Waziri wa Kenya aidharau Tanzania

Waziri wa Kenya aidharau Tanzania

Wanasiasa wetu wamezidi kuifanya kenya ndo roll model ya maendeleo kila mbunge akisimama utaskia wenzetu kenya lakin ki ukweli hawa watu wana dharau sana na wanapenda mashindano yasiyokua na tija.. Lakin pia kauli yake ina ukweli ndan yake bandar yetu inashindwa kuchangamkia opportunity kwa wachache kuendekeza ubinafsi na sio mawazo ya kiujamaa kama alivyosema. Tungekua na viongozi shupavu na wazalendo mfano wa mwalimu serikali ya kenya ingebidi iombe msamaha.

Mkuu ukianza kuangalia yanayoendelea Tanzania kwa sasa ni lazima tukubaliane na jinsi tunavyodharauliwa. Dharau tumejitafutia wenyewe, wanaposema kuwa tunaakili mgandao inatokana na tunavyofanya mambo yetu. Mfano mzuri kabisa ni bandari yetu uliyoitaja.

Kama unaweza kukumbuka huko nyuma, Nyerere akiongea watu walikuwa wanasikiliza, na watu wakitaka kufanya jambo lolote kwenye nchi zao walikuwa wanakuja Tanzania.

Leo hata vikao muhimu vya kikanda nchi yetu inawekwa pembeni, sasa East African community inaanza kuonekana kuwa ni ya Kenya, Rwanda na Uganda. na kama utakuwa umefuatulia unaweza hata kusoma hapa JF anayosema Kagame kuhusu Tanzania na rais wetu.

Kutoka nchi iliyoheshimika duniani na Afrika nzima, na kuwa nchi ambayo Kagame anayweza kumkejeli rais wake, serikali yake na hata kumtishia, siwezi kushangaa waziri wa kenya kusema anayosema.
 
Fact... Inafika wakat mnataman huyo kagame apige hatua zaid ili akili za watawala ziamke na wananchi wafumbuke labda itatusaidia kubadilika
 
Hayo maneno ni kweli tupu kama tungeweka sawa bandari ya Tanga unazani mombasa port sj ingeshakufa zamani. Kwakuwa wabongo ukwwli hatuutaki na hizi ni dalili za kuathiliwa na ccm ambao ukweli kwak ni sumu tuchukue hiyo changamoto tuiue mombasa port
 
Mkuu ukianza kuangalia yanayoendelea Tanzania kwa sasa ni lazima tukubaliane na jinsi tunavyodharauliwa. Dharau tumejitafutia wenyewe, wanaposema kuwa tunaakili mgandao inatokana na tunavyofanya mambo yetu. Mfano mzuri kabisa ni bandari yetu uliyoitaja.

Kama unaweza kukumbuka huko nyuma, Nyerere akiongea watu walikuwa wanasikiliza, na watu wakitaka kufanya jambo lolote kwenye nchi zao walikuwa wanakuja Tanzania.

Leo hata vikao muhimu vya kikanda nchi yetu inawekwa pembeni, sasa East African community inaanza kuonekana kuwa ni ya Kenya, Rwanda na Uganda. na kama utakuwa umefuatulia unaweza hata kusoma hapa JF anayosema Kagame kuhusu Tanzania na rais wetu.

Kutoka nchi iliyoheshimika duniani na Afrika nzima, na kuwa nchi ambayo Kagame anayweza kumkejeli rais wake, serikali yake na hata kumtishia, siwezi kushangaa waziri wa kenya kusema anayosema.

Haya matatizo ya kutengwa na majirani yanatokana na kuwa na waziri wa mambo ya nje ambaye ni incompetent, sadly, anatamani kuwa rais. Pili tumekuwa na rais dhaifu mnooooo...

Tabia ya haya maCCM kuamini kuwa maendeleo yataletwa na wazungu na kutwa kucha kuzunguka nchi za Ulaya na Amerika kuomba msaada badala ya kujenga utegemezi ndio imetufikisha hapa. Nchi yetu haina uhusiano mzuri na majirani zake pande zote. Ingawa hatuna vita lakini bifu na Malawi bado bichi kabisa, tumeshindwa kuwatengenezea barabara wakongomani wapitishe mizigo yao kupitia Kigoma, tumeshindwa kuwatengenezea barabara ndugu zetu wa kihistoria Msumbiji ili wawe wanakuja kuleta na kufuata biashara Tanzania kwa LAMI, tumeshindwa kuwapunguzia umbali mrefu wazambia kwa kujenga Bandari ya Mtwara na barabara nzuri ya lami kutoka Mtwara hadi Tunduma ili mizigo yao isafiri umbali wa mfupi, pia kwa watu wa Malawi. Kwa ujumla ni kwamba serikali yetu dhaifu haijui majirani zetu wanataka nini kutoka kwetu na sisi tunataka nini kutoka kwao na hivyo tukae pamoja na kuwekeza ili kuleta maendeleo ya pamoja na sio kutembea na bakuli kwa wazungu.

