Waziri Nape Nnauye aomba kura za chaguzi zipigwe Mitandaoni "Electronic Voting"

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema nia Serikali ni kuhakikisha inakamilisha mchakato ili ikiwezekana chaguzi zijazo zitumie teknolojia ikiwememo Mtu kupiga kura mtandaoni badala ya kupanga foleni na kusubiri muda wa kupiga kura ambapo amesema hilo linawezekana kwakuwa Watanzania Milioni 34 wanatumia internet.

Waziri Nape amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam kupitia Jukwaa la Uhuru wa Internet Africa “Forum on Internet Freedom in Africa 2023” ambalo limehusisha zaidi ya Mataifa 30, huku idadi ya Washirikii ikiwa ni zaidi ya 200.

“Commitment ya Nchi ni kuhakikisha kwamba ikiwezekana chaguzi zijazo ziwe chaguzi zinazotumia teknolojia kwamba kwanini isifike mahali kuwe na uwezo wa mtu kupiga kura mtandaoni awe na uwezo wa kupiga kura popote alipo badala ya kwenda kupanga foleni na kusubiri muda wa kura, chaguzi zijazo zitumie Teknolojia ikiwemo mtu kupiga kura mtandaoni badala ya kupanga foleni na kusubiri muda wa kupiga kura”

Electronic Voting kwa kifupi ikifahamika kama e-voting ni aina ya uchaguzi unaofanyika kielektroniki ambapo mfumo huo usaidia katika kuchagua mgombea na kuhesabu kura kidijitali zaidi.

Kuna aina mbili za Electronic Voting.

1. e-voting at polling station: ambapo uchaguzi ufanyika katika kituo cha upigaji kura na mashine maalumu zinazoitwa Electronic Voting Machine (EVM) ufanya kazi mbalimbali za uongozaji wa kumsaidia mtu kuchagua mgombea anayemtaka kidijitali. Hivyo hivyo nazo zimegawanyika;

kuna zile ambazo mnapiga kura kwenye karatasi lakini yenyewe inahesabu kwa kuangalia umechagua mgombea yupi na kuzihesabu karatasi zote za kura na mwisho kukupa majibu ya idadi ya kura.

na Kuna zile mashine zenyewe zinakuwa kama simu, unabonyeza tu sura ya mgombea kisha inatunza taarifa na badae kujumuisha zote zilizopigwa na kutoa majibu ya waliopiga kura. Na aina zote hizi ufanyika katika kituo cha kupigia kura cha eneo husika, na anakuwepo msimamizi wa kituo.

2. Online Voting: Upigaji kura huu ufanyika mahali popote ambapo mpiga kura yupo, na inakubidi mpiga kura utumie simu au kifaa chochote cha internet. Hii ni aina ambayo upigaji kura wake umekuwa maarufu zaidi katika mashirika na serikalini. Ambapo kunakuwa na Website au Server maalumu ambayo mpiga kura ataingia kwa kutumia kifaa chake kisha ataweka namba yake ya uthibitisho kama ni yeye mfano namba ya mpiga kura, ya NIDA au itakayohitajika ili hasijirudie kupiga kura, kisha atapiga na kuchagua mgombea anayemtaka.


Mfumo huu kwa ujumla unafanyika katika nchi mbalimbali Duniani, mfano Marekani. Na uchaguzi wa aina hii unafaida kama kuokoa muda, kurahisisha kuhesabu kura kwa sababu mfumo wenyewe ndio unajiendesha, hivyo majibu hutoka haraka. Athari ni kama Mfumo ukizingua (machine error au server error), kushindwa kufanya kazi (shutdown, jam) , ukidukiliwa na wataalamu wa Teknolojia (hacking) kisha watu wakapanga matokeo yao. Inahitaji teknolojia ya hali ya juu kulinda upiga kura wa aina hii zidi ya mahalamia, kwa sababu mtu ambaye hajui kutumia teknolojia anaweza kuibiwa kura ambapo anayemuelekeza akapiga kwa niaba yake bila kujua, kwa sababu ni kubonyeza tu mashine au simu.
 
Bilashaka aliteleza katika matamshi yake.Kufanyika hilo,labda mwaka 2095,siyo miaka hii ya karibuni.
 
Wakiiruhusu hii hawatakuwa tena madarakani
Hawatakuwepo madarakani kivipi... Uchaguzi wa haina hiyo ni sawa na kumpa kichaa Rungu... Mtakungutwa mpaka muombe poo, maana hiyo Mifumo sisiem wenyewe ndio watatengeneza, na wao ndio watakaokuwa wanajua waguse wapi kwenye mfumo kuiba kura
 
Bilashaka aliteleza katika matamshi yake.Kufanyika hilo,labda mwaka 2095,siyo miaka hii ya karibuni.
Huo mfumo ukipitishwa basi, vyama pinzani visahau kushinda 😂... Wazee watakuwa wanapiga kona wao na kufunga wao
 
Wanataka wacheze na system ama ni mpango wa kumpindua bi.tozo..

Huko kijijini kwenye ccm kindaki ndaki hawajua hata maswala ya smartphone itakuaje?
😂 Huko kijijini watafahamu tu kupiga kura, mbona NIDA wanazo.... Ambao hawana smartphone, watapewa namna mbadala kama kutumia viswaswadu kwa kubonyeza mfano *160*066# au wataambiwa watumie simu za wenzao.

Serikali ikiamua hakuna cha kushindikana
 
huyu watamwondoa, kwasababu anataka washindwe. tukipiga kura electronic tu CCM itaanguka asubuhii na mapema.
 
huyu watamwondoa, kwasababu anataka washindwe. tukipiga kura electronic tu CCM itaanguka asubuhii na mapema.
Braza labda sio kwa Sisiem hii... Maana hata watakao tengeneza mifumo hiyo ni hao hao sisiem, kwa hiyo hawatashindwa kuikorokocha na kuweka kura zao bandia
 
Braza labda sio kwa Sisiem hii... Maana hata watakao tengeneza mifumo hiyo ni hao hao sisiem, kwa hiyo hawatashindwa kuikorokocha na kuweka kura zao bandia
ila kuna siku Mungu atawaondoa, confusion itawapata, watajiondoa wenyewe kwa wenyewe hata hawatajua wanafanya nini hadi watakapojikuta wapo ndani ya kiota.
 
Back
Top Bottom