Waziri Mkuu: Wakulima wa korosho watalipwa baada ya kujiridhisha kama korosho hizo zimetoka nchini

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika ununuzi wa korosho, Bodi ya Mazao Mchanganyiko inafanya kwanza thamini na kujiridhisha kama korosho hizo zimezalishwa nchini, kuangalia ubora na kama aliyepeleka ndiye mkulima. Baada ya kujiridhisha, ndipo utaratibu wa malipo unafuata.
 
Hatushangai maani haya tuliyajua mapema na tukaonya kupitia hapa JF.

Wakulima wa korosho msibweteke na ahadi za majukwani bali subirini kwanza kuona utekelezaji - JamiiForums

Inawezekana kabisa hizi zikawa ni delaying tactics(danadana) wakati wanajaribu kutafuta fedha za kununulia hizo korosho.

Hata wafanyakazi waliahidiwa kuongezwa mishshara baada ya uhakiki ila mpaka leo imebaki hadithi tu.

Hawa wakulima wa korosho watageuka kuwa wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki-wazee wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa karne ya 21.

Hii ndio CCM mpya katika rangi zake halisi(true colours).

Only fools will relax and be comfortable in this country.
 
Kuna uzi nimeukuta humu humu JF Greatthinker anauliza Kwanini Utawala wa Marais Waislam ndio Utawala wao hupwaya!?

Pia kabla ya kulipa tuhakiki Kama hilo shamba alilipata kihalali Au Kwa Njia Za kifisadi

Pia tujiridhishe anathamini juhudi Za Serikal katika Suala la Hilo la Korosho Au laa?

Tuhakiki jee hakushiri Kwenye Vurugu Za Gesi 2014?
 
Wanaposema kupwaya wamakusudia nini hao mkuu?
 
tapatalk_1544182704954.jpeg
 
Kulikuwa na haja gani ya serikali kujiingiza katika jambo ambalo hailiwezi?? Huenda sasa ndio wametambua madhara ya jambo hili walipolichukulia kisiasa. Huwezi kuchubguza ubora wa kitu huku tayari unakihifadhi wewe! Ndio kusema serikali ikisema ubora ulikuwa wa chini basi bei nayo itaanguka? Je mkulima ataruhusiwa kuchukua korosho yake kama atakataa bei mpya?

Wakulima walipwe pesa zao na polisi walinde mipaka kuzuia korosho ya nje isiingizwe nchini. Kama habari hii ni ya kweli - madhila ya jambo hili yametokea mapema kuliko wengi walivotarajia.
 
Ndio korosho zote zitakapo chukuliwa BURE. Walishangilia mwanzo, sasa tusubiri washangilie kwenye kulipwa.

Ila hapo kwenye hio game kuna mawili,

1) Either, nusu ya wenye korosho wataambiwa hawana mashamba hivyo hawalipwi, au nusu wataambiwa wamezitoa nje ya nchi, labda INDIA au SOMALIA. Wataangukia kidevu

2) Au CCM wanasubiri mwakani 2019 ndio WAWALIPE WAKULIMA fedha zao, kifupi ndio njia "INDIRECT" pengine wanataka iwe ya kupiga kampeni za uchaguzi ili wapunguze STRESS ya kukaziwa na wagombea wa upinzani.

Mtazamo wangu,
Zitto
 
Kulikuwa na haja gani ya serikali kujiingiza katika jambo ambalo hailiwezi?? Huenda sasa ndio wametambua madhara ya jambo hili walipolichukulia kisiasa. Huwezi kuchubguza ubora wa kitu huku tayari unakihifadhi wewe! Ndio kusema serikali ikisema ubora ulikuwa wa chini basi bei nayo itaanguka? Je mkulima ataruhusiwa kuchukua korosho yake kama atakataa bei mpya?

Wakulima walipwe pesa zao na polisi walinde mipaka kuzuia korosho ya nje isiingizwe nchini. Kama habari hii ni ya kweli - madhila ya jambo hili yametokea mapema kuliko wengi walivotarajia.
Kifupi serikali haikujiandaa ilichukua maamuzi kwa pupa.

Wengine tukishauri tunaambiwa tunashirikiana na mabeberu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom