Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

OJ simpson mwenyewe anasema hajauwa... Chenge anasema hajala pesa za rada. Nenda kwenye death roll yoyote kisha waulize wale wauwaji, wote watakwambia not guilt. Sasa what should we expect from masha?
 
Habari zinazotiririka sasa hivi ni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha amekanusha madai kukutana na watu wa SAGEM jinsi ilivyoripotiwa na gazeti moja nchini wiki iliyopita. Hata hivyo Bw. Masha amekiri kuwa katika tarehe iliyotajwa ni kweli alikuwa Uswisi. Habari zaidi zaja.

Awe alikutana nao au hakukutana nao hilo si tatizo kwake.

Tatizo ni kama alichukua chochote na akasema atawasaidia na deal likasambaratika hapo ndipo atalijua jiji.Hawatakubali yaishe kimya kimya atakonda mtu.
 
Hizi ni mbinu za kiutu uzima tu.Hata mimi nisingekiri kwamba nimekutana nao!

Habari zinazotiririka sasa hivi ni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha amekanusha madai kukutana na watu wa SAGEM jinsi ilivyoripotiwa na gazeti moja nchini wiki iliyopita. Hata hivyo Bw. Masha amekiri kuwa katika tarehe iliyotajwa ni kweli alikuwa Uswisi. Habari zaidi zaja.
 
Kama mwanakijiji alivyosema kwamba kukanusha siku zote ni rahisi kwa hiyo hapa cha kufanya ni kwa nipashe kutoa evidences zao zote walizonazo kwani hio itakuwa ni njia pekee ya kumbana Masha!
 
It seems you are the one who does not have a clue. This was a question of tendering, they said they wanted to tender-that will have definitely included all the aspects you have raised. Do you want to tell me that Masha's SAGEM has a track record of dealing with all the aspects you have raised? The answer is NO!. This government guys would have teamed up with other experts in the area and saved a lot of tax payers money. By the way, we have RITA which is a government agency dealing with such issues. They could have done the job as well. CCM guys are just looking for money there for fueling their presidential ambitions. Before it was Mungai, then Membe now Masha....this ID thing is a sniff!

Asha

Da' Asha, for $95 million you cannot do a nationwide ID system, maybe a laminated one that any Tom, Dick and Harry can do using a somewhat ok printer and lamination station! I have a feeling that the price tag is going to go up, way up simply because a smart card solution needs a smart card reader at every station that this id is going to be used - huyu mpigapicha wa serikali angeweza kudeliver vyote hivi kwa US $95million? Mavi kunuka!!

And yes, "Masha's SAGEM does have a track record of dealing with with all the aspects I have raisde", albeit not a good one maana na wao wameshawahi kuvurunda huko west Afrika.

For your information RITA is responsible, among other things, with registration of birth and deaths, marriages/divorces etc - a good national ID taps into their database, and many other databases kama za driver's licenses, business registrations, voter registration, land management etc, in a sense, all registration systems in Tanzania ambazo huyu mpiga picha wa serikali angebidi kutap into. Sasa simple ID za kuingilia Ikulu tu zinamshinda, sembuse national ID?

As I said, give me a break!
 
Last edited:
........du, hili balaa jingine, kwa kweli wabunge wetu Mungu awajalie wafanikiwe kupiga chini hiyo dili yakifisadi. Maana yawezekana ikawa ni stail ya kutafuta pesa za uchaguzi siunajua 2010 inakuja kwa kasi.
mkuu ni kweli, lakini itakuwaje kama hao wabunge ni miongoni mwa wanoimezea mate hiyo tenda ya vitambulisho?
 
What about Mpiga Chapa wa Serikali?😕😕😕


Sunday Feb 15, 2009

Six firms race for IDs project

DAILY NEWS Reporter, 15th February 2009 @ 10:18


The government has short-listed six companies from which only one could get a tender to produce the country’s first national identity cards using the smart-card technology. ..............................................................
.................................................................................

The six companies were identified as Unisys (South Africa), Giesecke & Devrient FZE (Dubai), Iris Corporation Berhad (Malaysia), Madra Security Printers (India), Marubeni Corporation in collaboration with Zetes and NEC (Japan) and Tata Consultancy Services in collaboration with Ontrack Innovations Ltd (India). The statement further explained that the second screening will begin soon, and that it is expected to be finalized soon.
[/B]

............................................................................................
.................................................................................................
[/COLOR]

Maybe ushauri aliyetoa mtu mmoja hapo juu kwamba ukiweka tundu la dari nyumbani kwako uende ukatafute fundi wa kutoka mbali na nyumba hiyo! Hii list haina local companies!

This means, there will be no transfer of technology to wazawa! This means whoever implements this system will have to own it outright by establishing an office here in TZ and staffing it with their own people or run it remotely from wherever they come from.....meaning kitu kikikorofisha inabidi kiwe routed through their offices wherever they are - it will be damn expensive!! Kaaazi kwelikweli!

If there is a transfer of technology through a local company is much better kwani wazawa wanapata kazi na uelewa/ujuzi wa technologia, mradi unakuwa owned na sisi wenyewe. Kuna mifano mingi sana ambayo through transfer of technology we are managing our own shit - Passports, Police fingerprint id system, kadi za nssf kwa wale wanachama etc etc

I sincerely hope they know what they doing - at least they eliminated the joker known as Mpiga Picha wa Serikali! LMAO!
 
Huu ndio mchakato wa vitambulisho vya Taifa
Yafuatayo ni mahojiano kati ya Mwandishi Wetu Sarah Mossi na Mkurugenzi wa Gotham International Limited, Jack Steven Gotham

SWALI: Ulipataje hii tenda? Mlishindanishwa na kampuni nyingine?

JIBU: Mradi ulikuwapo siku za nyuma, ulipitishwa na Bunge mwaka 1986, akini wazo la kuwapo vitambulisho vya Taifa lilizaliwa 1968 na nchi nne za Tanzania, Kenya, Malawi na Zambia. Marais wa nchi hizi walifikiria juu ya kuwapo Muungano lakini baadaye wazo hili likakwama.

Mwaka 1972 wazo hili likaibuka tena lakini bado likakwama. Mwaka 1995 wakati nchi ilipoingia katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kila chama kikilalamikia chama kingine kwamba kilipandikiza watu toka nje ya nchi kupiga kura, wengine wakapiga kura zaidi ya mara mbili na wengine walipiga kura chini ya umri wa miaka 18. Wewe ni shahidi wa yaliyokuwapo Zanzibar. Likaja wazo la kuwe na vitambulisho vya Taifa ambalo lingeweza kuondoa malalmiko haya. Lakini likaja wazo jingine kwamba hatuna hela wala teknolojia na wakasema tujigharimie watu wanunue vitambulisho.

Mwaka 1996, Serikali wakaita tenda ya wazi na kampuni ya Regional Services Ltd ikashinda tenda hiyo. Kampuni hii ilisajiliwa katika visiwa vya Isle of Man nchini Uingereza. Ni ngumu sana kuitress kwani kampuni kama hizi husajiliwa kwa ajili ya kupata unafuu wa kodi na unaweza kufungua kampuni kwa saa tu. Mmiliki wake alikuwa Nairobi akiitwa Horatius Dagama-Rose, huyu alikuwa muasia wa Kabila la Goa.

Wakati akiwa katika mjadala na serikali alitaka kujua idadi ya Watanzania atakaoshirikiana naye pamoja na idadi ya watu nchini lakini serikali ikayumba katika majadiliano, ilikuwa haina uhakika na idadi ya watu. Na alikuwa mjanja baada ya kuona serikali inayumba akapandisha bei ya tenda aliyoshinda na kuruka mara mbili.

Serikali ikakataa na kutaharuki na kumtaka aandike hayo kwa maandishi kwa sababu hakukuwa na proper procurement procedure. Hii kampuni ikaipeleka serikali mahakamani na mahakama ikasema pande zote mbili zirudi mezani. Ndipo serikali ikashinda kwa kampuni ile kushindwa kuthibitisha gharama kubwa waliyoipandisha.

