Waziri Mkuu azindua Kampeni ya Siku 16 za Uanaharakati Kupinga Ukatili wa Kijinsia. Aagiza Shule za Msingi mpaka Vyuo kuwa na madawati ya jinsia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,146
2,000
Habari Wadau,

Karibuni katika uzinduzi wa Siku 16 za Uanaharakati Kupinga Ukatili wa Kijinsia unaofanyika leo tarehe 25 Novemba, 2021 katika ukumbi wa Mlimani City.

Kauli mbiu ya kampeni hii mwaka huu ni Ewe mwananchi komesha ukatili wa KIjinsia sasa

1637914684563.png

Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, akiambatana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.

Siku 16 za Uanaharakati Kupinga Ukatili wa Kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayolenga kuongeza uelewa kuhusu athari za ukatili, hasa kwa wanawake.

Kampeni huanza tarehe 25 Novemba, Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, na kuhitimishwa tarehe 10 Desemba, Siku ya Haki za Binadamu. Tarehe hizi zilichaguliwa ili kuhusisha kiishara unyanyasaji dhidi ya wanawake na masuala ya haki za binadamu. Hasa, kampeni hii inasisitiza ukweli kwamba vurugu, kwa namna yoyote, ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ni lengo kuu la kazi ya utetezi ya WiLDAF, uundaji wa sera na mabadiliko ya kijamii katika jamii.

1637821226824.png

Picha: Wadau Mbalimbali waliohudhuria tukio hili

FFBJLoCWQAMm2C5

Picha: Band ikitoa burudani ukumbini


UPDATES
- Watu mbalimbali wamewasili katika tukio hili tayari kwa ajili ya tukio zima la siku ya leo.

- Wasanii wanatoa burudani kwa watu waliohudhuria ukumbini.

- Halima Mwaisungu kutoka Bugando Medical Centre anawasilisha utafiti wake kuhusu 'Uwezeshwaji kielimu na uongozi kwa wasichana walio nje ya mfumo wa shule kutokana na mimba.' Utafiti huu ulifanyika kwa kuzingatia mkoa wa Mwanza.

FFBPvg-XIAYafaW

Picha: Dkt. Halima Mwaisungu akiwasilisha Utafiti wake

Dkt. Halima Mwaisungu: Dhumuni la utafiti huu ni kuangalia ni jinsi gani tunaweza kusaidia mabinti na kuwawezesha kielimu na kiuongozi katika nyanja mbalimbali. Huyu kijana ni taifa la kesho tukimuondoa huyu kijana kwasababu amepata ujauzito sio sawa.

- Wadau mbalimbali wanauliza maswali na kutoa michango yao ya hoja kutokana na utafiti uliowasilishwa na Halima Mwaisunga.

Halima Mwaisungu: Wazazi/Walezi wawe na mpango maalum wa kuwawezesha watoto wa kike na kiume kujitambua tangu wakiwa na umri mdogo. Itawasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa wakati sahihi. Wazazi tuwe mfano wa kuigwa na watoto wetu.

KUWASILI KWA MGENI RASMI
Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa amewasili Mlimani City kuzindua rasmi kampeni ya siku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia.

UKARIBISHO
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Amos Makalla anafanya ukaribisho kwa kuongea kwa dakika chache

Mh.Makalla: Nitumie fursa hii kutoa taarifa kwamba nilifanya mikutano ya kusikiliza kero za wananchi katika maeneo mbalimbali Dar es Salaam. Katika kero 927 tulizosikiliza 30% zinahusiana na Ukatili wa Kijinsia.

Kwenye kero nilizozikuta wapo wanaume wanaonyanyaswa. Kuna wanawake wana fedha wanahitaji tu wanaume wa kuwaoa, hivyo anaweza kumpa kitu mwanaume na kumnyang’anya punde wakiachana

Sasa swali linakuja hii sio ukatili? Naona kuna mjadala mpana katika hili suala la unyanyasaji wa kijinsia ndio mana mjadala mzuri wenye lengo la kuboresha sheria za ndoa,


UTAMBULISHO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anafanya Utambulisho wa waliohudhuria katika shughuli ya leo wakiwamo viongozi wa kitaifa, Asasi za kiraia, Mabalozi wa nchi mbalimbali.

SALAMU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI

ANNA MEELA KULAYA - WILDAF TANZANIA

Salaam kutoka kwa Mratibu wa Siku 16 Kitaifa WiLDAFTz

Anna Kulaya: Mhe Mgeni Rasmi, Kauli Mbiu ya Kampeni mwaka huu ni “Ewe Mwananchi: Komesha Ukatili wa Kijinsia Sasa! Kauli mbiu hii tumeitohoa kutoka kauli mbiu ya Kimataifa inayosema Komesha ukatili Dhidi ya Wanawake Sasa.

FFBgRdZWQAU23b1

Picha: Mratibu wa WILDAFTZ Anna Meela Kulaya

Anna Kulaya: Kwetu Tanzania, sisi wana MKUKI na asasi zisizo za kiserikali na wadau wa maendeleo tumeamua kuangazia maeneo makuu 4:
1. Ukatili majumbani,
2. Ukatili dhidi ya wenza au wapenzi,
3. Ukatili wa mitandaoni hasa kwa wanawake
4. Rushwa ya ngono katika taasisi za elimu ya juu

Anna Kulaya: Matukio ya ukatili kwa watoto yaliyoripotiwa na Jeshi la Polisi Jan'21 - Sept'21 yanaonesha Watoto 6168 kati yao wasichana 5287 na wavulana 88 wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Kati yao watoto 3524 walibakwa, 637 walilawitiwa, 1887 walipata mimba, 130 walichomwa moto. Wakati umefika sasa, wa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake katika kukomesha vitendo vya ukatili.

Anna Kulaya: Wananchi wakichukua hatua na kukataa kuvumilia vitendo vya ukatili wa kijinsia, na kwa upande wa serikali, kuendelea kuimarisha sera, sheria, mifumo na miundo mbinu itasaidia kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Anna Kulaya: Mtandao wa [Mashirika] Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) tunaiomba Serikali:
1. Kutunga sheria ya kudhibiti Ukatili wa Kijinsia (Gender Based Violence Violence Act). Kwani ukosefu wa sheria mahususi ya makosa ya ukatili ni changamoto kubwa katika katika upatikanaji wa haki kwa watendewa na kuwatia hatiani watuhumiwa.

2. Kuharakishwa kwa mabadiliko ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ili kuokoa mabinti zetu dhidi ya ndoa za utotoni.

3. Kuboresha muundo na kutengwa bajeti ya kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto MTAKUWWA.

4. Kufuta sheria zote za kibaguzi mathalani Sheria ya Kimila ya Mirathi, Tangazo la Serikali Namba 436 la Mwaka 1963 ambayo inanyima wanawake haki yao ya Kikatiba ya kumiliki mali kupitia urithi.

ADDOU HODAN - SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA KITENGO CHA WANAWAKE
Addou Hodan:
Sote tuna jukumu la kuhakikisha tunafikia lengo la kila mwanamke, kila msichana na kila mtoto kuishi katika jamii isiyo na ukatili wa kijinsia.

FFBjEjXXsAI7kXm

Picha: Addou Hodan

Addou Hodan: Kupitia Siku 16 natumaini wote tutapaza sauti kukomesha Ukatili ili kuleta mabadiliko ya kudumu katika jamii zetu ambapo wanawake, wasichana na wavulana watafikia ndoto zao. Tukomeshe ukatili sasa.

UBALOZI WA MAREKANI
Ukatili wa kijinsia, bila kujali unatokea kwa njia gani, hupelekea matokeo mabaya kielimu, kiuchumi, nk. Lazima tufanye kila jitihada kutokomeza aina zote za ukatili.

MARRY O'NEILL - BALOZI WA IRELAND
Balozi Mary O’Neill:
Kwa sababu mbalimbali kesi nyingi za ukatili haziripotiwi. Ukatili wa Kijinsia unawanyima wanawake wengi fursa na kuwazuia kufikia ndoto na matarajio yao.

JANE MATINDE - Shirika la Huduma za Sheria - LSF

Katika Siku 16 tutaendelea kuwezesha upatikanaji wa haki tukiweka kipaumbele kwa wanawake na watoto. Tutashirikiana na serikali kuhakikisha malengo yanatimia. Tunaamini Siku 16 za uanaharakati zitakua hatua muhimu katika safari yetu ya kuelekea kukomesha aina zote za ukatili wa kijinsia nchini.

HOTUBA YA MGENI RASMI, WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
Kassim Majaliwa;
Nawashukuru kwa dhati kwa kunialika katika shughuli hii lakini pia Niwashukuru WILDAF na MKUKI kwa ushirikiano wenu kutoa elimu lakini sasa tunaanza kampeni maalumu ya kitaifa itakayozunguka kila mkoa.

FFB0GwyWQAcRF8e.jpg

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa

Kauli mbiu hii inaunga mkono juhudi za kimataifa kupinga ukatili wa kijinsia ambao umekuwa ukiwagusa zaidi, wanawake, watoto, wazee na watu wenye ulemavu.

Viongozi wa kitaifa wana matumaini makubwa kwamba kampeni hii ya Siku 16 itahamasisha jamii kupaza sauti ili kukemea mianya ya ukatili na kufichua vitendo vyote vya ukatili nnchini

MKUKI mmefanya jambo kubwa sana katika jamii yetu kwa ubunifu wa kampeni hii ya Siku 16. Ukatili unajitokeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika maeneo ya biashara, masoko, vyuoni n.k. Kila mmoja ana wajibu wa kupambana na ukatili.

Tunatamani kuona watu wote nchini bila kujali hali zao wanaishi kwa usawa. Licha ya sheria kali zilizopo bado vitendo vya ukatili vinajitokeza, hivyo ushiriki wa pamoja unahitajika ili kutokomeza vitendo vya ukatili

Licha ya sheria kuwepo, vitendo hivi bado vinaendelea kutokea. Nguvu ya pamoja inahitajika kukomesha vitendo hivi katika maeneo mbalimbali. Tunahitaji vitu hivi visitokee katika jamii zetu.

Wizara ya afya ikae na wadau na kufanya mapitio ya sheria ili tuziimarishe zaidi. Lengo letu ni kuona watanzania wanaendelea kuishi kwa matumaini makubwa.

Rushwa ya ngono imekua ni changamoto inayoshamiri katika vyuo vikuu na maeneo ya kazi. Kuna haja ya kubuni mipango thabiti kukabiliana na ukatili huu wa kijinsia. Tuna kazi ya kuhamasisha jamii kubadilisha fikra zao.

Serikali imeandaa mtaala wa mafunzo wenye kuzingatia masuala ya kijinsia kwa wasaidizi wa kisheria nchini wenye lengo la kuharakisha upatikanaji wa haki kwa wanawake na watoto hususani wahanga wa vitendo vya ukatili

Changamoto kukabiliana na vitendo vya ukatili ni pamoja na: mila na desturi potofu na ushiriki hafifu wa wananchi. Tushirikiane ili kuhakikisha taratibu zetu zinalenga haki, utu, hadhi na heshima ya mwananchi popote alipo.

MAAGIZO YA WAZIRI MKUU
Natoa agizo shule zote za msingi na sekondari zianzishe madawati ya jinsia.

Natoa agizo vyuo vya elimu nchini vianzishe madawati ya jinsia na yatangazwe wazi ili wanachuo wote wajue uwepo ma madawati hayo.

Natoa agizo jeshi la polisi liimarishe utendaji kazi katika madawati ya jinsia

Natoa agizo mamlaka za serikali za mitaa ziimarishe utaratibu wa upatikanaji wa taarifa za uvunjifu wa sheria hasa kwenye maeneo ya ukatili wa kijiWizara

Wizara ya afya iendelee kuimarisha uhusiano na sekta binafsi. Tupokee maoni, tusikie changamoto za sekta binafsi na serikali iwahakikishie ushirikiano.
 

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,445
2,000
Hii ni Kampeni ya Kimataifa ya kila mwaka inayoanza Novemba 25 ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na kuhitimishwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, Desemba 10

Inalenga kuhamasisha Raia na Mashirika duniani kote kupaza sauti kuhusu kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana

=====

The 16 Days of Activism against Gender-Based Violence is an annual international campaign that kicks off on 25 November, the International Day for the Elimination of Violence against Women, and runs until 10 December, Human Rights Day. It was started by activists at the inaugural Women’s Global Leadership Institute in 1991 and continues to be coordinated each year by the Center for Women’s Global Leadership. It is used as an organizing strategy by individuals and organizations around the world to call for the prevention and elimination of violence against women and girls.

In support of this civil society initiative, the United Nations Secretary-General’s UNiTE by 2030 to End Violence against Women campaign (UNiTE campaign) calls for global actions to increase awareness, galvanize advocacy efforts, and share knowledge and innovations.

The global theme for this year’s 16 Days of Activism against Gender-Based Violence, which will run from 25 November to 10 December 2021, is “Orange the world: End violence against women now!”
 

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,097
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salama, Amos Makalla amesema pamoja na kupokea kero za wanawake wanaokutana na unyanyasaji wa kijinsia wapo wanaume wanaohitaji msaada kutokana na changamoto za aina hiyo.

Akizungumza Alhamisi Novemba 25, 2021 wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Makala amesema sasa hivi wanaume wamekuwa na malalamiko dhidi ya wanawake wenye fedha.

“Nilikuwa na ziara ya kusikiliza kero za wananchi, asilimia 30 ya kero 927 nilizopokea zinatokana na changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia."

“Kwenye kero nilizozikuta wapo wanaume wanaonyanyaswa. Kuna wanawake wana fedha wanahitaji tu wanaume wa kuwaoa, hivyo anaweza kumpa kitu mwanaume na kumnyang’anya punde wakiachana,” amesema Makalla.