Mfano mzuri wa Kenya kwa kutambua uwepo wa Sudan kusini wanao Mradi wa dola bilioni 30 kujenga bandari ya Lamu iweze kubeba mizigo yote ya Sudan Kusini. Sisi hata kuwekeza katika Bandari tuliyonayo tunashindwa, tunawatesa majirani zetu kwa kuwaongezea gharama katika biashara zao kwa kung'ang'ania kubeba mizigo na malori badala ya kuimarisha reli. Reli ikiimarika itapunguza sana gharama kwa nchi za Rwanda, Burundi, Kongo, Zambia, Malawi na hata Uganda. Sisi tumeachana na Reli na sasa tunawekeza katika Malori kwa kuwa ndio BIASHARA YA RIZIWANI...

Kama humsaidii jirani yako na yeye anakupotezea. Kagame hawezimkuendelea kuwakenulia meno watanzania wakati mnamuongezea wiki mbili kwenye kuufikisha mzigo nchini kwake kwa upuuzi wenu wa kutokuwa efficient, au kutoimarisha miundombinu. Undugu ni kusaidiana, wasidieni majirani zenu kwa kuwapatia huduma nzuri na kuwapunguzia gharama zisizo za lazima. CCM ndio imetufikisha hapa...
 
Hiyo ndio hali halisi hata wafanyabiashara na viongozi wa nchi yetu wanajua ila hakuna wa kumvisha paka kengele...

Bandari ya Dar es Salaam ni kimeo sana, na hii hupelekea hata wafanyabiashara wa Kitanzania kulazimika kutumia Bandari ya Mombasa...

Tena naona huyo Waziri katumia lugha ya staha kabisa, alipaswa kutuita jina mbadala zaidi ya hilo....
 
Wewe Mtu wa Shamba inaonekana watu wakisema ukweli kuhusu sisi Watanzania unahamaki. Hivi ueledi wa kuendesha uchumi wetu uko wapi? Leta mifano humu JF tuijadili.Nijuavyo Viongozi wetu kuanzia Mkuu wa kaya wamebobea kwa ufisadi na wizi wakupindukia.Mfano wa weledi wetu: Msanii Mkuu wetu karopoka kauli tete kuhusu Rwanda sasa kila aliye na ufinyu wa kufikiri analalamika kuwa Mkuu anadharauliwa na Kagame fedheha gani hii! Kamau kanena na kuzingatia tulivyo watu wa hovyo!?
From: Cartels a threat to efficiency at port, JKIA, says Kamau - News - nation.co.ke 9/7/2013

kamau.jpg
Transport and Infrastructure Cabinet Secretary Michael Kamau gestures during a meeting with the Senate Committee on Energy and Transport at the Kenyatta International Conference Centre (KICC) July 9, 2013. On the left is Infrastructure Principal Secretary John Mosonik. ANN KAMONI

Waziri wa Usafirishaji na Miundo Mbinu wa Kenya Bwana Michael Kamau, leo ametoa kauli ya dharau kwa Tanzania kwenye kikao cha Kamati ya Seneti ya Wizara hiyo ya Usafirishaji na Miundombinu. Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa Kenyatta International Conference Center.

Wakati wa kikao hicho, pamoja na mambo mengine Bwana Kamau alisema: "iwapo watanzania wasingekuwa watu wa namna walivyo, bandari ya Mombasa ingekuwa imekufa kitambo. Kwa bahati nzuri, kwa mawazo yao ya kijamaa, hawawezi kupeleka vitu haraka"
“If the Tanzanians were not people that they are; Mombasa would have died a long time ago. Fortunately, with their Ujamaa thinking, they are not able to develop things very fast,”.

Maneno haya si maneno mazuri kutoka kwa Waziri wa nchi ambayo tunapanga kuingia nayo katika ushirikiano wa karibu katika Jumuiya ya Africa Mashariki.

Watanzania tunataka viongozi wetu wasimame imara na kuturudishia heshima mbele ya nchi za jirani na katika jumuiya ya kimataifa.

