Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo

JOSE KASANO

Senior Member
Apr 23, 2013
120
93
Habari wanabodi,

Bila shaka kila mmoja wetu anafahamu pilikapilika za wanafunzi kusoma shuleni. Imekuwepo tabia ya baadhi ya shule kuwabakiza wanafunzi kipindi cha likizo kwa kigezo cha kuwaandaa na mitihani ya taifa.

Kitendo hicho ni kinyume na sera pamoja na miongozo ya elimu inayomuhitaji mtoto ajumuike na wazazi wake kipindi cha mapumziko.

Mwaka jana serikali walitoa tamko lililopiga marufukuku wabakiza watoto shuleni kipindi cha likizo ili wajumuike na wazazi na ndugu zao pamoja na jamii kwa ujumla.

Katika kuelekea likizo hii ya mwezi juni 2023, tayari baadhi ya shule zimeanza harakati za kuwabakiza watoto shuleni kwa kigezo hicho hicho ambacho Kishimba (mbunge) huwa anapingana nacho siku zote lakini huwa hawamuelewi. Kutafuta ufaulu wa kwenye karatasi tu kwenye mfumo wa elimu.

Tunayo matumaini kuwa Mh. Waziri wa Elimu, Prof. Mkenda na wasaidizi wake watalichukulia maanani hili, waelekezeni maafisa elimu, wakuu wa shule msingi na sekondari waruhusu watoto wote wajumuike na wazazi wao kipindi cha likizo.

Faida za mtoto kwenda likizo:-

1. Kujumuika na kukaa na wazazi wake kwenye familia katika mambo mbalimbali ya kifamilia.

2. Kuwatambua na kutengeneza mahusiano na ndugu zake kwenye famila.

3. Kuwatambua ndugu na jamaa zake wengine mfano wajomba,mashangazi,baba wadogo,mama wadogo na wakubwa,mababu.Mabibi nk.

4. Kuwatambua wanajamii wengine na kushiriki shughuli nyinginezo za kijamii nje ya shule tofauti na kubaki na walimu na shughuli za shule tu muda wote mfano,misiba,harusi,mikutano,kujitolea kwenye shughuli kadha wa kadha.

5. Kutambua na kubaini maisha mbadala baada ya shule hususani fursa za kiuchumi kwenye jamii.

Hizo ni baadhi tu kutaja kwa ajili ya msisitizo.

Tunawasilisha
 
Hoja hazina mantiki hizi, ninachofahamu sio lazima mtoto akabaki shule kipindi Cha likizo kamchukue mwanao apumzike likizo.
 
Mbaya zaidi hawa watoto wamepigishwa kwata kwa siku sita za wiki kuanzia saa kumi na mbili asubui hadi saa mbili usikua wakisa wanakaririshwa masomo. Profesa tunaomba uingilie kati hawa watoto bado ni wadogo wengine hata miaka kumi na mbili hawajafikisha.
 
Mimi toka nasoma sijawahi bakizwa shule, iweje elimu ya sasa ambayo ni nyepesi watoto wabakizwe shule?

Kama mzazi wajielewa mchomoe mtoto wako.

Shule zenye mambo ya kipumbavu wapaswa hamisha mtoto.

NB: Kuna wazazi wapumbavu ndo hushirikiana na shule
 
Elimu si tu ile ya shuleni hata kujifunza kazi za nyumbani ni elimu kubwa sana .Na wengi wakimaliza shule zile kazi za nyumbani ambazo hazipewi uzito ndio zinakuwa ajira zao :mfano mama ntilie ,udereva ,kusuka,Kinyozi, wengine kuolewa.kilimo,ufugaji.
 
Shule zinalazimimisha watoto kubaki shuleni haswa Anazak,Tusiime,Righty way na nyinginezo kama hizo kisa tu wanataka wanafunzi wapate A.
Kwani wakipata A ni vibaya.? Je mwanao ulimpeleka pale aidhalilishe kupata F,? Baba mhamishe mwanao mpeleke shule za kijinga akapate unachotaka
 
Back
Top Bottom