Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Cheo kikubwa namna hiyo unadanganya wananchi watu wa hivi tunao lakini ni hatari kwa taifa
 
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea naye kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salamu.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.

JPM akiwa mortuary, Waziri Mkuu alitoa hizo statements.
Tulio DSM tayari tulisha liona lile Gun Carriage la jeshi sehemu za Mwenge.
Mungu amsamehe Mahaliwa kwa kukosa busara ya jinsi ya ku handle situation.
Alipofariki Mwalimu kule St Thomas London, Waziri Mkee wakati huo Rashid Kawawa alienda kumwona akiwa bado ICU.
Aliporudi waandishi wa habari walimwuliza swali Mwalimu anaendeleaje.
Kawawa huku machozi yskimlengalenga alisema, nina jambo zito moyoni, na hakuendelea kuongea.
Watu walimwelewa.
 
kama unaakili vizuri hebu tueleze ni nchi gani kiongozi wao akiwa madarakani alishawahi kufariki dakika mbili wakatangaza? juwa yule ni kiongozi wa nchi siyo kiongozi wa kundi la wavuta bange anaongoza watu wa aina tofauti tofauti we huoni ilivyotangazwa chadema wakaanza kufanya sherehe? ila sasa hivi wanalia kuliko hata angekuwepo
Kwa hiyo kwako ni sahihi afe tarehe 20 uje useme alikufa tarehe 30? Ili nini sasa?
 
🤣
Makaburi yanaanza kufukuliwa!

Halafu anakwenda kudanganyia kwenye nyumba ya ibada bora angesemea sokoni

Kakobe ajitokeze amwambie huyu atubu
 
🤡🤡🤡👇
downloadfile-4.jpg
 
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea naye kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salamu.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.

Naidownload hii kabisa, akichukua tu fomu ya Urahisi kule mbele tunaye😀😀😀
 
Back
Top Bottom