Wakati wote huo kukawa na shinikizo kubwa kutoka kwa nchi wahisani wakisema ni lazima iwepo vitambulisho kwa ajili ya uchaguzi, ili kutatua migogoro inayojitokeza wakati wa chaguzi.

Na wakati wote huo nilikuwa Special Envoy wa Rais Laurent Kabila DRC niliwavutia watu nyumbani wakasema naweza kusaidia kutatua tatizo la Vitambulisho vya Taifa nikaitwa na serikali kuja kutoa ushauri juu ya nini kifanyike.

Kutokana na uzalendo kwa nchi yangu niliishauri serikali mambo manne. Moja ni kwamba mradi huu asipewe mtu binafsi kwa sababu ni la usalama wa taifa. Jambo la pili nikashauri kiundwe chombo cha Serikali kitakachosimamia huo mradi.

Nikashauri pia vitambulisho vitolewe bure na tuwapigie magoti wahisani watusaidie kwani kwa kuwa na vitambulisho nchini tutakuwa tunajua nguvu kazi zetu ni za namna gani, tupeleke maendeleleo kwa kina nani, utakuwa unajua idadi ya watumishi ulionao serikalini pamoja na idadi ya walimu uliyonayo.

Nikashauri pia kitambulisho kilenge kumsaidia Mtanzania katika uchaguzi na kitaondoa kelele za watu kupiga kura mara mbili au kupiga kura chini ya umri. Nikawaaambia tukiyabeba haya tutapata fedha mara moja toka kwa wafadhili na hatutotumia fedha katika bajeti yetu.

Na ili kuyaweka haya vizuri nikashauri uwapo utafiti wa kina ili tuyaweke haya kimaandishi na iwepo andiko ambalo serikali italitumia kuelimisha watu wake juu ya umuhimu wa vitambulisho vya taifa.

Nikawaeleza serikali watafute mtu wa kufanya feasibility study na mimi nitaendelea kumshauri huyo mtu lakini nitakachosaidia ni kutengeneza hadidu za rejea utafiti huo. Nikatengeneza nikawaeleza nitaendelea kutoa ushauri ili kuendelea kuleta yale tunayohitaji Tanzania.

Lakini niliwashauri pia watafute kampuni kama za National Statistic Bureau na TISCO katika hili hawa kwa miaka mingi walikuwa wakitengeneza project nyingi za serikali, pia nikashauri wawatafute wataalamu pale UDSM wa kitengo cha Research Economic Bureau ambao hawa ni wataalamu wa mfumo wa mawasiliano wangewasaidia sana kwani ukija na huu mradi lazimi ujue nani duniani amewahi kuwa na vitambulisho kama hivi.

Serikali ikasema wakitangaza tenda hawana bajeti ya ufatifi huo ingawa walikuwa wakiamini hii ni muhimu. Wakati huo mimi nikaanza kupiga ndogondogo Jumuia ya Ulaya. Hawa wakasema tuko tayari kufadhili mradi ila tuletewe feasibilitu study yenu.

Nikaona aibu kurudi kwa EU kuwaambia hatuna hata hela ya kufanyia feasibility study. Wakati wote huo nilikuwa nikiendelea kushauriana na serikali nini kifanyike.

Ushauri wangu kwa serikali wazichukue taasisi nilizozitaja ili wajadiliane nao kiserikali. Bado mimi milikuwa naendelea kushauri bila malipo.

Walipokwenda ikaonekana hizi taasisi wanahitaji kulipwa ndipo serikali wakaomba niwasaidie niongee na EU. Nikawaambia waende kwa Rais lakini bado wakawa wagumu. Wakati huo Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Mohammed Seif Khatib baadaye akaja Omar Mapuri.

Na wakati wote huo nikiwa katika hali ngumu huku EU wakizidi kunitia presha ndipo nikasema nione nitakavyoweza kusaidia na kuanza kuzungumza na rafiki zangu hapa Tanzania nikawaeleza hali halisi wakaahidi kuona itakavyokuwa, hiyo ilikuwa 2003—04.