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza, “Nimeyaona hayo wale wanaume marioo waliozoea kitonga wanakuja ofisini kulalamika kuwa walipewa mali na wanawake lakini wakanyang’anywa.

“Sasa swali linakuja hii sio ukatili? Naona kuna mjadala mpana katika hili suala la unyanyasaji wa kijinsia ndio mana mjadala mzuri wenye lengo la kuboresha sheria za ndoa,”.

Mwananchi
 

Mwamba 777

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
1,265
2,000
walikubali kuolewa wenyewe, unapoolewa mwenye sauti na nguvu ni aliyekuoa, hivyo basi vijana walioolewa na hao wamama wakubali matokeo ya ndoa, waache utani hio ndo hali halisi hamna namna.
 

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
7,347
2,000
Kwa hiyo hao wanaume makala anataka kuwatetea kwa namna gani ....


Najaribu kuwaza sipati jibu...
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
14,133
2,000
Ndo maana sitaki kuishi dar.ni kuja kuchugua mzigo kula Bata kidogo na kutembea mbele watu karibia wote wamedata data
 

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
2,443
2,000
Makalla kama hajaenda shule vile.

Ni Makalla huyu RC hajui kuwa kuna wanawake wenye hela na wameajiri wanasheria ili kulinda maslahi yao.

Ni Makalla huyu hajui kuwa kuna wavulana makapuku waliotoroka shule wakakimbilia kuolewa na wanawake wajanja ambao ukimletea za kuleta utarudi mavumbini kama ulivyokuja duniani.

Wanaume wasio makapuku hawawezi kuanzisha ligi na hao wamama, hivyo wakijua kimenuka huachana nao kimya kimya wala hawaendi kushitaki kwa mama wala Makalla.

Wenye hekima (wanaume) msaidieni RC wa Dar naona kapungukiwa hekima japo ni mwanaume.
 

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,186
2,000
Makalla kama hajaenda shule vile.

Ni Makalla huyu RC hajui kuwa kuna wanawake wenye hela na wameajiri wanasheria ili kulinda maslahi yao.

Ni Makalla huyu hajui kuwa kuna wavulana makapuku waliotoroka shule wakakimbilia kuolewa na wanawake wajanja ambao ukimletea za kuleta utarudi mavumbini kama ulivyokuja duniani.

Wanaume wasio makapuku hawawezi kuanzisha ligi na hao wamama, hivyo wakijua kimenuka huachana nao kimya kimya wala hawaendi kushitaki kwa mama wala Makalla.

Wenye hekima (wanaume) msaidieni RC wa Dar naona kapungukiwa hekima japo ni mwanaume.
Tunataka haki
 

pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
8,003
2,000
Hizi kero rahisi rahisi tu,
Njoo kariakoo uone malori yanavyoziba njia na kuharibu barabara mpyaaaa haina hata mwezi hapo mtaa wa likoma na mtaa wa ndanda, narun'gombe, masasi na agrey

Hayo unayoongelea ni mambo ya mapenzi tu sie wengine hatuendi mpaka tuangushane kwa mieleka kwanza.
Mumeonea bureee wamachinga
Malori nikero zaidi
 

Msudu

JF-Expert Member
Aug 19, 2021
418
1,000
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salama, Amos Makalla amesema pamoja na kupokea kero za wanawake wanaokutana na unyanyasaji wa kijinsia wapo wanaume wanaohitaji msaada kutokana na changamoto za aina hiyo.

Akizungumza Alhamisi Novemba 25, 2021 wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Makala amesema sasa hivi wanaume wamekuwa na malalamiko dhidi ya wanawake wenye fedha.

“Nilikuwa na ziara ya kusikiliza kero za wananchi, asilimia 30 ya kero 927 nilizopokea zinatokana na changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia."

“Kwenye kero nilizozikuta wapo wanaume wanaonyanyaswa. Kuna wanawake wana fedha wanahitaji tu wanaume wa kuwaoa, hivyo anaweza kumpa kitu mwanaume na kumnyang’anya punde wakiachana,” amesema Makalla.

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza, “Nimeyaona hayo wale wanaume marioo waliozoea kitonga wanakuja ofisini kulalamika kuwa walipewa mali na wanawake lakini wakanyang’anywa.

“Sasa swali linakuja hii sio ukatili? Naona kuna mjadala mpana katika hili suala la unyanyasaji wa kijinsia ndio mana mjadala mzuri wenye lengo la kuboresha sheria za ndoa,”.

Mwananchi
Imeandikwa Mwanaume atakula kwa Jasho
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom