Waziri Mkuu Kassim Majaliwa "amekosea" kwamba Tanzania inaongoza Afrika kusambaza umeme kiwango cha 80% kwa sababu sio kweli

sijali kuhusu takwimu, najali hasa kilichofanyika uko mavijijini (REA) , umeme kama wote
processing mills zilizokua zinatumia Diesel sasa zinatumia umeme kupunguza gharama za uendeshaji,

unataka ufanyiwe nini hasa wewe mtanzania usiekua na shukrani ?
Shukrani inakujaje wakati ni wajibu wa serikali husika tena inaezeshwa kwa Kodi za wavujajasho walio wengi TZ...Tuache kufikiria Jambo Kama shukrani bali ni wajibu tena uliowekwa kisheria kupitia Katiba...I hate cheap political stunts
 
kama umenuna kunya boga, tulia unyolewe tena mwaka huu
 
Soma andiko lote Hilo
NImesoma Mkuu lakini hakuna ukweli kwa hili la 80%. Angalia wanasema "kusambaza umeme kote nchini hadi vijijini na kufikisha asilimia 80%". Hiyo 80% unaiweka wapi? Believe me, sio kwamba 80% ya vijiji vyote vya Tanzania vina umeme.

Angalia hii taarifa;

1597755613454.png
 
CCM mseme tu kuwa labda PM alinukuliwa vibaya au alimaanisha East Africa! Vinginevyo tuleteeni takwimu kama alivyojustfy mtoa post!
PM alikuwa sahihi kabisa sema uelewa wa watu ndiyo tatizo. Ni kwamba hakuna nchi yeyote Afrika inayoifikia Tanzania katika kasi ya ongezeko la usambazaji wa umeme kwa sasa yaani kutoka vijiji 3000 mwaka 2015 hadi vijiji 9000 mwaka 2020. Kwa lugha rahisi hakuna nchi yeyote iliyounganishia wanachi wake kwa ongezeko la vijiji 6000 kwa muda wa miaka mitano kutoka 2015 hadi 2020.
 
Nimeisikia hii habari ikitangazwa leo nikapatwa kigugumizi.
Yaani pale kijijini kwangu na tena waweza kusema ni nusu mji, ndugu yangu pamoja na kuwa na nyumba nzuri aliomba umeme yapata mwaka wa 3 sasa kila akienda anaaambiwa Tanesco Mkoa wanasubiria fungu na hata akitaka alipie nguzo kwani anahitajika 3 anaambiwa hawaruhusiwi katu malipo yake ni elfu 27 tu! Sasa hiyo inayosemwa vijiji asilia 80 ni wapi huko. Kweli viongozi acheni kutudanganya wakati tunaona.
 
Majaliwa ana uwoga wa kupokonywa uwaziri mkuu mwache tu ajitoe akili

Hizo piko anazopakaa kichwani zimemuweka ganzi ya akili
 
kumbe wanadai

nilidhani una uhakika

basi Majaliwa nae amedai

usimhukumu
Sawa tumekuelewa. Kwa hiyo Wamisri wakila majongoo ni sawa waziri wetu mkuu kula majongoo. Kama kudai ni hoja angedai Tanzania tumefikia 105% basi ili tuwazidi wengine waliodai ndio aseme tunaongoza. Una akili kweli wewe.
 
PM alikuwa sahihi kabisa sema uelewa wa watu ndiyo tatizo. Ni kwamba hakuna nchi yeyote Afrika inayoifikia Tanzania katika kasi ya ongezeko la usambazaji wa umeme kwa sasa yaani kutoka vijiji 3000 mwaka 2015 hadi vijiji 9000 mwaka 2020. Kwa lugha rahisi hakuna nchi yeyote iliyounganishia wanachi wake kwa ongezeko la vijiji 6000 kwa muda wa miaka mitano kutoka 2015 hadi 2020.
Na haya unayosema hapa ndiyo aliyosema PM? Hebu tuonyeshe ilipo hiyo 80% katika uliyosema.

Watu mna wendawazimu kweli. Yaani mko tayari kutunga maneno yenu ili kuukaribia ukweli kwa kuwa tu hamtaki kukiri kwamba PM kachemsha? HUo ndio uzalendo mnaoimba kila siku? Kweli kuna watu mmelishwa limbwata la kisiasa
 
....
Si mara ya kwanza kuona viongozi wetu wakitumia takwimu zisizo za kweli ili kuisifia Tanzania. Kuna wakati kiongozi mmoja alitamba kwamba SGR yetu itakuwa na treni ya kasi ya juu zaidi katika Afrika kwa spidi ya 150-170kmhr, wakati Morocco tayari wana treni zenye spidi zaidi ya hiyo.

