Waziri Tabia Mwita Azinduza Tunzo za Kimataifa za Muziki Zanzibar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Mh. Tabia Maulid Mwita, amesema Serikali itaendelea kusimamia sanaa ya Zanzibar katika kuimarisha miundombinu itakayowawezesha wasanii kuzalisha kazi zao katika mazingira mazuri.

Akizungumza katika uzinduzi wa tunzo ya Zanzibar International Music waziri Tabia amesema hivi sasa wasanii wanafanya kazi katika mazingira magumu jambo ambalo linasababisha kutofikia malengo .

Amesema Serikali inadhamira njema ya kuwasaidia wasanii hivyo ina mpango wa kujenga chuo cha sanaa kitakacho wawezesha wasanii kujiendeleza na kuweza kuzalisha kazi zao ili ziendane na soko la sanaa la kimataifa.

Amesema sanaa ni zao la utamaduni hivyo, watahakikisha wanasimamia masuala ya utamaduni na masuala ya sanaa ili kuwaendeleza wasanii na kufikia malengo yao.

amesema wasani wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali hali ambayo wanashindwa kufikia malengo na kuwataka kukaa pamoja ili kutatuwa matatizo yao kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Pia, amewataka wasanii hao kuendelea kujituma kwa kuzitangaza kazi zao vizuri kwa lengo la kufika mbali na kupata mafanikio.

Akitaja utaratibu wa ugawaji wa tunzo Mwenyekiti wa kamati ya Zanzibar international Music awards Ramadhan Bukini amesema tasnia mziki imekua kwa kasi hivyo ni lazima kwa wasanii kufanya muziki unaoendana na soko la kibiashara.

Hata hivyo, Bukini amewataka wasanii hao kuzisajili kazi zao kwani kufanya hivyo kutawarahisishia kupata kipato kizuri.

Katibu mtendaji wa baraza la sanaa Taifa ( BASATA) Dkt Kedmon Mapana, amesema kuanzishwa kwa tunzo kutasaidia wasanii kupata fursa ya kutangaza kazi zao na kujulikana kimataifa.

Amesema tunzo ndio msingi pekee wa kuibuwa na kuendeleza vipaji vya wasani mbalimbali ambayo vitawahamasisha kufanya kazi kwa weledi.

Nao wasanii wamesema wamefurahishwa na hatua ya Serikali ya kuweka tunzo kwani zitasaidia kujitangaza na kufika mbali.

WhatsApp Image 2023-10-28 at 15.24.16.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-28 at 15.24.16(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-28 at 15.24.18(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-28 at 15.24.19.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-28 at 15.24.19(1).jpeg
 
Back
Top Bottom