Ikumbukwe hivi karibuni tumesikia kauli za kejeli toka kwa Rais wa Rwanda, sasa hii nayo toka kwa Waziri wa Kenya na zingine zitafuata...

Watanzania wenzangu naomba maoni yenu.
 
mi nafikiri iwe kama changamoto kwa viongoz wa tz ni aibu mpaka wagen wanajua maovu yao, 2badilike kama 2naka development
 
Sasa kama unafundisha class utashindwa tofautisha kati ya wa kwanza na wa mwisho baada ya mtihani. Kama kasema uongo uonyeshe uongo huo! KAMA NI KWELI BASI MWACHE ATUCHANE TU pengine makelele ya nje yatatuamsha.
 
Mambo kama haya yananitia hasira. Nashindwa kutoa comments. Inauma sana
 
Waziri anazuiwa na itifaki kutamka kauli tata zinazohusu nchi rafiki au nchi washirika.

Kumbuka Kenya tuko nao katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Jumuiya ipo katika kuendelea kuongeza ushirikiano kufikia muunganiko wa sarafu. Kauli kama hizi zinajenga kutoaminiana katika nchi na zinarudisha nyuma ushirikiano huo.

mtu shamba nimejaribu sana kutafuta namna ya kukujibu bila kukukwaza! samahani mkuu ni dhahir huna exposure kabisa ww maana mwenendo wa fikra zako ndio kikwazo kikubwa sana cha maendeleo nchini kwetu!
Yani tunaepuka kusema facts kisa eti itifaki hairuhusu! Viongozi wetu ni wajinga na wazembe, na kama sisi wananchi tumeshindwa kuwa hold responsible tumshukuru Mungu kuwa labda dharau kutoka nje zitawaamsha!
Sasa ww unataka usifiwe uongo jamani wakati ukweli uko wazi eti ndio itifaki inazingatiwa. What utter nonsense!
Unafahamu cobnstructive criticism?
 
I liked his argument! Watanzania ujamaa umetulemaza sana tumekuwa mazezeta. Yaani pamoja na umaskini wote tulionao na kuchelewa kote huku kwa maendeleo tulikonako utakuwa mijitu inakaa hapa kuitetea na kuisimamia CCM, sasa unabaki unajiuliza hivi tuna watanzania wenye akili timamu kweli. Worse enough watu walioenda shule wamekuwa waoga, hawahoji wala hawajishughulishi na chochote chenye impact kwa taifa lao. Hii nchi ni kama ina laana hivi. Inapata viongozi wachovu, lakini wakikosolewa wakali na wapo tayari kung'oa watu meno na kucha ili waendelee kuwepo madarakani.

lukolo umefunga kazi, kazi yetu sisi ni kusema ccm itatawala milele, akitokea mpinzani basi ana uchu wa madaraka; ila wao waliotawala kwa miaka 50 bila mafanikio ndio wenye haki na uwezo wa kutawala, utadhani tz haina watu wenye uwezo zaidi yao, jambo ambalo si kweli, hebu angalia jinsi Lowassa urais unataka kumtia kichaa, eti bado anatamani kuwa kiongozi. kazi mnayo watz.
 
Waziri anazuiwa na itifaki kutamka kauli tata zinazohusu nchi rafiki au nchi washirika.

Kumbuka Kenya tuko nao katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Jumuiya ipo katika kuendelea kuongeza ushirikiano kufikia muunganiko wa sarafu. Kauli kama hizi zinajenga kutoaminiana
katika nchi na zinarudisha nyuma ushirikiano huo.

Ndo mjue mnaungana na watu gani...ushirikiano wa kisiasa na yatokanayo hauwezi badili tabia na attitude...

Chungu kumeza lakini dawa!!!
 
From: Cartels a threat to efficiency at port, JKIA, says Kamau - News - nation.co.ke 9/7/2013

kamau.jpg
Transport and Infrastructure Cabinet Secretary Michael Kamau gestures during a meeting with the Senate Committee on Energy and Transport at the Kenyatta International Conference Centre (KICC) July 9, 2013. On the left is Infrastructure Principal Secretary John Mosonik. ANN KAMONI

Waziri wa Usafirishaji na Miundo Mbinu wa Kenya Bwana Michael Kamau, leo ametoa kauli ya dharau kwa Tanzania kwenye kikao cha Kamati ya Seneti ya Wizara hiyo ya Usafirishaji na Miundombinu. Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa Kenyatta International Conference Center.

Wakati wa kikao hicho, pamoja na mambo mengine Bwana Kamau alisema: "iwapo watanzania wasingekuwa watu wa namna walivyo, bandari ya Mombasa ingekuwa imekufa kitambo. Kwa bahati nzuri, kwa mawazo yao ya kijamaa, hawawezi kupeleka vitu haraka"
“If the Tanzanians were not people that they are; Mombasa would have died a long time ago. Fortunately, with their Ujamaa thinking, they are not able to develop things very fast,”.

Maneno haya si maneno mazuri kutoka kwa Waziri wa nchi ambayo tunapanga kuingia nayo katika ushirikiano wa karibu katika Jumuiya ya Africa Mashariki.

Watanzania tunataka viongozi wetu wasimame imara na kuturudishia heshima mbele ya nchi za jirani na katika jumuiya ya kimataifa.

Ikumbukwe hivi karibuni tumesikia kauli za kejeli toka kwa Rais wa Rwanda, sasa hii nayo toka kwa Waziri wa Kenya na zingine zitafuata...

Watanzania wenzangu naomba maoni yenu.

Tuna bandari za Tanga, Dar es Salaam na Mtwara ila bado mizigo mingi ya kanda ya kaskazini inapitia Mombasa badala ya Tanga, kwanini asiseme mawazo ya kijamaa yasiyoweka mbele utaifa ndiyo yanawafanya Watanzania wapitishie mizige Mombasa badala ya Tanga?
 
Hivi...ni nini role ya waziri wa mambo ya nje, waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki, na wabunge wa afrika mashariki katika hizi choko choko na dhiaka ambazo viongozi mbali mbali wa Kenya, Uganda na Rwanda wanazitupa kwetu!?
Ni kweli, hawa mabwana wanapaswa kusimama na kuitetea nchi. Kunyamaza kimya kwa kauli kama hizi kunatufanya tuzidi kudharaulika.
Hata kama hawatasema kwa maneno, lakini ni wakati sasa wa kufanya mambo hata kwa vitendo ili kuwajibu hao watu. Mathalani, tunaweza kufanya kweli kwenye ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo inaweza kuiua hiyo bandari ya Mombasa
 
Wewe kama huoni ubaya nenda basi huko uhamie Kenya unakowaona wa maana. Tuachie Tz yetu na ujamaa wetu.

we acha mawazo finyu jifunze kutoka kwa wenzio walikuwa mbele na siyo kuwa na mawazo kigamba hatutaendea kwa staili hiyo
 
Binafsi namshukuru huyu Waziri kwa kauli yake, maana katupa mbinu ya kuiua Bandari ya Mombasa.
Ukiwa na mtu anayependa kulala usingizi kupitiliza na kila ukimwamsha hataki kuamka, inabidi utumie njia mbadala kama kumchapa kiboko au kummwagia maji.
Hizi kejeli na dharau tunazozipata tunastahili kuzipata kwa sababu ya utendaji mbovu wa viongozi wetu.
Tanzania ingekuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uchumi nzuri barani Africa, kama siyo Umbulula, Ufisadi, na Ubinafsi wa Viongozi wa Serikali ya CCM.
 
Kwani Makosa ya Waziri iko wapi?.Waziri hii ya Nyayo inaletea sisi changamoto ya kujichungusa na kurekebisa mipango yetu ya namna nzuri ya kufanya kasi zetu kama nchi na kuacha hii ubabaisaji ilyopo ndani ya Nchi hii.
 
Ni kweli, hawa mabwana wanapaswa kusimama na kuitetea nchi. Kunyamaza kimya kwa kauli kama hizi kunatufanya tuzidi kudharaulika.
Hata kama hawatasema kwa maneno, lakini ni wakati sasa wa kufanya mambo hata kwa vitendo ili kuwajibu hao watu. Mathalani, tunaweza kufanya kweli kwenye ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo inaweza kuiua hiyo bandari ya Mombasa

Bandari ya Bagamoyo ya nini? Ishughulikiwe Bandari ya Tanga.
 
Kwani Makosa ya Waziri iko wapi?.Waziri hii ya Nyayo inaletea sisi changamoto ya kujichungusa na kurekebisa mipango yetu ya namna nzuri ya kufanya kasi zetu kama nchi na kuacha hii ubabaisaji ilyopo ndani ya Nchi hii.

Wewe ni Chalii ya wapi, Nyeri au Machakosi?
 
Back
Top Bottom