kenya haitaweza hata kuyaona mavumbi yetu kwani tutawaacha mbali na kuwa meza moja na nchi kama china....inawezekana!
Kila mtz mahali alipo ajihoji mwenyewe badala ya kupiga kelele kwa viongozi, tukitimiza wajibu hata huyo anaejiita ni kiongozi mbona hawezi kufanya ujinga!?
Ujamaa hauna tatizo hapa, mbona kuna nchi nyingi tu zimefanikiwa na ujamaa wao!? Tatizo ni sisi wenyewe kutotimiza wajibu...tena kwa kuwa hatupendi kuambiwa maneno tusiyotaka kuyasikia...mie naomba wazidi tu kuyasema ili tupate hasira ya kuweka utaifa kwanza! tz ni kama 'sleeping giant' ktk EAC! I would like it to be unleashed!
Hata adui yako ukimsikiliza kwa makini unaweza pata vitu vya kukusaidia!