Kwa aina ya ubabe uliotumika kutoka kwa policcm na uvccm walio jipachika jukumu la utiss, hata ungekuwa ni wewe ungekuwa tu mpole! Na usingefanya lolote.
Mbaya zaidi walipozwa na posho nene ya laki tatu na ushee!! Jambo ambalo halikuwa la kawaida. Ukichukulia hiyo fedha haikutoka kwa Mabeberu!
. Ilikuwa ni fedha ya ndani kwa maelezo ya mwenye nchi na wapambe wake.
Hii ni taarifa niliyopewa na mtu wangu wa karibu aliyekuwa ni mmoja wa wasimamizi.
Pesa iliyotumika kuendesha uchaguzi ni pesa ambayo mabeberu waliitoa kwaajili ya kuwasaidia watanzania kupambana na corona. Yeye akaipeleka kwenye uchaguzi, na kuongea uwongo kuwa eti ni pesa yetu ya ndani. Ndiyo sababu, baada ya Bunge la Ulaya, kupata uhakika huo, waliomba taarifa ya pesa yao waliotoa kwaajili ya kupambana na corona, namna ilivyotumika. Mpaka leo Serikali imeshindwa kutoa taarifa ya matumizi.
Serikali yetu inaendesha mambo kwa hadaa.
Utakuwa mjinga hasa kuamini kuwa Serikali hii ina uwezo wa kuboresha mishahara ya wafanyakazi wa umma. Lakini ifahamike pia, imesababisha kupotea kwa ajira nyingi kwenye sejta binafsi, na hata kusababisha maslahi duni kwenye sekta binafsi. Matokeo ya kuua sekta binafsi yatamgusa kila mtu isipokuwa PolePole na wenzake wanaotembelea na maV8.
Maadamu bado kuna watanzania wengi ni wajinga, na ndio hasa wanaoiunga mkono CCM, ni vema kila mmoja akawa tayari kisaikolojia kuishi kwa namna hawa wevi wa kura watakavyopenda.
Suala la uchaguzi unaozingatia maamuzi ya wananchi lilitakiwa kuenziwa na kupiganiwa na kila mwananchi, bila ya kujali upo chama gani. Kama CCM, CJADEMA, ACT, au CUF, wanapata uongozi kwa njia ya hila, wakikengeuka, mimi mwananchi nitakuwa na nyenzo gani ya kumwadhibu?
Magufuli aliharibu uchaguzi kuanzia ndani ya CCM, akajichagulia anaowataka yeye, wanaCCM kimya. Hawa akina Katambi waliopata kura 3 halafu ni wabunge, watamsikiliza mwanaCCM au Magufuli?
Hawa akina Gwajima ambao wamepitishwa na Magufuli kuanzia kura za maoni mpaka kwenye uchaguzi mkuu kwa kura za kwenye mafuko myeusi, bungeni watawatetea wananchi au Magufuli?
Akina Halima, waliopewa ubunge na Ndugai, Ndugai aliyepewa ubunge na uspika na Magufuli, watawatetea nani?
Bunge sasa limejaa watu wa kumtetea na kumpamba Magufuli, wananchi hawana watetezi. Wananchi kika watakachotendewa, kama ni chema, ni kwa hisani ya Magufuli.
WANANCHI HAWANA WAWAKILISHI BUNGENI.