Waziri Stergomena Tax akutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
997
662
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax, tarehe 28 machi, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Hungary Bw. Peter Sziijarto na ujumbe wake katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar-es-Salaam.

Katika Mkutano huo, Waziri wa Ulinzi na JKT na mwenzake wa Mambo ya Nje wa Hungary walizungumzia ushirikiano katika masuala mbalimbali yanayohusu Amani na Usalama Kimataifa na Ushirikiano katika Sekta ya Ulinzi kati ya Tanzania na Hungary.

Waziri wa mambo ya Nchi za nje wa Hungary alimueleza Waziri Stergomena Tax utayari wa Hungary katika kushirikiana na Tanzania katika kuzikabili changamoto za kiulinzi na kiusalama kimataifa na ushirikiano katika sekta nyingine.

Waziri Stergomena Tax alimshukuru Waziri Peter Sziijarto kwa ushirikiano unaoendelea kuimarika kati ya nchi hizi mbili na kumhakikishia utayari wa Wizara ya Ulinzi na JKT kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Hungary.
20240330_035304.jpg
20240330_035308.jpg
20240330_035300.jpg
 
Style ya nywele ya Waziri wa Hungary ni ya kuweka mbali na watoto, duh!
 
Back
Top Bottom