Waziri Nape Nnauye, inakuaje unajisifu kuona Watanzania milioni 5 ndio wako online? Je, nia ya kutaka 100% wawe connected ni ya kweli au siasa?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Waziri wa Mawasiliano, Nape Nnauye akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Mkoa ya Rufaa, Lindi amejisifu kuwa na digital divide kubwa mbali na kuwa yeye ndiye Waziri wa mawasiliano, tukiamini anafanya kazi kuhakikisha watu wanakuwa online kama ambavyo bajeti ya serikali ya mwaka 2023/24 na Rais Samia wamejinasibisha kutaka watu wote wawe connected.

Nape amesema walioko mtandaoni ni 16% ambapo 40% kati yao wako nje ya nchi. 40% ya 16% ni 6.4%. Maana yake ni kwamba watanzania walioko Tanzania ambao wako mtandaoni ni 9.6%.

Wakati huo TCRA wanatuonesha kwamba kwa mwezi Juni 2023 kulikuwa na digital devices 34,047,407 zilizokuwa subscribed mtandaoni. Devices hizi zinaonesha kwamba watu wengi wapo connected tofauti na anavyosema Waziri, je nani tumuamini?

Tuendelee. Kwa kuwa watanzania 9.6% ya watanzania ndio wako mtandaoni maana yake katika vifaa milioni 34 vinavyotangazwa na TCRA ni vifaa 3,273,837 ambavyo vina access ya mtanadao.

Hata hivyo kwa watanzania milioni 61, tukisema waliokuwa connected ni 9.6% maana yake ni watanzania 5,856,000 walioko mtandaoni.

Rais Samia aliwahi kusema kwamba anataka kuona watanzania 100% wanakuwa mtandaoni kufikia mwaka 2030. Bajeti ya serikali na sera ya TEHAMA zinaonesha nia ya kutaka watanzania kuwa connected lakini Waziri anayesimamia suala hilo anajisifu Watanzania wachache kuwa mtandaoni. Je, Tanzania ya kidigitali itafikiwa?

Nimejiuliza sana huyu Nape waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari kusema uongo kwa Rais tena hadharani ni kiburi chake tuu au anamdharau anaye muaddress yaani Rais?

Majuzi huyu huyu na watu wa TCRA walikuwa wanatamba kuwa kiwango cha watumiaji wa Internet kimepanda sana hadi kufikia users zaidi ya milioni 36 nchi nzima.

Sasa hizi Habari za users mil 9 au 16% ya watanzania inatoka wapi tena? Anataka kutuaminisha kuwa basi taifa hili liko chini sana kima endeleo ya technology ya Habari kuliko nchi nyingi sana duniani?

Kama anaweza kutoa habari za uongo kwa Rais hadharani, jee huko ofisini anamvunga kiasi gani?

Naye mama Samia anashida gani mbona anapenda kulea uongo na waongo?

View: https://youtu.be/kkAeHH-vvfE?si=fsv07bOiBb9rY4iU
 
Waziri wa Habari Mh. Nape anesema siyo kila mtumia Internet anatumia Mitandao ya Kijamii.

Nape anasisitiza kuwa huu ni Ukweli mchungu kwa wanaodhani Dunia yote wanatumia Social media.

Ameandika kwenye Ukurasa wake wa X.

Wale mnaopinga 16% njooni mjibu siyo mnakurupuka tu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ”ฅ๐Ÿผ.
 
Waziri wa Habari mh Nape anesema siyo kila mtumia Internet anatumia Mitandao ya Kijamii

Nape anasisitiza kuwa huu ni Ukweli mchungu kwa Wanaodhani Dunia yote wanatumia Social media

Ameandika kwenye Ukurasa wake wa X

Wale mnaopinga 16% njooni mjibu siyo mnakurupuka tu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ”ฅ๐Ÿผ
Anajaribu kuwatoa maana watumia mitandao wakati yeye na serikali yake wote wana accounts za hiyo mitandao na wanazitumia kutoa updates mara nyingi zaidi kuwafikia hao wana mitandao kulinganisha na zinazowafikia wananchi wa Kawaida.

Nape ni mpuuzi na nusu, anatengeneza vita isiyo na tija yoyote ile.
 
Waziri wa Habari Mh. Nape anesema siyo kila mtumia Internet anatumia Mitandao ya Kijamii.

Nape anasisitiza kuwa huu ni Ukweli mchungu kwa wanaodhani Dunia yote wanatumia Social media.

Ameandika kwenye Ukurasa wake wa X.

Wale mnaopinga 16% njooni mjibu siyo mnakurupuka tu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ”ฅ๐Ÿผ.
Labda watoto wadogo na wazee!
Lakini kwa watu wazima asilimia kubwa kama hayupo twiter basi anatumia facebook, whatsapp, linkeldin nk
 
Waziri wa Habari Mh. Nape anesema siyo kila mtumia Internet anatumia Mitandao ya Kijamii.

Nape anasisitiza kuwa huu ni Ukweli mchungu kwa wanaodhani Dunia yote wanatumia Social media.

Ameandika kwenye Ukurasa wake wa X.

Wale mnaopinga 16% njooni mjibu siyo mnakurupuka tu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ”ฅ๐Ÿผ.

As of April 2023, there were 5.18 billion internet users worldwide, which amounted to 64.6 percent of the global population. Of this total, 4.8 billion, or 59.9 percent of the world's population, were social media users.

Source:
 
Waziri wa Habari Mh. Nape anesema siyo kila mtumia Internet anatumia Mitandao ya Kijamii.

Nape anasisitiza kuwa huu ni Ukweli mchungu kwa wanaodhani Dunia yote wanatumia Social media.

Ameandika kwenye Ukurasa wake wa X.

Wale mnaopinga 16% njooni mjibu siyo mnakurupuka tu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ”ฅ๐Ÿผ.

Waziri wa Habari Mh. Nape anesema siyo kila mtumia Internet anatumia Mitandao ya Kijamii.

Nape anasisitiza kuwa huu ni Ukweli mchungu kwa wanaodhani Dunia yote wanatumia Social media.

Ameandika kwenye Ukurasa wake wa X.

Wale mnaopinga 16% njooni mjibu siyo mnakurupuka tu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ”ฅ๐Ÿผ.
Mbona jamaa anapaparika san na majority ya social media? Kuna nn anahofia
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Kazi kweli kweli!
Angalia huyu Nape anavyopingana na maneno yake mwenyewe na ya Rais.
Jee anataka kutuaminisha kuwa wote ni waongo?
 
Waziri wa Habari Mh. Nape anesema siyo kila mtumia Internet anatumia Mitandao ya Kijamii.

Nape anasisitiza kuwa huu ni Ukweli mchungu kwa wanaodhani Dunia yote wanatumia Social media.

Ameandika kwenye Ukurasa wake wa X.

Wale mnaopinga 16% njooni mjibu siyo mnakurupuka tu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ”ฅ๐Ÿผ.
Anajiyekenya na kujichekesha mbele ya kioo

Waziri Nape enzi zimeisha
 
Back
Top Bottom