Waziri wa Elimu Prof. Mkenda, sisitiza umuhimu wa kutowabakiza watoto shule kipindi cha likizo

Habari wanabodi,

Bila shaka kila mmoja wetu anafahamu pilikapilika za wanafunzi kusoma shuleni. Imekuwepo tabia ya baadhi ya shule kuwabakiza wanafunzi kipindi cha likizo kwa kigezo cha kuwaandaa na mitihani ya taifa.

Kitendo hicho ni kinyume na sera pamoja na miongozo ya elimu inayomuhitaji mtoto ajumuike na wazazi wake kipindi cha mapumziko.

Mwaka jana serikali walitoa tamko lililopiga marufukuku wabakiza watoto shuleni kipindi cha likizo ili wajumuike na wazazi na ndugu zao pamoja na jamii kwa ujumla.

Katika kuelekea likizo hii ya mwezi juni 2023, tayari baadhi ya shule zimeanza harakati za kuwabakiza watoto shuleni kwa kigezo hicho hicho ambacho Kishimba (mbunge) huwa anapingana nacho siku zote lakini huwa hawamuelewi. Kutafuta ufaulu wa kwenye karatasi tu kwenye mfumo wa elimu.

Tunayo matumaini kuwa Mh. Waziri wa Elimu, Prof. Mkenda na wasaidizi wake watalichukulia maanani hili, waelekezeni maafisa elimu, wakuu wa shule msingi na sekondari waruhusu watoto wote wajumuike na wazazi wao kipindi cha likizo.

Faida za mtoto kwenda likizo:-

1. Kujumuika na kukaa na wazazi wake kwenye familia katika mambo mbalimbali ya kifamilia.

2. Kuwatambua na kutengeneza mahusiano na ndugu zake kwenye famila.

3. Kuwatambua ndugu na jamaa zake wengine mfano wajomba,mashangazi,baba wadogo,mama wadogo na wakubwa,mababu.Mabibi nk.

4. Kuwatambua wanajamii wengine na kushiriki shughuli nyinginezo za kijamii nje ya shule tofauti na kubaki na walimu na shughuli za shule tu muda wote mfano,misiba,harusi,mikutano,kujitolea kwenye shughuli kadha wa kadha.

5. Kutambua na kubaini maisha mbadala baada ya shule hususani fursa za kiuchumi kwenye jamii.

Hizo ni baadhi tu kutaja kwa ajili ya msisitizo.

Tunawasilisha
Mwenye huo waraka naomba pdf
 
Back
Top Bottom