Nikawaeleza Serikali nipo tayari kufanya feasibility study kwa kushirikiana na timu yangu lakini je nitalipwa vipi? Kwa vile nakopa hela za watu, Serikali ikajibu tutakulipa na kunihakikishia kunilipa baada ya kuwa approved. Ndipo tukashauriana na rafiki zangu tuisaidie serikali. Nilifika mahali nikaacha shughuli zangu. Ilitugharimu na ikafikia kuogopa iwapo serikali haitolipa hela za watu lakini kwa kujenga uaminifu kwa watu waliotoa fedha zao bila riba kwa nia ya kuisaidia serikali.

Nikaanza kuangalia katika Afrika kuna vitambulisho katika nchi za Kenya na Afrika Kusini na Switzerland na kuanza kuwasiliana na watu wangu kule. Nikaendea Afrika Kusini kuangalia vitambulisho vyao na kupata picha ya wenzetu wanavyofanya. Kenya hatukuridhika sana, lakini hata Afrika Kusini nako tukaona havikidhi haja.

Tukaanza kuzunguka dunia nzima kila tunakosikia kuna vitambulisho na sapoti ya serikali katika safari zetu zote ni kupata connection ya nchi tunayokwenda ili tusaidiwe kiserikali.


© New Habari (2006) Ltd
All rights reserved
 
Hivi jamani kabla hatujaendelea na michanga hapa, ebu mtu anayefahamu vizuri atwambie sura ya hiyo National ID itakuwaje (physical appearance, on its face itaonyesha taarifa zipi e.g jina, birth date etc), pia itakuwa na features gani (data gani zitakuwa stored in it), na je, standard cost per unit ya kutengeneza hii kitu ni kiasi gani (angalia nchi ambazo zinavyo tayari), na je, kutakuwa na kuupdate data on it? Je, kwa changes zinazotokea i.e new births, deaths.....tutakuwa tunatangaza tender upya?

If anyone has a clue on these questions...please help, then tutachangia vizuri!
 
Mimi nafikiri habari yenyewe kuhusu masha ina ukweli kidogo, si suala la kupokea rushwa au kukutana na hao wa SAGEM. Mimi nafikiri issue ni kuingilia mchakato wa upatikanaji wa mzabuni kinyume na sheria. kama alikuwa anajua sheria ya manunuzi kwa nini alilamika kwa waziri mkuu kuhusu kutengwa akijua kuwa yeye ni afisa wa rufaa katika swala la uzabuni? nafikiri kwa hilo hakutumia busara na sheria na hilo kwangu mimi naona ndilo kosa lake. alikuwa na utashi gani kuandika barua na kwa maslahi ya nani? kwanini hakuripoti PPAA ambayo inasikiliza rufaa za mtu ambaye anafikiria kuwa ameonewa na kamati ya Zabuni.

tufike mahali wanasiasa waaachie watendaji wa wizara na serikali wafanye kazi yao. mimi nafikiri isingekuwa wanasiasa Richmond isingetokea. so lets put politics aside when it comes to expert matters.
 
Hivi jamani kabla hatujaendelea na michanga hapa, ebu mtu anayefahamu vizuri atwambie sura ya hiyo National ID itakuwaje (physical appearance, on its face itaonyesha taarifa zipi e.g jina, birth date etc), pia itakuwa na features gani (data gani zitakuwa stored in it), na je, standard cost per unit ya kutengeneza hii kitu ni kiasi gani (angalia nchi ambazo zinavyo tayari), na je, kutakuwa na kuupdate data on it? Je, kwa changes zinazotokea i.e new births, deaths.....tutakuwa tunatangaza tender upya?

If anyone has a clue on these questions...please help, then tutachangia vizuri!

Physically it will look as your normal ATM card with your name, photo, and address and probably a unique number, but it will have a chip that will store your biometric info ie fingerprints, and will have all your pertinent information such as names, picture, birth dates/place, living address etc and a unique id/number that will immediately identify you wherever you go and won't create duplicates e.g ukienda kupata id kwa jina lako Next Level basi info zote zitakuwa stored in that chip na ukija omba drivers license utaulizwa id yako ipo wapi na ukitoa itasomwa na card reader na utakuwa issued a drivers licence with the same name and not Level Next au jina lingine, hata kama ukienda kufungua account bank au kuomba TIN kule TRA utatumia jina hilohilo, signature hiyohiyo.

