Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

(Samahani nje ya mada🙂 Sheria hii ni sheria dume kama mhusika ni wa kike?
Miaka ile wakati napitiapitia mambo ya sheria nshawahi kusoma kuwa in law they have used a masculine gender just for the purpose of ease in writting.The principles apply to both genders.In short as far as law is concerced then 'he' includes 'she' in it!!
 
A thought of the day

1.I'm I working on forming a better tANZANIA ? Imp not there yet, but am work in progress...What about you?

2. And to all Christians out there," 2 Chronicles 7:14 If my people, which are called by my name, shall humble themselves, and pray, and seek my face, and turn from their wicked ways; then will I hear from heaven, and will forgive their sin, and will heal their land.
Are we upholding our leaders in prayers? Are we repenting, on behalf of this nation, are we seeking godly solutions, or are we in the bandwagon of complaining.
 
invisible/ wana jf

naomba mtume tena ile attachment yenye barua ya masha kwenda kwa waziri mkuu pinda. Niliifungua juzi nikaisoma nusu sasa nataka kuimalizia kuisoma tafadhali

asanteni kwa ushirikiano wenu

hiyo ipo katika forum moja inaitwa bidii afrika mashariki
 
Kilichobaki skendo mingi sana. Aachie ngazi!!! Hivi anasubiri nini?? Au ndo tuseme mwanume kufa na tai shingoni?
 
Invisible/ Wana JF

Naomba mtume tena ile attachment yenye Barua ya Masha kwenda kwa Waziri Mkuu Pinda. Niliifungua juzi nikaisoma Nusu sasa nataka kuimalizia kuisoma Tafadhali

Asanteni kwa Ushirikiano wenu

Duh, wewe kifimbo inaonekana kama kungekuwa na kiingilio cha kusoma hiyo barua ungeomba ulipie nusu sababu hukumaliza!
 
Date::2/14/2009
Vitambulisho: Mpigachapa wa serikali angechapa kwa Sh95bn badala Sh222bn
Na Lauden Mwambona
Mwananchi

WAKATI serikali ikiendelea na mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya uraia ya Sh222 bilioni, imebainika kwamba kiasi hicho cha fedha ni kikubwa mno na kama wangemtumia Mpigachapa wa Serikali kazi hiyo ingetumia Sh95 bilioni tu.

Habari zilizopatikana zinaeleza kwamba, ingawa mpigachapa wa serikali alishaomba zabuni hiyo kufanya kazi hiyo, lakini hajachaguliwa bila ya sababu maalumu.

Siri hiyo ilifichuka juzi wakati Kamati ya Bunge ya Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Miscellaneous Amendments) ilipotembelea ofisi ya Mpigachapa Mkuu kujionea utendaji kazi ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Benson Mpesya ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini kupitia CCM na kugundua kuwa ofisi hiyo ya serikali ina uwezo wa kufanya hiyo kazi kwa bei nafuu zaidi.

Mbunge wa Moshi mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Philimon Ndesamburo ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa serikali, itoe sababu za kuikatalia Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wake, kuandaa vitambulisho vya uraia kwa gharama ya Sh95 bilioni badala yake kung'ang'ania zabuni itakayogharimu Sh222 bilioni.


Akifafanua hoja yake mbunge huyo, alisema akiwa kwenye ziara hiyo, alimuuliza Mpigachapa Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo, kama Ofisi yake inao uwezo wa kuchapa vitambulisho vya taifa na aliwajibu wajumbe wa Kamati ya Bunge kwamba, ofisi yake inaweza kutengeneza vitambulisho hivyo kama itapatiwa fedha.

Mbunge huyo alimkariri Chibogoyo akisema kwamba, ofisi yake ilishaomba kazi ya kuchapa vitambulisho hivyo kwa gharama ya Sh95 bilioni miaka miwili iliyopita, lakini hadi sasa hajui kinachoendelea.

Ndesamburo alisema kauli ya Mpiga Chapa iliwashitua wajumbe wote wa kamati hiyo iliyoambatana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

"Mimi ninachotaka kujua kutoka serikalini ni kwa nini isiimarishe zaidi ofisi yake ambayo mpaka sasa inachapa siri nyingi za serikali kwa kuipatia kazi hiyo hata kama ni Sh150 bilioni kwa sasa, ili kuondokana na utata unaoendelea?" alihoji.

Mbunge huyo alisema mpigachapa mkuu alieleza kwamba, kabla ya kuomba kazi hiyo alifanya utafiti katika nchi kadhaa ikiwamo Ujerumani na kuona wazi kwamba, kazi hiyo ingefanyika kwa kiwango cha kimataifa kwa gharama ya Sh95 bilioni.

"Serikali ingepunguza gharama na kuondoa malumbano yanayoendelea kama ingetoa kazi kwa Ofisi yake (mpiga chapa), ambayo inaongozwa na mtu ambaye alikuwa Rais wa Shirikisho la Wapigachapa wakuu duniani," alisema na kuongeza:

"Mpigachapa Mkuu anasema sehemu ya fedha hizo zitatumika kununua mtambo wa kisasa ambao baada ya kuchapa vitambulisho utabaki hapa hapa nchini."

Chibogoyo alipopigiwa simu jana ili kufafanua taarifa hizo, alikataa katakata kuzungumzia suala hilo kwa maelezo kwamba, mambo ya wabunge yanatolewa na wabunge wenyewe.

Naye Mpesya licha ya kukiri kwamba kamati yake ilitembelea ofisi hiyo ili kupata maelezo mbalimbali hususan jinsi ya kuchapa sheria, hakutaka kufafanua zaidi juu ya yaliyojitokeza.

Akizungumzia hali hiyo jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, alisema kwa sasa bado mchakato huo unaendelea, hivyo hawezi kuzungumza lolote juu ya suala hilo kwa kuwa kila mmoja ameomba tenda na serikali bado inaendelea kuzichambua.

"Kwa kuwa mchakato wenyewe bado haujaanza, siwezi kusema lolote juu ya hilo, hivyo basi nakuomba usubiri mpaka zoezi hilo litakapokamilika ndipo ujue ni nani ameshinda tenda hiyo na kuniuliza swali lako," alisema Masha.

Aliongeza kuwa kuchelewa kwa mchakato wa kutengeneza vitambulisho vya uraia, kunatokana na kumtafuta mzabuni mwenye sifa anayeweza kusimamia kazi hiyo kwa umakini.

Kazi ya kuchapisha vitambulisho vya uraia imekuwa chanzo cha mvutano mkubwa miongoni mwa wanasiasa na baadhi ya watendaji wa serikali.

Katika mkutano wa bunge uliomalizika wiki hii mjini Dodoma, Mbunge wa Karatu, Dk Wilibrod Slaa alitaka kuwasilisha hoja binafsi akidai kuwa waziri Masha ameingilia kati mchakato wa kuchapisha vitambulisho hivyo kinyume cha taratibu.

Hata hivyo, hoja hiyo ilishindwa kujadiliwa na wabunge baada ya Spika kuizuia kwa maelezo kwamba, kufanya hivyo ni kuingilia kati mchakato mzima wa zabuni hiyo unaoendelea.

Suala la kuchapisha vitambulisho vya uraia nchini, limekuwa likiingia utata mara kwa mara kutokana na baadhi ya wakubwa kudaiwa kutaka kujinufaisha na zabuni hiyo.

Mchakato wake wa zabuni ya kuchapa vitambulisho hivyo ulianza mwaka 2004 na kwamba, umekuwa ukisuasua kutokana na kuzingirwa na mizengwe.

Mradi huo ulioanza kuzungumzwa miaka ya katikati ya 1970 na ambao utagharimu kiasi cha Sh222 bilioni, unaelezwa kwamba umo katika hatua za mwisho za kutaka kutekelezwa japo taarifa zinaonyesha kwamba, ni mpango mwingine mkubwa wa ulaji fedha za umma.

Mbali na suala la vitambulisho, Ndesamburo alisema kipindi hiki ni cha wanasiasa mafisadi kujuta kwa kuwa wataendelea kuumbuliwa.

Alisema kipindi hiki ni onyo kwa viongozi waliopo madarakani kwamba wasipotekeleza wajibu na kupenda ufisadi yatawafika makubwa wakati wowote.

Kuhusu masuala ya jimbo lake alisema wapiga kura wake wapo imara na wanampenda na kuipenda Chadema.

"Nilitaka kung'atuka, lakini wanachama wenzangu Moshi mjini wamenitaka niendelee kipindi kijacho, hivyo nitagombea ili CCM waendelee 'kusota'," alifafanua.
 
Mkuu BUBU katika hoja za leo niligusia kuwa imefika mahali pa Watanzania kuonekana WAJINGA na WAJINGA NDIO WALIWAO. hebu mtu alete JUSTIFICATION kutoka bilioni 95 mpaka bilioni 222. Kuna WIZI wa mchana hapa nadhani ni bora tudai hili ZOEZI ZIMA LA VITAMBULISHO lismamishwe mara moja. nina hakika mahali fulani BLA BLAA ya faida ya hivyo vitambulisho itakuwa imezungumzwa au kuelezewa nafikiri kuna haja ya kusita na kufikiria tena.
 
........du, hili balaa jingine, kwa kweli wabunge wetu Mungu awajalie wafanikiwe kupiga chini hiyo dili yakifisadi. Maana yawezekana ikawa ni stail ya kutafuta pesa za uchaguzi siunajua 2010 inakuja kwa kasi.
 
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote

Nchi yangu Tanzania, Jina lako ni tamu sana,

Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee,

Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote



Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini,

Kutazamaa maajabu, biashara nayo makazi

Sitaweza kusahau mimi

Mambo mema ya kwetu kabisa

Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote



Hivi hii tuliimba wote au wengine wametokea Zambia?
 
Ths 222 billion -Tshs 95 billion=Tshs 127 billion for CCM 2010 ELECTION
 
Mmh,hawa waandishi&wahariri nao...Hivi kweli kuna kitu kama 'vitambulisho vya URAIA'??
 
