Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika ununuzi wa korosho, Bodi ya Mazao Mchanganyiko inafanya kwanza thamini na kujiridhisha kama korosho hizo zimezalishwa nchini, kuangalia ubora na kama aliyepeleka ndiye mkulima. Baada ya kujiridhisha, ndipo utaratibu wa malipo unafuata.