Waziri Mkuu Kassim Majaliwa "amekosea" kwamba Tanzania inaongoza Afrika kusambaza umeme kiwango cha 80% kwa sababu sio kweli

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,563
Siamini kwamba kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme ameitoa yeye mwenyewe bila kuongozwa na washauri. Na kama ni washauri wake wamempa hizo taarifa potofu basi wanapaswa kuwajibishwa kwa kusababisha Waziri Mkuu kutoa kauli ya "uwongo" bila kujitambua.

Mtu yeyote mwenye akili na busara, kabla ya kutoa kauli kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme atataka kujiridhisha juu ya viwango vya kusambaza umeme vya nchi kama South Afrika, Botswana, Morocco, Egypt, ili usije ukatoa kauli ambayo watu wenye uelewa watakubeza.

South Africa hadi sasa kiwango cha kusambaza umeme nchini ni asilimia 91.2%. Misri na Morocco wao wanadai kiwango chao cha kusambaza umeme ni 100%. Mauritius wana kiwango cha 98%, Ghana wana 83%. Sasa labda Waziri Mkuu atueleze inakuwaje 80% ya Tanzania ni kubwa kuliko 91.2% ya Afrika Kusini, 83% ya Ghana, 98% ya Mauritius, au 100% ya Misri na Morocco?

Si mara ya kwanza kuona viongozi wetu wakitumia takwimu zisizo za kweli ili kuisifia Tanzania. Kuna wakati kiongozi mmoja alitamba kwamba SGR yetu itakuwa na treni ya kasi ya juu zaidi katika Afrika kwa spidi ya 150-170kmhr, wakati Morocco tayari wana treni zenye spidi zaidi ya hiyo.

Ni vema kuisifia nchi yetu, lakini acha tuisifie nchi yetu kutokana na takwimu za kweli badala ya propaganda za kisiasa.

Chanzo: PM: Tanzania ya kwanza Afrika kusambaza umeme
 
Tuambie tu unaona aibu (kama unayo) kwamba viongozi wenu CCM wana silka ya kusema uongo kila wakati. Ukibishana na hili la Majariwa basi wewe mwendawazimu, facts ziko wazi. Waziri Mkuu anapaswa kukiri hadhari kwamba "amenukuliwa vibaya"

sijali kuhusu takwimu, najali hasa kilichofanyika uko mavijijini (REA) , umeme kama wote
processing mills zilizokua zinatumia Diesel sasa zinatumia umeme kupunguza gharama za uendeshaji,

unataka ufanyiwe nini hasa wewe mtanzania usiekua na shukrani ?
 
Rudi hapo kwenye mada na utuambie alisema inaongoza kwa usambazaji afrika kwa vigezo na wakati gani?

Je ni kwa mwaka, kwa miaka mitano au kwa kipindi cha awamu ya tano?

Je anazungumzia mradi wa kusambaza umeme vijinini? Au anazungumzia usambazaji kwa ujumla wake?

Hao South Africa na 90+ % yao je ni kwa muhula upi? Ni kwa eneo gani nk.

Wasalaam
 
Acha uvivu, soma link. Wewe unaona kabisa source ambayo ina habari ya leo halafu unakuja na maswali asiyo na kichwa hapa. Soma hizo links ujiridhishe. Au hujui maana ya source unafikiri ni souce ya chips mayai?
 
sijali kuhusu takwimu, najali hasa kilichofanyika uko mavijijini (REA) , umeme kama wote
processing mills zilizokua zinatumia Diesel sasa zinatumia umeme kupunguza gharama za uendeshaji,

unataka ufanyiwe nini hasa wewe mtanzania usiekua na shukrani ?
Kwa hiyo kuwa na shukurani kwa REA ni pale ambapo uongo ukisemwa juu yao kila mtu ashangilie?

Wewe ni aina ya mtu ambae mkeo akiwa na kipato kukuzidi akakununulia gari, basi mtu akikuambia mkeo anakutawala na kukunyanyasa unakasirika kwamba unata watu wakufanye kuwa hna shukurani kwa mkeo kwa kukununulia gari. Sasa nitaongea nini na mtu kama wewe? Hako katabia katakuja kukufanya ukubali kufanyiwa kitu mbaya kwa sababu tu unataka kuonyesha shukurani.
 
Siamini kwamba kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme ameitoa yeye mwenyewe bila kuongozwa na washauri. Na kama ni washauri wake wamempa hizo taarifa potofu basi wanapaswa kuwajibishwa kwa kusababisha Waziri Mkuu kutoa kauli ya "uwongo" bila kujitambua.

Mtu yeyote mwenye akili na busara, kabla ya kutoa kauli kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme atataka kujiridhisha juu ya viwango vya kusambaza umeme vya nchi kama South Afrika, Botswana, Morocco, Egypt, ili usije ukatoa kauli ambayo watu wenye uelewa watakubeza.

South Africa hadi sasa kiwango cha kusambaza umeme nchini ni asilimia 91.2%. Misri na Morocco wao wanadai kiwango chao cha kusambaza umeme ni 100%. Mauritius wana kiwango cha 98%, Ghana wana 83%. Sasa labda Waziri Mkuu atueleze inakuwaje 80% ya Tanzania ni kubwa kuliko 91.2% ya Afrika Kusini, 83% ya Ghana, 98% ya Mauritius, au 100% ya Misri na Morocco?

Si mara ya kwanza kuona viongozi wetu wakitumia takwimu zisizo za kweli ili kuisifia Tanzania. Kuna wakati kiongozi mmoja alitamba kwamba SGR yetu itakuwa na treni ya kasi ya juu zaidi katika Afrika kwa spidi ya 150-170kmhr, wakati Morocco tayari wana treni zenye spidi zaidi ya hiyo.

Ni vema kuisifia nchi yetu, lakini acha tuisifie nchi yetu kutokana na takwimu za kweli badala ya propaganda za kisiasa.

Chanzo: PM: Tanzania ya kwanza Afrika kusambaza umeme
Propaganda tu hizo
 
Acha uvivu, soma link. Wewe unaona kabisa source ambayo ina habari ya leo halafu unakuja na maswali asiyo na kichwa hapa. Soma hizo links ujiridhishe. Au hujui maana ya source unafikiri ni souce ya chips mayai?
Ahhahhah,eti source ya chips mayai
 
Katika Swala la umeme mimi sitajali izo takwimu ila tu natoa kongole kubwa sana kwa awamu hii haswa kasi ya usambazaji umeme wa REA hatukatai REA imekuwepo tangu enzi za kikwete ila kwa sasa iko speed sana tembeeni vijijini muone ata ile asilimia tatu wanayonikata REA kila nikinunua umeme bado naona ni ndogo, Kongole kwa Jp magufuli, PM majaliwa na Minister Kalemani
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom