Polisi (TPF-NET) Arusha yawaonya Jamii za Kifugaji zinazoendelea na Ukatili kwa Watoto na Wanawake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Arusha kuelekea Siku 16 za kupinga ukatili umeendelea na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ambapo wametoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa jamii za kifugaji kata ya Lengijave wilaya ya Arumeru Mkao wa Arusha na kuwaonya baadhi ya wananchi wa jamii ya kifugaji wanaofanya ukatili kwa wanawake na Watoto.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed ambapo amesema mtaandao huo umeendelea na kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia huku akibainisha kuwa wameona vyema kuangalia kundi hilo la jamii ya kifugaji.

Ameendelea kusema kuwa lengo ni kuendelea kutoa elimu na kutoa ujumbe huku akibainisha kuwa hapo awali kulikuwepo na changamoto za ukatili kwa jamii hiyo ambapo amesema wanaendelea kutoa elimu ilikuwajengea uwezo wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kwa jamii hiyo ya kifugaji huku akitoa wito kwa jamii ya kifugaji kuchukia vitendo vya ukatili.

Sajeti wa Polisi Upendo Molleli amewataka wananchi wa Jamii ya Kifugaji kuendelea kutoa taarifa ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili wa wanawake na mabinti wa kimasai ambavyo vimekuwa chanzo cha kuwarudisha nyuma kimaendeleo makundi hayo.

d85985cf-b4a9-4979-a506-87564667b0a9.jpeg

5f34be9c-9d92-41b0-8eb7-c5d9404d5267.jpeg

Upande wake Edina Rabiki mkazi wa Kata ya Lengijave Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha licha ya kushukuru Jeshi hilo amesema kuwa jamii ya kifugaji ili kuwa na tabia ya kuoa Watoto wadogo ambapo ameushukuru mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha kwa namna ambavyo wameendelea kutoa elimu kwa makundi hayo ya kifugaji.

Nae Sajeti wa Polisi Upendo Molleli amewataka wananchi wa jamii hiyo ya kifugaji kuendelea kutoa taarifa ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili wa wanawake na mabinti wa kimasai kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili.
5f11ec5d-27ab-41bf-952b-fb3f28411be1.jpeg
 
Back
Top Bottom