Waulize watu wanaofanya kazi kwenye mabenki, au TRA etc wanavyohangaika na multiple names of account holders ndio utaelewa umuhimu wa kuwa na a unique id card.
 
Sidhani wakati wote unahitaji local professionals kufanya kazi.Kuna suala la security na ufichaji teknolojia watu wasiibe wakaanza kuvitengeneza ovyo.

Swali ni je Mpiga chapa wa serikali anayo credibility ya kuficha siri ya tecknolojia yake ya kuchapisha document za siri? Wafayakazi wake waweza aminika na wana historia ya uaminifu wa kuficha siri na kutochapisha vya ziada na kuwapa wageni mamluki?

Documents nyingi zenye features za siri zikiwemo passport,fedha,cheki na kadhalika za nchi nyingi tu duniani huchapishwa na nchi nyingine si kuwa wataalamu wanakuwa hawapo katika nchi hizo nadhani hata marekani hawachapi passport na pesa zao huchapishwa kwingine pamoja na uwezo mkubwa wa teknolojia walionao.India pekee ndio nasikia wanachapa pesa zao wenyewe nchini mwao.Nadhani inawezekana kwao sababu culture ya wahindi ni wasiri mno wao labda wwanaweza mambo haya.Ila kwa watanzania sijui.Mtu akipewa hiyo kazi kusema akilewa hataropoka kwenye baa sijui.

Labda kama mpiganaji nitoe siri ndogo ya kivita kwa wanaojenga nyumba.Unapojenga nyumba unapoweka dari usimchukue fundi wa kupiga dari wa karibu na eneo unaloishi.Mtafute fundi toka mbali hata kama wapo mafundi wengi tu kwenye eneo unaloishi.Sababu ni kuwa kwenye dari kuna lile tundu unalomalizia kufunga dari ambalo mtu aweza kupanda akitaka kuingia darini.Lile tundu unalomalizia kufunika dari ni eneo la vita hatakiwi mtu ajue liko wapi asijue liko sebureni,chumbani,jikoni,au wapi.Wakija majambazi waweza panda kwa spidi ya mwewe darini ukawasubiria kwenye eneo la tundu ya dari na bastola au bunduki yako au jiwe lako la fatuma.Sasa majambazi yakikaribia hilo eneo unalifungua kwa spidi ya mwewe na kuwamiminia risasi na kurukia mbali eneo lingine ambako hata warushe risasi hawakupati au ukishawamiminia risasi kwa spidi unafumua bati au kigae na kuruka nje na kukimbia kwa spidi ya kenge aliyejeruhiwa kusalimisha maisha yako au kuitia msaada au kuhamishia vita nje kweupe kwenye uwanja mnapoweza kuonana vizuri.

Sasa kama kazi ya kumalizia dari ukimpa fundi wa maeneo jirani aweza mwaga siri kwa majambazi wakajua eneo lako la kujidai kivita liko wapi.Ina maana unampa fundi wa mbali si kwa sababu mafundi hawapo bali una vitu hutaki vijulikane hovyo kwa usalama wako.

Sipingi wazawa kuchapisha lakini kuna vitu vingine kinachoangaliwa si uwezo tu wa kufanya kazi lakini pia usiri,usalama n.k Kama waweza na wana historia ya usiri na usalama wapewe si kuchapa vitambulisho tu bali hata pasipoti na kazi za kuchapa pesa wawape tu.

Lol

Mzee mfano wako ni mzuri sana, na unafurahisha.

Lakini kwa upande mwingine kama hilo tundu la dari lingekuwa linaji-loki siku za baridi mpaka umtafute fundi aliyelikutengenezea, pengine ungebadili mawazo. Kama hilo tundu la dari lingekuwa linatakiwa liwe na mfanyakazi wa kulitazama kila siku, au tundu lako la dari linahitaji ukarabati kila wiki, pengine ungebadili mawazo. Kama tundu lako la dari lingekuwa linahitaji mashine kuubwa za kutengenezea ambazo kuzisafirisha ni gharama kubwa, nahisi ungemshauri hata huyo fundi wako wa mbali akodishe hizo mashine karibu kama zipo ili gharama zako zipungue. Kama tundu lako la dari kulifunga na kulifungua unahitaji password ambayo anakaa nayo fundi aliyetengeneza, pengine ungebadili mawazo. Au mbaya zaidi kama tundu lako la dari huwa linahamahama na ili kujua lilipo inabidi umuite fundi aliyelitengeneza aje akuonyeshe lilipo, hapo ungetamani kumuajiri awe anakaa huko ndani kwako tu ... au ungemtengea helkopta standbay ili ukivamiwa na majambazi fundi aletwe faster?
 
Jamani mi naomba nitoe mchango wangu: Mi sidhani kama waandishi makini kama Raia Mwema na Nipashe (mwandishi ndo huyo huyo wa This Day) wanaweza kuandika kitu wasichokuwa na uhakika nacho. Mi nadhani kwamba kuonyesha passport kuwa alirudi kutoka Dubai okt 1 haina maana kuwa waandishi hawajakosea tarehe. Inawezekana kuwa alifika Geneva tarehe 5 hiyohiyo. Sasa Okt 1 ina maana gani? Pili, je kama walikosea na badala ya oktoba ilikuwa Septemba 5/
Mi nadhani Masha angetakiwa afanye full disclosure kusema hajaenda kabisaa Geneva basi tutakubali. Huyo aliyemfanyia interview TBC alikuwa pale kumpa leading questions hii si thibitisho. The question is: "Did you go to Geneva to attend the conference?" "Did you meet the aforementioned gentleman from Sangem?" Akianza kusema oh, tarehe... unamwambia, "The date doesn't matter, did you or did you not meet the Sangem representative and visit the company?" Akiendelea kukana, unamwuliza, "Are you ready to say this under oath?' Ahhh! Yaani wengine tungepata chance tungefanya "Hardtalk" wanasiasa wote wangeacha usanii wao!
 
Shalom,

Next time don't attack me personally.

inawezekana tatizo limeanzia pale ulipotangaza kwamba humpendi mzee mengi badala ya kutangaza kutoyapenda mambo yake!!!!kwahiyo basi mkulu usishangae watu wengine nao kukujadili wewe badala ya kujadili hoja yako.
Kwahiyo mkulu inabidi uwe mvumilivu tu, hii ndiyo JF bwana, where everybody dare to talk openly!!! tehe.....tehe....teheeee......!!!
 
Jamani mi naomba nitoe mchango wangu: Mi sidhani kama waandishi makini kama Raia Mwema na Nipashe (mwandishi ndo huyo huyo wa This Day) wanaweza kuandika kitu wasichokuwa na uhakika nacho. Mi nadhani kwamba kuonyesha passport kuwa alirudi kutoka Dubai okt 1 haina maana kuwa waandishi hawajakosea tarehe. Inawezekana kuwa alifika Geneva tarehe 5 hiyohiyo. Sasa Okt 1 ina maana gani? Pili, je kama walikosea na badala ya oktoba ilikuwa Septemba 5/
Mi nadhani Masha angetakiwa afanye full disclosure kusema hajaenda kabisaa Geneva basi tutakubali. Huyo aliyemfanyia interview TBC alikuwa pale kumpa leading questions hii si thibitisho. The question is: "Did you go to Geneva to attend the conference?" "Did you meet the aforementioned gentleman from Sangem?" Akianza kusema oh, tarehe... unamwambia, "The date doesn't matter, did you or did you not meet the Sangem representative and visit the company?" Akiendelea kukana, unamwuliza, "Are you ready to say this under oath?' Ahhh! Yaani wengine tungepata chance tungefanya "Hardtalk" wanasiasa wote wangeacha usanii wao!


