Serikali Yaja na Mpango Mkakati wa Kumlinda Mkulima wa Korosho Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

SERIKALI YAJA NA MPANGO MKAKATI WA KUMLINDA MKULIMA WA KOROSHO NCHINI.

Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi imeendelea na jitihada za kuimarisha bei ya korosho nchini kwa kufufua viwanda vya kubangua korosho pamoja na kuanzisha viwanda vipya sambamba na kuanzisha kongani la viwanda (Industrial Park) vya kubangua korosho ili kuongeza thamani ya korosho na kuuza moja kwa moja katika nchi walaji badala ya kuuza korosho ghafi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Lulindi Mhe. Ally Issa Mchungahela alilouliza kuwa “Je, baada ya kuporomoka kwa bei ya korosho katika msimu wa 2022/2023 Serikali imechukua hatua gani kuhakikisha hali hii haijirudii” Mhe. Mchungahela

“Vilevile, Serikali itaanzisha kongani la viwanda (Industrial Park) vya kubangua korosho ili kuongeza thamani ya korosho na kuuza moja kwa moja katika nchi walaji badala ya kuuza korosho ghafi” Naibu Waziri Mavunde

Naibu Waziri Mavunde amesema mwenendo wa beiya korosho nchini hutegemea mwenendo wa bei katika soko la dunia hivyo mabadiliko hayo huchochewa na kiasi cha korosho kilichozalishwa duniani na mahitaji kwa wakati husika.

“Kwa wastani katika msimu wa 2022/2023 bei ilishuka kutoka Shilingi 2,150 hadi Shilingi 1,850 kwa kilo kwa korosho daraja la kwanza na Shilingi 1,595 hadi Shilingi 1,332 kwa korosho daraja la pili” Naibu Waziri Mavunde

Kufuatia majibu hayo ya Serikali yakamsimamisha Mbunge huyo kwa maswali mawili ya nyongeza kutokana na jimbo hilo kuwa wazalishaji wakubwa wa Malighafi ya hivyo viwanda vilivyoahidiwa na serikali kujengwa

“Je? Serikali itajenga viwanda vingapi Jimbo la Lulindi? Swali la Pili, Kilimo cha Korosho ni Zao pekee linalochangia Mfuko wa Kilimo Je? Serikali haioni Sababu ya kutumia kiasi cha fedha zilizoko katika Mfuko huu kwaajili ya Kutengenezea bima?” Mhe. Mchungahela

Aidha amekiri eneo hilo kuwa wazalishaji wakubwa wa zao la Korosho a kutambua hilo serikali na sekta binafsi zitaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda hivyo ili wakulima wanufaike sambamba na kukamilisha taratibu za bima ya Taifa kwa lengo la kumlinda Mkulima pale bei inapoporomoka.

“Ni kweli ni kati ya wazalishaji wakubwa a korosho kwa kutambua hilo Serikali pamoja na Sekta Binafsi tutaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kubangua Korosho katika eneo hili la Lulindi, ili wakulima wengi waweze kunufaika” Naibu Waziri Mavunde.

Tumeshafanya mazungumzo na shirika la Bima la Taifa kwaajili ya kuhakikisha wanaingia katika zao hili ili tuweze kumlinda Mkulima pale bei inapoporomoka na hivi sasa tupo katika hatua nzuri na baadhi ya maeneo tumeaanza majaribio naamini itawafikia wakulima wengi zaidi na itakuwa mkombozi mkubwa kwa mkulima wa Korosha hapa nchini” Naibu Waziri Mavunde.

xfcg.jpg
dxdghj.jpg
 
View attachment 2655962View attachment 2655964
dadaangu kachoma mkopo wa 30m yote kwenye korosho now anasema mwenyewe kama chizi
 
Back
Top Bottom