Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,330
- 24,215
Yanayoendelea katika mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kwa sasa hivi hanasikitisha. Kenya ni jirani yetu na jirani ni ndugu.
Hivyo basi, matukio matatu ya haraka haraka yaliyotokea yanatushangaza. Kwanza ndege ya ujumbe wa Kenya ili rudi au kurudishwa Nairobi hivi majuzi.
Ndege hii ilikuwa na ujumbe wa viongozi waliokuwa wanakuja kuaga na kuhani msiba wa Mzee Mkapa.
Pili, Kenya iliondoa ukaribisho kwa Watanzania, kati ya nchi nyingi, kwenda Kenya ati kutokana na janga la Korona.
Tatu, leo Tanzania kwa kulipiza kisasi imeondoa ruksa ya ndege za Kenya, KQ kutua Tanzania toka tarehe 1 Agosti, yaani kesho.
Sasa hapa napata wasi wasi juu ya ukaribu na mfululizo wa matukio haya.
Je, hakuna hotline kati ya wizara za nje kati ya Kenya na Tanzania?
Kweli watu wanafanya kazi zao kwa weledi hadi mambo yatokee hadharani na kuzivunjia heshima nchi zote mbili?
Mimi nayachukulia masuala haya kama failure in Diplomacy, na watu inabidi wawajibishwe.