Mkuu Susuviri, kama wewe si mwandishi nakushauri ingia huko haraka ukatusaidie. Kama hutaki kwenda moja wka moja, uwe unafanya part time hasa kwenye tv au radio ili uwabane hawa wanaorushwa maswali mepesi mepesi
 
mimi naona hapa wanaangalia zaidi vitu vingi sio bei peke yake
nazani huyu mchapaji wa serikali hana uwezo wa kuweka some features maana ni ishu ya utambulisho wa taifa so it must contain a lot of things in it na wameshaangalia upande huo wakaona solution isiwe bei bora wala bora bei iwe na uwezo thats ALL
 
Leo Masha amejaribu kujitetea wakati anahojiwa na TBC1. Hata hivyo amenishangaza pale aliposema kuwa ile barua kwa PM ilikuwa kwa ajili ya kumweleza maendeleo ya uchambuzi wa tenda (Just a note to give him a sort of progress report)???? Je kwa wale walioiona hiyo barua inafanana na progress report? Pia amekanusha kukutana na Segem huko Uswiss na akasema tarehe zilizotajwa hakuwa Geneva bali aliondoka Dar 5 Oktoba 2008. Nani anasema ukweli hapa?? Yapo mengi aliyojaribu kusema lakini jingine la kushangaza ni kuwa Segem imetolewa kwa sababu ilitoa malalamiko kuhusu tenda bila kufuata utaratibu.

Kwa hiyo LM anasema hana kashfa yoyote na hawezi kujiuzulu. Hata hivyo amesema kama kuna ushahidi wa kuonesha kuwa alivunja sheria yuko tayari kuanchia mchuma.

Hata chenge aliwaambia waandishi wa habari hivihivi kuwa hakuna sbb ya yeye kujiuzulu kwa kuwa hana kashfa yeyote
 
Mimi nafikiri habari yenyewe kuhusu masha ina ukweli kidogo, si suala la kupokea rushwa au kukutana na hao wa SAGEM. Mimi nafikiri issue ni kuingilia mchakato wa upatikanaji wa mzabuni kinyume na sheria. kama alikuwa anajua sheria ya manunuzi kwa nini alilamika kwa waziri mkuu kuhusu kutengwa akijua kuwa yeye ni afisa wa rufaa katika swala la uzabuni? nafikiri kwa hilo hakutumia busara na sheria na hilo kwangu mimi naona ndilo kosa lake. alikuwa na utashi gani kuandika barua na kwa maslahi ya nani? kwanini hakuripoti PPAA ambayo inasikiliza rufaa za mtu ambaye anafikiria kuwa ameonewa na kamati ya Zabuni.

Kwa maneno yake mwenyewe LM, amesema alimwandikia PM kumpa taarifa ya maendeleo ya zabuni (like a progress report). Na kwamba SEGEM waliondolewa kwa sababu walivunja sheria kwa kulalamika kabla process haijaisha!! Ila hakusema kama waliyempelekea malalamishi yao alivunja sheria au la!!

tufike mahali wanasiasa waaachie watendaji wa wizara na serikali wafanye kazi yao. mimi nafikiri isingekuwa wanasiasa Richmond isingetokea. so lets put politics aside when it comes to expert matters.

Mara 2 zote ambazo nimemuona LM akijitetea kupitia TBC1 sijaona kama ana chembe yoyote ya sifa za kumfanya aitwe mwanasiasa. Wakati wote anakuwa mwoga na nadhani yale maswali wanakuwa tayari wameyapitia pamoja (yeye na Marini Hassani) na kukubaliana. Kwa jinsi anavyoonesha wasi wasi ukimweka kitimotoa (kama kwenye hardtalk) anaweza kuvunja kamera! Hili ni tatizo kubwa kwa nchi yetu, siku hizi hatuna wanasiasa bali tuna wafanyabiashara na wajasiriamali wanaofanya siasa!😕
 
Masha atoe uthibitisho kwani si mara ya kwanza kutuhumiwa. Je mnakumbuka kwenye kesi ya Babaye ilitamkwa mahakamani alilitukana jeshi la polisi?
 
Back
Top Bottom