Waziri na Wizara ya Mambo ya Nje wanashindwa majukumu yao: tit fot tat na Kenya

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,169
23,860
Yanayoendelea katika mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kwa sasa hivi hanasikitisha. Kenya ni jirani yetu na jirani ni ndugu.

Hivyo basi, matukio matatu ya haraka haraka yaliyotokea yanatushangaza. Kwanza ndege ya ujumbe wa Kenya ili rudi au kurudishwa Nairobi hivi majuzi.

Ndege hii ilikuwa na ujumbe wa viongozi waliokuwa wanakuja kuaga na kuhani msiba wa Mzee Mkapa.

Pili, Kenya iliondoa ukaribisho kwa Watanzania, kati ya nchi nyingi, kwenda Kenya ati kutokana na janga la Korona.

Tatu, leo Tanzania kwa kulipiza kisasi imeondoa ruksa ya ndege za Kenya, KQ kutua Tanzania toka tarehe 1 Agosti, yaani kesho.

Sasa hapa napata wasi wasi juu ya ukaribu na mfululizo wa matukio haya.

Je, hakuna hotline kati ya wizara za nje kati ya Kenya na Tanzania?

Kweli watu wanafanya kazi zao kwa weledi hadi mambo yatokee hadharani na kuzivunjia heshima nchi zote mbili?

Mimi nayachukulia masuala haya kama failure in Diplomacy, na watu inabidi wawajibishwe.
 
Sema hawajui pia anachokitaka boss wao
 
Attachments

  • IMG-20200731-WA0090.jpg
    IMG-20200731-WA0090.jpg
    63.2 KB · Views: 2
Mkuu Kenya tupende tusipende hatuwezi kuikwepa kibiashara. Kenya ndio nchi ya pili kwa ukubwa wa biashara na Tanzania.

Hivyo tuyalee mahusiano hayo.

Ukubwa jinga wao usitufanye watupande vichwani mwetu, Tz ni Taifa huru na maendeleo yetu yanawategemea sana watanzania wenyewe na si hao vibaraka,waendelee tu na upuuzi wao tuone nani atakayeloose zaidi.
 
Sasa mkuu ndege imeshindwa kuja bongo kisa hali ya hewa unataka wizara ya mambo ya nje ifanye nini? Kuna diplomasia ya kutuliza hali ya hewa? Au kenya kuzuia watanzania kufika kwao kisa corona ni swala la kiafya hilo na wako sahihi tu, ili tusiambukizane corona yafaa kila mtu abakie nchini kwao. Sasa kuna diplomasia gani hapo inahitajika katika corona na muingiliano wa watu?

Ndege kuzuiwa kufika ni swala la wizara ya uchukuzi hilo. Na hiyo ni hatua kulingana na janga hili la corona. Kenya ipo corona sana sasa waje huku watuletee corona? Au watoke na corona huku? Na pia kwa nini imekataza vibali vya ndege zetu kutua kwao wakati zao zinakuja kwetu? Hili mamlaka za usafiri wa anga wamalizane wenyewe.
 
Tuliokuwepo miaka ya Iddi Amin mambo yalianza na masuala ya kijinga tu. Mwisho wake tuliona nani waliumia-wananchi pande zote.
 
Kenya na Tanzania kuna escalation of conflict inafanyika. Ni ujinga kutengeneza maadui bila sababu za maana. Yani India na Pakistan wanagombea Kashmir, China na India wanagombea mpaka afu sisi tunazozana kisa ugonjwa uliokuja wenyewe.

Kila mmoja anahitaji mwenzake, FM za nchi zote mbili zinafanya uzembe. Hatuna haja ya kuishi na Kenya kama possible enemy wakati tunaye Malawi ambaye miaka ijayo muda wowote ataibuka tu na clause yake. Tuache umwamba, mkishakuwa majirani kisha mnadindiana mnakosa wote tena na kuhatarisha mapigano.
 
Tuliokuwepo miaka ya Iddi Amin mambo yalianza na masuala ya kijinga tu.
Mwisho wake tuliona nani waliumia-wananchi pande zote.

Mkuu, ishu ya nduli na hii ni tofauti kabisa. Hakuna uhusiano. Na pia kama ulikuwepo enzi hizo mbona uone ajabu kwa hatua hizi? Hii ligi na upinzani wa jadi havijaanza leo. Kumbuka tulishafungiana mipaka kabisa na maisha yaliendelea tu vizuri.

Wacha huyo mpuuzi atumike kujenga mashirika ya ndege ya wenzie wa CoW kwanza nao washike mizizi vizuri kwenye hii block ndio atajua hajui.
 
Wakenya huwa wanakuja kununua sna mazao tz
Na Bidhaa zingine, tukipigana pini wote tutaumia

Ova
Yap,umesema kweli tunategemeana tena sana tu.sema hawa jamaa wanajiona wao ni europe africa bahati mbaya.

EAC wao ndo wanajiona wakubwa(super power)alafu nchi zingine ni wadogo.

Sasa wanalianzishaga alafu TZ inamaliza. Wakileta ugoko tunaweka nondo.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom