Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,940
- 20,401
Boris Johnson waziri mkuu wa Uingereza baada ya kukalia kuti kavu kwa masaa 24 yalopita hatimae leo mchana atatangaza kujiuzulu baada ya mawaziri 55 kujiuzulu nafasi zao na serikali kushindwa kujiendesha.
===
Serikali ya Waziri mkuu wa Uingereza amezama katika mzozo ambao athari zake hazijajulikana ambazo zimepelekea kujiuzulu kwa mawaziri na maafisa wengine wa ngazi ya juu waliodai kuwa wamekosa imani na uongozi wa nchi wa Johnson.
Msukosuko huo ulianza Jumanne wake, kufuatia kashfa ya unyanyasaji wa kingono inayomuhusisha Chris Pincher – mbunge wa Conservative ambaye yuko karibu na Johnson, akiwa Waziri wa uchumi , Rishi Sunak , na Waziri wa afya. Sajid Javid, viongozi wakuu katika serikali, walijiuzuru.
Sunak alidai kuwa raia wanaitarajia serikali iendeshwe kwa njia "inayofaa, uwezo na kwa umakini "; huku Javid akidai kuwa utawala wa Johnson "haufanyi kazi kwa maslahi ya taifa".
Tangu wakati ule, katika kipindi cha saa 24, zaidi ya maibu mawaziri 40 na maafisa wengine wa ngazi ya juu wamewasilisha barua zao za kujiuzuru.
Jumatano Michael Gove, mjumbe wa muda mrefu wa baraza la mawaziri, alimuomba Waziri mkuu ajiuzuru. Ombi hili baadaye liliungwa mkono naa maafisa kadhaa wa ngazi ya juu, akiwemo Waziri wa mambo ya ndani Priti Patel.
Mawaziri kadhaa muhimu wa nchi hiyo pia walihudhuria makao makuu ya serikali ya Uingereza katika ofisi ya Waziri mkuu 10 Downing Street, ambao waliidhinisha uungaji mkono wao wa kumtaka Jonson aendelee kuwa mamlakani. Hawa ni pamoja na Waziri wa utamaduni,Nadine Dorries, na Waziri wa fursa za Brexit Opportunities, Jacob Rees-Mogg.
Kwa upande wake, Boris Johnson anaonekana kupinga uwezekano wa kung’atuka madarakani na badala yake alimuondoa mamlakani Gove, mtu ambaye amekuwa muhimu katika chama cha Conservative Party kwa muongo uliopita.
''Boris Johnson wants tanataka kuendelea kupambamba .Anaamini ana watu wa kutosha wanaomzingira wanaoweza kumuwezesha kusonga mbele ,"Waziri Dorries salielezea kwa kifupi alipokuwa akiondoka katika makao makuu ya serikali Jumatano usiku.
Boris amekuwa ni kiongozi Uingereza ambaye amepokea barua za kujiuzuru nyingi zaidi tangu mwaka 1932, alikabiliwa na maswali ya wabunge Jumatano kuhusu utawala wake, ambako alieleza wazi utashi wake wa kuendelea kubakia mamlakani.
Miito inayomtaka ajiuzuru inakuja mwezi mmoja baada ya Waziri huyo mkuu kukabiliwa na hoja ya kutokuwa na imani naye ambapo 41% ya wabunge kutoka chama chake walipiga kura dhidi yake.
BBC Swahili