Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Siamini kwamba kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme ameitoa yeye mwenyewe bila kuongozwa na washauri. Na kama ni washauri wake wamempa hizo taarifa potofu basi wanapaswa kuwajibishwa kwa kusababisha Waziri Mkuu kutoa kauli ya "uwongo" bila kujitambua.
Mtu yeyote mwenye akili na busara, kabla ya kutoa kauli kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme atataka kujiridhisha juu ya viwango vya kusambaza umeme vya nchi kama South Afrika, Botswana, Morocco, Egypt, ili usije ukatoa kauli ambayo watu wenye uelewa watakubeza.
South Africa hadi sasa kiwango cha kusambaza umeme nchini ni asilimia 91.2%. Misri na Morocco wao wanadai kiwango chao cha kusambaza umeme ni 100%. Mauritius wana kiwango cha 98%, Ghana wana 83%. Sasa labda Waziri Mkuu atueleze inakuwaje 80% ya Tanzania ni kubwa kuliko 91.2% ya Afrika Kusini, 83% ya Ghana, 98% ya Mauritius, au 100% ya Misri na Morocco?
Si mara ya kwanza kuona viongozi wetu wakitumia takwimu zisizo za kweli ili kuisifia Tanzania. Kuna wakati kiongozi mmoja alitamba kwamba SGR yetu itakuwa na treni ya kasi ya juu zaidi katika Afrika kwa spidi ya 150-170kmhr, wakati Morocco tayari wana treni zenye spidi zaidi ya hiyo.
Ni vema kuisifia nchi yetu, lakini acha tuisifie nchi yetu kutokana na takwimu za kweli badala ya propaganda za kisiasa.
Chanzo: PM: Tanzania ya kwanza Afrika kusambaza umeme