Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,327
- 24,209
Kwa kawaida nakerwa sana viongzi kuongelea mambo ya kitaalam bila kutafuta ushauri.
Hivi karibuni Mh. Waziri Mkuu alishangazwa kibanda cha Mlinzi katika mradi wa VETA huko Tabora kugharimu Ths 11 million.
Mimi sikushangzwa na gharama lakini nilishangazwa na kauli ya Waziri Mkuu Majaliwa kusema hadharani kuwa pale kuna upigaji!
Nikiwa mhandisi, niliamua kutafuta picha za kazi hiyo na kutenngeneza Rough Estimates za mradi huo kama ungekuwa Dar es Salaam kwa sasa hivi.
Gharama nilizo pata Kwa MKOANI DAER ES SALAAM ni Tsha 11,371,650.0
Kwa vile tabora ni mbali na supplier vifaa vingi , niliamua kuweka factor ya 1.2, hivyo GHARAMA ZA JENGO TABORA KUWA 13,645,980.
Naomba washauri wa Mh Waziri Mkuu wawe wanamtonya kama anakosea.
Gharama za kibanda ni sawa, tena ni pungufu kidogo.
KIBANDA CHA MLINZI VETA , TABORA | ||||||
S.No | ITEM | UNITS | QUANTITY | UNIT COST | COST | REMARKS |
1 | Kuset kibanda na ngazi zote | sum | 20,000 | |||
2 | Kuchimba misingi | m3 | 3.8 | 12,000 | 45,600 | |
3 | Kuweka zege la msingi, nyumba na ngazi | |||||
0.2m thick | m3 | 0.45 | 180,000 | 81,000 | ||
4 | Tofali za kulaza misingi | m2 | 21 | 37,000 | 777,000 | |
5 | Tofali ngazi za kupandia kibanda | m2 | 3.6 | 37,000 | 133,200 | |
6 | kuujaza udongo wa murram | m3 | 27.5 | 15,000 | 412,500 | |
na kushindilia | ||||||
7 | kuweka mawe ndani ya msingi na ngazi | m3 | 4.5 | 35,000 | 157,500 | |
8 | Kumwaga zege la jamvi 150mm | m3 | 4.5 | 180,000 | 810,000 | |
9 | Kuset kuta za nyumba, tofali za | m2 | 13.5 | 25,000 | 337,500 | |
kusimama 150mm mpaka | ||||||
beam soffit | ||||||
10 | Shuttering ya ring beam | m2 | 4.6 | 26,000 | 119,600 | |
11 | Kukunja na kuweka nondo | kg | 98 | 4,000 | 392,000 | |
12 | Kumwaga zege la beam | m3 | 1.25 | 180,000 | 225,000 | |
13 | Tofali za level mtambaa panya | m2 | 13.45 | 25,000 | 336,250 | |
na gable | ||||||
14 | Kufunga wall plate na truss, na | nos | 5 | 1,500 | 7,500 | |
15 | Kufunga fascia board nyumba nzima | m | 15 | 1,500 | 22,500 | |
16 | Kufunga purlins 50x50mm | m | 120 | 8,000 | 960,000 | |
17 | Kupiga bati za IT4 na kofia, kila bati 3.4m | nos | 38 | 65,000 | 2,470,000 | |
18 | Kupiga brandering ya ceiling | m2 | 25 | 4,000 | 100,000 | |
19 | Kufix gypsum board ya ceiling | m2 | 25 | 6,800 | 170,000 | |
20 | Kujaza uwazi kati ya bati na ukuta | sum | 45,000 | |||
21 | Fufunga bomba za kupitisha | sum | 50,000 | |||
Umeme na box za switches | ||||||
22 | Kufunga frame za madirisha | nos | 2 | 150,000 | 300,000 | |
23 | Kufunga frame za milango | nos | 3 | 150,000 | 450,000 | |
24 | Kupiga render za kuta nje na ndani | m2 | 148.5 | 2,000 | 297,000 | |
25 | Kupiga plaster nje na ndani | m2 | 148.5 | 2,000 | 297,000 | |
26 | Kufunga madirisha ya aluminium | nos | 2 | 240,000 | 480,000 | |
27 | Kufunga milango mbao ya mkongo | nos | 3 | 260,000 | 780,000 | |
28 | Electrical wiring na kufunga switch | sum | 650,000 | |||
29 | Kupiga rangi nje na ndani | m2 | 148.5 | 3,000 | 445,500 | |
TOTAL | 11,371,650 | |||||
NB | ||||||
1 | Gharama hizi ni za DAR ES SALAAM | |||||
2 | Kibanda hiki kiko TABORA, hivyo kwa kusafirisha vifa hivyo kwend TABORA, factor gharama kwa 1.2 , | |||||
3 | Hivyo Gharama ya jengo la VETA , TABORA =13,645,980.00 |
UPDATE:
Katika makadirio wadau wamenitonya yafautayo
1. Hapo pembeni kuna kichumba ambacho waafikiri ni choo, gharama za kuvuta maji, choo chenyewe na wall tiles inaweza kuongeza gharama kwa arond 1.0 million
2.Kuna floor tiles amnazo sijazigsa kabisa, gharama ambayo tiles kwa nyuma nzima na ngazi inaweza kufikia 1.2million
Hivyo kazi hii ya nyongeza ni Tshs 2,2 million n jumla kuu kwa kazi ya kibanda=Tshs 15,845,980.00
OMBI
Ofisi ya Waziri Mkuu wakimaliza uchunguzi wao wa kitaalam , watuwekee hadharani makadirio yao kwa viwango vya kazi husika ya kibanda cha VETA Tabora(kwa kulinganisha tu)