Mwananchi au mfanyabiashara atakayetaka kusafirisha korosho kwa barabara kuomba kibali kwa polisi na mkuu wa mkoa! Nini maoni yako?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
Mhe. Rais ameelekeza korosho yote ya Mtwara isafirishwe kwa njia ya meli kupitia bandari ya Mtwara; vinginevyo ukitaka kusafirisha kwa barabara lazima uombe kibali kwa mkuu wa mkoa na polisi ikieleza kwanini uruhusiwe kutumia barabara.

Kwanini amri hii imetolewa ? Kuna faida gani kutumia bandari na kuna hasara gani kutumia barabara? Je, kwa wananchi wa mikoani watatumia bandari? Nchi jirani je nao wakitaka korosho watatumia bandari? Naombeni elimu kuhusu hoja hizi na faida kwa mkulima endapo tutatumia bandari

Hivi karibuni Mhe. Bashe alisema muda wa kumdhibiti mkulima wapi auze mazao yake umeisha sasa hivi mkulima anayo haki ya kuchagua nani amuuzie........je kauli ya Mhe. Bashe kwenye korosho haitahusika?

Lakini pia naona kama jeshi la polisi siyo taasisi sahihi kudhibiti biashara NCHINI hasa pale ambapo hakuna sheria iliyolipuliwa; kwa mfano mfanyabiashara amekamatwa anasafirisha korosho kwa barabara jeshi la polisi litatumia sheria gani kumchukulia hatua?

Lakini pia kauli hii haijaweka wazi, ni wakati gani polisi wataanza kuhesabu kwamba umesafirisha korosho kwa barabara? Ukitoka Mtwara au hata ndani ya Mtwara? Vipi mikoa mingine ambayo bandari ya Mtwara siyo sehemu sahihi yakupakia?

Mwisho utatofautishaje korosho za Pwani na zile za Mtwara? Najaribu kupata concept ya matumizi ya bandari ya Mtwara vs mfumo wa ununuzi wa korosho sipati majibu sahihi.......naona hata zile korosho za kula sasa zitaondoka super market na wananchi wanaofanya biashara hiyo wataathirika sana...


Serikali itoe mwongozo kwenye hoja hii kabla ya wapinzani kuichukua na kuifanya agenda
 
Kutengeneza mazingira ya rushwa na kutesa wananchi hakukuanza leo na waasisi wake ni CCM.

Miaka sitini ya uhuru wa mateso.
 
Hiyo biashara inaonekana inafanya na wafanyabiashara waliokaribu na Rais, sasa kuzuia kusafirisha kwa barabara ni njia ya kuwazuia wafanyabiashara huru, na mkulima aendelee kunyonywa kwa bei ndogo na hao marafiki wa CCM.
 
Wapumbavu tu hao maana kuna korosho Singida,kuna korosho manyoni,kuna korosho kaliua kuna korosho Urambo,kuna korosho igagara na wanalima kwa nguvu zao na hakuna bahari waache uchuzi wao tutawatoa kamasi na si utani.nitasafirisha korosho zangu kwa barabara nitalipa ushuru wa kijiji ili watengeneze barabara polisi akija Kamata korosho zangu Tanzania na dunia watajua nitakachomfanya na si utani
 
Wapumbavu tu hao maana kuna korosho Singida,kuna korosho manyoni,kuna korosho kaliua kuna korosho Urambo,kuna korosho igagara na wanalima kwa nguvu zao na hakuna bahari waache uchizi wao tutawatoa kamasi na si utani.nitasafirisha korosho zangu kwa barabara nitalipa ushuru wa kijiji ili watengeneze barabara polisi akija Kamata korosho zangu Tanzania na dunia watajua nitakachomfanya na si utani
 
Korosho ya mtwara isafirishwe kwa meli

Sio korosho ya lindi, pwani, morogoro, kigoma, rwanda au malawi nk

Ni korosho ya mtwara! Au miMi sijaelewa ulicho andika mtoa mada
 
Mhe. Rais ameelekeza korosho yote ya Mtwara isafirishwe kwa njia ya meli kupitia bandari ya Mtwara; vinginevyo ukitaka kusafirisha kwa barabara lazima uombe kibali kwa mkuu wa mkoa na polisi ikieleza kwanini uruhusiwe kutumia barabara.
Nazani huwa kuna check points au vizuizi kwa ajili ya ukaguzi wa mazao ya misitu, madini nk

Hivyo mazao yanayo tokea mtwara yatafahamika kupitia ukaguzi utakao kuwa unafanyika
 
Na kuna sheria mfano mbao au mkaa kama sijakosea huwa marufuku kusafirisha usiku!

Ukiona jua limezama weka gari pembeni, kwa sababu kila kizuizi una unatakiwa kufanyiwa ukaguzi, kama mabasi ktk vituo vya ukaguzi wa taarifa za traffic ktk vituo vya mabasi
 
Back
Top Bottom