The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
1. Mwanangu amechaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita (F. V & VI) mwaka huu 2021 Shule ya Sekondari Nyantakara katika tahususi (Combination) ya Chemistry, Biology & Geography (CBG) iliyoko wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera. Hii ni shule ya serikali ya Tanzania.
2. Licha ya orodha ya mahitaji mengi anayotakiwa aende nayo mfano; fagio wa kufagilia ndani, sabuni ya maji ya chooni, fagio wa kufagilia nje, ream ya kataratasi nk nk, lipo hili ambalo mimi limeniacha hoi hata kujiuliuza kulikoni hizi shule za serikali? Nimeambiwa nimnunulie mwanangu
[A.] Vitabu yote vya tahasusi (subject combinations) anayokwenda kusoma yaani CBG & Basic Applied Maths
[B.] Dissecting Kit ya somo la Bailojia
3. Nikajiuliza ina maana shule hii anayokwenda kusoma mwanangu haina vitabu? Imekuwaje inaanza kidato cha tano huku ikiwa haina vitabu? Kipi kilipaswa kuanza, majengo au vitabu na walimu kwanza? Hivi mzazi kama nanunua vitabu vyangu kwa ajili ya mwanangu, si bora asomee nyumbani sasa na siku ya mtihani aende kufanya tu?
4. Nimelileta humu tujadiliane ili tujue majigambo ya serikali kuwa imeboresha elimu Tanzania, yana maana gani kama hali iko hivi ktk shule zake?
4. Naambatanisha na Joining instructions ya shule kwa ajili ya ushahidi na reference zaidi kwa atakayetaka kuthibitisha maelezo yangu.
5. Honestly, baada ya kuipata hii fomu ya maelekezo, nimeanza kusaka fedha tu na kufikiri kumpeleka shule ya binafsi.