.....
Chanzo: PM: Tanzania ya kwanza Afrika kusambaza umeme
Ulivyo kiazi, JPM alisema sub-saharan Afrika.
 
Ulivyo kiazi, JPM alisema sub-saharan Afrika.
Sasa wewe ndio unamfanya PM aonekane kiazi hata zaidi yako. Kwani South Africa sio Sub-Sahara? Seychelles? Mauritius?

Kwa uzuzu ulionao najua unadhani Sub-Sahara maana yake nchi masikini, kwa hiyo South Africa haimo.

Yaani kuna watu wajinga na hamuoni aibu kuonyesha ujinga wenu! Eti alimaanisha Sub-Sahara Africa, ni wazi hujui hata maana ya Sub-Sahara-Africa unaropoka tu.
 
Acha jazba soma ujumbe wangu ulihusu SGR na siyo umeme! Unajazba sana bwana mdogo
 
Acha jazba soma ujumbe wangu ulihusu SGR na siyo umeme! Unajazba sana bwana mdogo
Sie tuko kwenye thread ya umeme wewe unaleta SGR, sasa tutakuelewa vipi? Ndio maana nikakupa majibu ya utumbo nikijua unatoa point za utumbo. Kama ulikuwa umetoka nje ya mada na sikukuelewa hupaswi kunilaumu, japo bado nitakuomba msamaha kwa kukubwatukia! Ashukumu Mkuu.
 
Unaumwa wewe, masuala ya SGR si wewe umeyaandika dogo you need to grow
 
Unaumwa wewe, masuala ya SGR si wewe umeyaandika dogo you need to grow
Acha jazba soma ujumbe wangu ulihusu SGR na siyo umeme! Unajazba sana bwana mdogo
Aaah, kumbe ni ile kauli ya treni zetu za SGR kuwa na spidi kuliko treni zote Africa!

Haya, ngoja tuseme ni kuliko treni zote SubSahara Afrika.

Spidi ya juu ya treni zetu inatarajiwa kuwa 160km/hr. Treni ya South Africa, Gautrain inaenda mpaka 160km/hr.

Sasa bado tu huoni ni kujimwambafy pasipo sababu?

Lakini nakumbuka alisema Africa, sio Sub-Sahara Africa, wakati Morocco wana ngoma inaenda 320km/hr inawaacha hata Germany na train zao za ICE zinazoenda 300km/hr!
 
Siamini kwamba kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme ameitoa yeye mwenyewe bila kuongozwa na washauri. Na kama ni washauri wake wamempa hizo taarifa potofu basi wanapaswa kuwajibishwa kwa kusababisha Waziri Mkuu kutoa kauli ya "uwongo" bila kujitambua.

Mtu yeyote mwenye akili na busara, kabla ya kutoa kauli kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme atataka kujiridhisha juu ya viwango vya kusambaza umeme vya nchi kama South Afrika, Botswana, Morocco, Egypt, ili usije ukatoa kauli ambayo watu wenye uelewa watakubeza.

South Africa hadi sasa kiwango cha kusambaza umeme nchini ni asilimia 91.2%. Misri na Morocco wao wanadai kiwango chao cha kusambaza umeme ni 100%. Mauritius wana kiwango cha 98%, Ghana wana 83%. Sasa labda Waziri Mkuu atueleze inakuwaje 80% ya Tanzania ni kubwa kuliko 91.2% ya Afrika Kusini, 83% ya Ghana, 98% ya Mauritius, au 100% ya Misri na Morocco?

Si mara ya kwanza kuona viongozi wetu wakitumia takwimu zisizo za kweli ili kuisifia Tanzania. Kuna wakati kiongozi mmoja alitamba kwamba SGR yetu itakuwa na treni ya kasi ya juu zaidi katika Afrika kwa spidi ya 150-170kmhr, wakati Morocco tayari wana treni zenye spidi zaidi ya hiyo.

Ni vema kuisifia nchi yetu, lakini acha tuisifie nchi yetu kutokana na takwimu za kweli badala ya propaganda za kisiasa.

Chanzo: PM: Tanzania ya kwanza Afrika kusambaza umeme
Takwimu za serikali hii sio za kuaminika kabisa.
 
Back
Top Bottom