Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson kutangaza kujiuzulu mchana huu

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,876
20,286
Boris Johnson waziri mkuu wa Uingereza baada ya kukalia kuti kavu kwa masaa 24 yalopita hatimae leo mchana atatangaza kujiuzulu baada ya mawaziri 55 kujiuzulu nafasi zao na serikali kushindwa kujiendesha.
===
Serikali ya Waziri mkuu wa Uingereza amezama katika mzozo ambao athari zake hazijajulikana ambazo zimepelekea kujiuzulu kwa mawaziri na maafisa wengine wa ngazi ya juu waliodai kuwa wamekosa imani na uongozi wa nchi wa Johnson.

Msukosuko huo ulianza Jumanne wake, kufuatia kashfa ya unyanyasaji wa kingono inayomuhusisha Chris Pincher – mbunge wa Conservative ambaye yuko karibu na Johnson, akiwa Waziri wa uchumi , Rishi Sunak , na Waziri wa afya. Sajid Javid, viongozi wakuu katika serikali, walijiuzuru.

Sunak alidai kuwa raia wanaitarajia serikali iendeshwe kwa njia "inayofaa, uwezo na kwa umakini "; huku Javid akidai kuwa utawala wa Johnson "haufanyi kazi kwa maslahi ya taifa".

Tangu wakati ule, katika kipindi cha saa 24, zaidi ya maibu mawaziri 40 na maafisa wengine wa ngazi ya juu wamewasilisha barua zao za kujiuzuru.

Jumatano Michael Gove, mjumbe wa muda mrefu wa baraza la mawaziri, alimuomba Waziri mkuu ajiuzuru. Ombi hili baadaye liliungwa mkono naa maafisa kadhaa wa ngazi ya juu, akiwemo Waziri wa mambo ya ndani Priti Patel.

Mawaziri kadhaa muhimu wa nchi hiyo pia walihudhuria makao makuu ya serikali ya Uingereza katika ofisi ya Waziri mkuu 10 Downing Street, ambao waliidhinisha uungaji mkono wao wa kumtaka Jonson aendelee kuwa mamlakani. Hawa ni pamoja na Waziri wa utamaduni,Nadine Dorries, na Waziri wa fursa za Brexit Opportunities, Jacob Rees-Mogg.

Kwa upande wake, Boris Johnson anaonekana kupinga uwezekano wa kung’atuka madarakani na badala yake alimuondoa mamlakani Gove, mtu ambaye amekuwa muhimu katika chama cha Conservative Party kwa muongo uliopita.

''Boris Johnson wants tanataka kuendelea kupambamba .Anaamini ana watu wa kutosha wanaomzingira wanaoweza kumuwezesha kusonga mbele ,"Waziri Dorries salielezea kwa kifupi alipokuwa akiondoka katika makao makuu ya serikali Jumatano usiku.

Boris amekuwa ni kiongozi Uingereza ambaye amepokea barua za kujiuzuru nyingi zaidi tangu mwaka 1932, alikabiliwa na maswali ya wabunge Jumatano kuhusu utawala wake, ambako alieleza wazi utashi wake wa kuendelea kubakia mamlakani.

Miito inayomtaka ajiuzuru inakuja mwezi mmoja baada ya Waziri huyo mkuu kukabiliwa na hoja ya kutokuwa na imani naye ambapo 41% ya wabunge kutoka chama chake walipiga kura dhidi yake.

BBC Swahili
 
Kufuatia Ongezeko la gharama za Maisha nchini humo hususani Mafuta na Gas kitu kilichopelekea Bidhaa na Maisha Kwa ujumla Kupanda .

Kushindwa kwake kuongoza na kufanya maamuzi ya kiuongozi .

Hatimaye kufuatia Ongezeko la Mawaziri wake zaidi ya 50 kujiuzulu Toka juzi .

Jamaa kabwaga Manyanga !!!


Wale WAMAGHARIBI wa Yombo , Buza na Kwa mtogole !!


URUSI NI TAIFA KUBWA , KUJARIBU KULITENGA NA DUNIA HAIWEZEKANI, HAIWEZEKANI !!


Sasa kimbunga ndo kimeanza, Rais Macron kapoteza Bunge Kwa wapinzani , Ujeruman Kansela naye anaanza kupumulia mashine !!
 
Boris Johnson waziri mkuu wa Uingereza baada ya kukalia kuti kavu kwa masaa 24 yalopita hatimae leo mchana atatangaza kujiuzulu baada ya mawaziri 55 kujiuzulu nafasi zao na serikali kushindwa kujiendesha.
Ila Michael Gove yule jamaa ni Milchawi kabisa. Vipi jamaa yako Dominic Raab ndo next pm nini?.

Naona Cummings ni full shangwe karma is a bitch
 
Angalau huko watu wanaangalia maslahi ya nchi kwanza! Maamuzi ya kijamaa, juhudi za kibepari!

Hawa wanaotumia UTI wa mgongo kufikiri, wenye elimu za kukariri, wanaodhani UREFU WA KAMBA na kujirundikia mabilioni ndio kufungua nchi(hata kama naelewa sasa nchi imefungulia ili nini kiingie), tumejihakikishia kuwa MASIKINI kwa angalau miaka 100 ijayo!
 
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameamua kujiuzulu nafasi hiyo baada kupata shinikizo kubwa kutoka kwa mawaziri wake na wabunge wa chama chake

Bwana Johnson kutangaza uamuzi wake huo muda sio mrefu kutoka sasa

Chanzo: BBC
Mkuu, Bosi Johnson hajaamua kujiuzulu mwenyewe alikuwa akikataa kuhusu jambo hilo. Taarifa zasema asubuhi hii amepelekewa barua na mawaziri wengi na maofisa wengine waandamizi wa serikali na kuambiwa asaini na aisome mwenyewe baadae leo.

Hutuwezi kufahamu hao maofisa ni akina nani ila ni wale "top government officials".

Na hiyo pia ni baada ya kuambiwa na waziri mpya wa fedha bwana Zahawi asubuhi hii kwamba ni muda umefika.

Wakuu wa vyombo na idara mbalimbali nyeti nchini humo wamekuwa na wasiwasi kwamba huenda wanashughulika na mtu ambae atawapa shida hivyo imeamuliwa kutoka juu kabisa aondoke kwa usalama wa nchi.
 
Angalau huko watu wanaangalia maslahi ya nchi kwanza! Maamuzi ya kijamaa, juhudi za kibepari!

Hawa wanaotumia UTI wa mgongo kufikiri, wenye elimu za kukariri, wanaodhani UREFU WA KAMBA na kujirundikia mabilioni ndio kufungua nchi(hata kama naelewa sasa nchi imefungulia ili nini kiingie), tumejihakikishia kuwa MASIKINI kwa angalau miaka 100 ijayo!
Hapa kwetu ,tuna maviongozi manasiasa yanabwabwaja tu, akili kiduchuu .

Wee cheki Bungeni walivyo , wanapiga makofi kwenye mambo ya kijinga tu.

Na Hawa viti maalumu Ndo kabisaaa Vitunguu Maji .
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom