Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Boris Johnson ahamia kwenye Tasnia ya Utangazaji

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
335
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson amejiunga na kituo cha televisheni cha ‘GB News’ kilichopo jijini London, Uingereza.

BBC imeripoti kuwa Johnson, ambaye alijiuzulu ubunge mapema mwaka huu, atafanya kazi katika kituo hicho cha habari kama mtangazaji, mtayarishaji wa vipindi na mtoa maoni.

"Atakuwa na jukumu muhimu" katika matangazo ya uchaguzi wa Uingereza na Marekani mwaka ujao na ataangazia masuala tofauti "kuonyesha nguvu ya Uingereza duniani kote," shirika hilo la utangazaji lilisema.

Aliahidi kushiriki "maoni yake ambayo hayajabadilika" kuhusu mada tofauti.

Johnson ni mwanasiasa wa hivi karibuni kutoka Chama cha Conservative kujiunga na shirika hilo la utangazaji, baada ya aliyekuwa Katibu wa Biashara Jacob Rees-Mogg, Naibu mwenyekiti wa chama Lee Anderson, na wabunge Esther McVey na Philip Davies.

Katika video iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Uingereza amesema: "Ninafurahi kusema kwamba hivi karibuni nitajiunga nawe kwenye GB News.”

Hata hivyo Boris Johnson si mgeni katika taaluma ya habari kwani 1989, aliajiliwa kama mwandishi wa Brussels, baadaye akawa mwandishi wa safu ya kisiasa kwenye gazeti la ‘The Daily Telegraph,’ kabla ya kupanda daraja na kuwa Mhariri wa 'The Spectator' toka mwaka 1999 hadi 2005.
 
Good for him.

Wampangie majukumu Gaza nafikiri itapendeza zaidi
 
Wenzetu wana professional nje ya siasa sio kutegemea siasa na dili za serikali tu, tujifunze pia
Siyo professional inaitwa proffesion. Sijui hizi elimu zenu ni wapi jamani. Au ndo product za udom na SAUT. Maana product ya udsm haiwezi kuchapia hivi
 
Hapa ndo unaona jinsi watanzania tulio wa pumbavu 'theme' ya comment yangu haiko huku, hata kwenye computer hicho kipengere cha ku edit spelling kipo, hi nchi ina watu wspumbavu kweli kweli af wanajifanya wssomi......
 
Kubali makosa ili ujifunze zaidi. Usishupaze shingo. Siku nyingine usichekwe kwa kuandika proffesional badala ya proffesion
 
Mkuu sijakosea chochote ila sitaki tubishane kwa vitu vidongo hao watu hawana professinal japo wana profession.........ebu ni kufafanulie zaidi mkuu professional is a member of a profession or any person who works in a specified professional activity.
 
"Professional is the member of profession"

Chutama mkuu,umeshavuliwa nguo
 
Mkuu usiniĺazimisha kukubaliana na wew niko sahihi 100% japò unaona uzito kukiri, sasa tufanye kama utani ili tuendelee kubadilisha mawazo tu

Naomba unitafusilie hi sentesi unionyeshe kosa liko wapi? Kwa kuikosoa

"My professional is media technician though its not my profession"
 
Mkuu sijakosea chochote ila sitaki tubishane kwa vitu vidongo hao watu hawana professinal japo wana profession.........ebu ni kufafanulie zaidi mkuu professional is a member of a profession or any person who works in a specified professional activity.
Proffesional ni adjective na proffesion ni noun. Ulipaswa kuandika proffesion siyo proffesional. Mana ni moja ila structure tofauti
 
Wenzetu wana professional nje ya siasa sio kutegemea siasa na dili za serikali tu, tujifunze pia
Siyo Africa tunataka watoto, wajukuu na vitukuu virithi nafasi zetu tena kwa udi na uvumba
 
Back
Top Bottom