Waziri Mkuu Kassim Majaliwa "amekosea" kwamba Tanzania inaongoza Afrika kusambaza umeme kiwango cha 80% kwa sababu sio kweli

Mtoa mada ili kuondoa ubishi tusemi hivi:
'TANZANIA INAONGOZA KATIKA NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI NA KATI'!!
Maana huwa mara nyingi tunajishindanisha na nchi ambazo ni majirani zetu.
 
sijali kuhusu takwimu, najali hasa kilichofanyika uko mavijijini (REA) , umeme kama wote
processing mills zilizokua zinatumia Diesel sasa zinatumia umeme kupunguza gharama za uendeshaji,

unataka ufanyiwe nini hasa wewe mtanzania usiekua na shukrani ?
Anataka ndoa za jinsia moja tu hakuna kingine anachotaka
 
CCM mseme tu kuwa labda PM alinukuliwa vibaya au alimaanisha East Africa! Vinginevyo tuleteeni takwimu kama alivyojustfy mtoa post!
 
sijali kuhusu takwimu, najali hasa kilichofanyika uko mavijijini (REA) , umeme kama wote
processing mills zilizokua zinatumia Diesel sasa zinatumia umeme kupunguza gharama za uendeshaji,

unataka ufanyiwe nini hasa wewe mtanzania usiekua na shukrani ?
Hujali takwimu? Utajuaje kama unasonga mbele au unarudi nyuma? Hujui kuwa Waziri Mkuu alichozungumzia ni takwimu? Unaishi dunia ya wapi wewe usiyetilia umuhimu wa takwimu? Shukrani tunayo sana tu lakini leta takwimu za ukweli.
 
Hii nchi iko wapi mlamu!
Ni kisiwa karibu km 650 kuingia baharini kutoka Senegal na Mauritania Afrika Magharibi

1597745632530.png
 
Kweli umeme umesambazwa lakini walikuwa na uwezo wa kufunga umemem huo wa REA ni asilimia ikizidi sana 30 au 40, huo ni ulimbukeni, Nenda Mahenge, kijiji cha Kuanzia pale Ruaha, Isyaga , sali nenda handeni kuelekea kilindi songe umeme umepita watu hawana uwezo wa kuweka
 
sijali kuhusu takwimu, najali hasa kilichofanyika uko mavijijini (REA) , umeme kama wote
processing mills zilizokua zinatumia Diesel sasa zinatumia umeme kupunguza gharama za uendeshaji,

unataka ufanyiwe nini hasa wewe mtanzania usiekua na shukrani ?
Hivi REA ilianza lini?
 
Mtoa mada ili kuondoa ubishi tusemi hivi:
'TANZANIA INAONGOZA KATIKA NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI NA KATI'!!
Maana huwa mara nyingi tunajishindanisha na nchi ambazo ni majirani zetu.
Hapo wala hakuna ubishi Mkuu. Ndio maana tunapendekeza aseme alinukuliwa vibaya
 
"Usambazaji Umeme vijijini"
Hiyo ya "usambazaji umeme vijinini" sio ya Waziri Mkuu. Na hata hivyo, ukitenganisha kati ya urban electrfication na rural electrification kwa Tanzania basi utakuta rural electrification iko chini sana ya kiwango cha 80%. Inayotunyanyua Tanzania hadi kufika 80% ni urban electrification

1597749842420.png
 
View attachment 1541074
hasidi hana sababu, hamna shukrani nyie watu, endeleeni kuponda
 
Siamini kwamba kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme ameitoa yeye mwenyewe bila kuongozwa na washauri. Na kama ni washauri wake wamempa hizo taarifa potofu basi wanapaswa kuwajibishwa kwa kusababisha Waziri Mkuu kutoa kauli ya "uwongo" bila kujitambua.

Mtu yeyote mwenye akili na busara, kabla ya kutoa kauli kwamba Tanzania inaongoza Afrika kwa kusambaza umeme atataka kujiridhisha juu ya viwango vya kusambaza umeme vya nchi kama South Afrika, Botswana, Morocco, Egypt, ili usije ukatoa kauli ambayo watu wenye uelewa watakubeza.

South Africa hadi sasa kiwango cha kusambaza umeme nchini ni asilimia 91.2%. Misri na Morocco wao wanadai kiwango chao cha kusambaza umeme ni 100%. Mauritius wana kiwango cha 98%, Ghana wana 83%. Sasa labda Waziri Mkuu atueleze inakuwaje 80% ya Tanzania ni kubwa kuliko 91.2% ya Afrika Kusini, 83% ya Ghana, 98% ya Mauritius, au 100% ya Misri na Morocco?

Si mara ya kwanza kuona viongozi wetu wakitumia takwimu zisizo za kweli ili kuisifia Tanzania. Kuna wakati kiongozi mmoja alitamba kwamba SGR yetu itakuwa na treni ya kasi ya juu zaidi katika Afrika kwa spidi ya 150-170kmhr, wakati Morocco tayari wana treni zenye spidi zaidi ya hiyo.

Ni vema kuisifia nchi yetu, lakini acha tuisifie nchi yetu kutokana na takwimu za kweli badala ya propaganda za kisiasa.

Chanzo: PM: Tanzania ya kwanza Afrika kusambaza umeme
Sijui kama mataga wamekuelewa
 
Serikali ya wanyonge inajua wanyonge wake hawaelewi kitu hasa kwenye takwimu hivyo inajificha kwenye percentage, kwa kua wafuasi wake ni mataahira wao kila kitu ni kushangilia tu.

Utasikia pesa zetu za ndani halafu wanachukua mikopo kimia kimia, utasikia makusanyo yameongezeka halafu mikopo inazidi kupanda kila siku.

Hii ni serikali ambayo imejikita kwenye uongo na uzushi. Kukabiliana na hilo inatunga sheria kila siku kuwafungwa watakaohoji takwimu zao za uongo.
 
Suala la umeme vijijini nawapongeza serekali coz umeme umefika hata maeneo ambayo sikutegemea kama umeme utakuja kufika. Tukimaliza la umeme tuhamie kwenye maji Sasa.
 
Usiamini Takwimu zao maana nyingi za kupika na hawaitaji taasisi huru zifanye uchunguzi.
 
Back
Top Bottom