Waziri Tabia Mwita Azindua Mradi wa Kukuza Maendeleo ya Utamaduni Zanzibar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

WAZIRI TABIA MWITA AZINDUA MRADI WA KUKUZA MAENDELEO YA UTAMADUNI ZANZIBAR

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Tabia Mwita Maulid amezindua Mradi wa UNESCO - ALWALEED PHILANTHROPIES unaolenga kukuza Maendeleo ya kijamii kupitia Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) na ajira zinazohusiana na Utamaduni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo mjini Zanzibar, Oktoba 24, 2023 amesema mradi huo utasaidia kutoa elimu ya kulinda Utamaduni pamoja na wadau wa Utamaduni kunufaika na bidhaa za Utamaduni.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Nicholas Mkapa amesema mradi huo utanufaisha vijana katika Utengenezaji wa Filamu, Muziki na Sanaa kwa kukuza uchumi na kuwawezesha vijana kupata kipato.

Aidha, mwakilishi wa UNESCO hapa nchini Dkt. Michael Toto amesema lengo la Mradi huo ni kukuza maendeleo ya jamii ya Tanzania kwa kutoa elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na ajira zinazotokana na Utamaduni.

F9WL6GMWAAEc_s8.jpg

F9WL7IlXgAAG53C.jpg
F9WL7udWUAA5n-1.jpg
F9WL8bkXAAANByT.jpg
 
Back
Top Bottom