Mmh,hawa waandishi&wahariri nao...Hivi kweli kuna kitu kama 'vitambulisho vya URAIA'??
Thread hijack??
Ths 222 billion -Tshs 95 billion=Tshs 127 billion for...
...hebu mtu alete JUSTIFICATION kutoka bilioni 95 mpaka bilioni 222. Kuna WIZI wa mchana hapa...
The margin couldn't be justified unless Ndg. Chibogoyo shade light about his institution proposal. Lazima tujue proposal yake ilikuwa inatoa solution ipi, I mean, final output yake inafanana na hizi zinazogharimu Tshs. 222 bil.?

Kuna umuhimu naye aitwe kwenye Kamati (maana ameshaonesha woga kuhesabiwa) ili kama solution yake ni justifiable and secure basi waangalie namna ya kurekebisha zoezi zima kwa maslahi ya nchi.
 
Tuwe waangalifu. Cheaper is not always better. Kuna sehem taifa limeingia gharama mara mbilimbili kwa kukimbilia cheapest bidder. Kuchapa siri za serikali na kutengeneza microchip embeded National IDs ni vitu tofauti. Tuna mifano ya barabara mkoani singina serikali ilibidi ilipe mara mbili, kunamifano ya AFIS system ya polisi ambayo the cheaper guy ameishia kutengeneza kitu kisichokua na function ya kueleweka na mabilioni amekula.

Labda tungeanza kwa kujiuliza kama tunahitaji kweli hizo Smart Card IDs au hata simple
magnetic strip Card zitafaa, au hata pengine hatuhitaji hizo Card kabisaa kwa sasa. Mpiga chapa nae asije akatuingiza mkenge kwa business asiyoijua vizuri.
 
Tuwe waangalifu. Cheaper is not always better. Kuna sehem taifa limeingia gharama mara mbilimbili kwa kukimbilia cheapest bidder. Kuchapa siri za serikali na kutengeneza microchip embeded National IDs ni vitu tofauti. Tuna mifano ya barabara mkoani singina serikali ilibidi ilipe mara mbili, kunamifano ya AFIS system ya polisi ambayo the cheaper guy ameishia kutengeneza kitu kisichokua na function ya kueleweka na mabilioni amekula.

Labda tungeanza kwa kujiuliza kama tunahitaji kweli hizo Smart Card IDs au hata simple
magnetic strip Card zitafaa, au hata pengine hatuhitaji hizo Card kabisaa kwa sasa. Mpiga chapa nae asije akatuingiza mkenge kwa business asiyoijua vizuri.

Sober
Am sure we need National IDs. Its also true that cheap sometimes is expensive! but when we will start using our proffesionals in our country? Wanatakiwa wafanye kazi ya ku-prove we always judge them wrong! Hatutaendelea kuabudu na kuamini kuwa vyote vilivyobora ni lazima vitoke ama vitengenezwe na watu wa nje.
Mfano
Wakati wa mkutano wa Sullivan pale arusha, tulikuwa na wataalamu wetu pale na walitengeneza Ids za chap chap na ni bora tu. Tunachotakiwa hapa ni Chibogoyo atueleze namna anavyotaka kutengeneza hizo IDs ili ziendane na technogy ya sasa. Its time we start using our people now!
 
Vitambulisho: Mpigachapa wa Serikali apewe hii zabuni. Sio tu kwamba yeye ameshaonyesha gharama zake ni ndogo (Sh 95bn badala ya Sh 222bn), bali kazi ikifanyika hapa nchini, vijana wetu watapata kazi na pia uzoefu.
Ijulikane kwamba uchapishaji wa vitambulisho utakuwa ni huduma ya kudumu kwa vile Watanzania wapya kila mwaka watakuwa wanahitaji utambulisho. Hata ikiwa ni lazima kwa sasa tuagize mitambo mipya, basi hiyo itakuwa ni uwekezaji wenyewe. Rais Kikwete ashauriwe kutupilia mbali zabuni zote za nje, na Serikali yake iimarishe Idara ya Mpigachapa wa Serikali na kuipa hii tenda.

Kilasara (JM Member)
 
uchaguzi 1961 - Account ya chama cha ushirika nyanza na kilimanjaro (NFCU + KCU)
uchaguzi 1965 - Paund 75ml zilizoachwa na gavana twinning.
uchaguzi 1970 - utaifishaji wa benk za Baclays
uchaguzi 1975 - vijiji vya ujamaa
uchaguzi 1980 - mafao ya wastaafu africa mashariki
uchaguzi 1985 - Ununuzi Dhahabu hewa NBC/BOT
uchaguzi 1990 - IPTL -
uchaguzi 1995 - CIS bn65
uchaguzi 2000 - Minara BOT, bn200
uchaguzi 2005 - EPA/Manji/nssf bn133+85 = bn218
uchaguzi 2010 - Vitambulisho/richmond - bn222
uchaguzi 2015 - liganga na mchuchuma - bn500
uchaguzi 2015 - uranium - bn700
uchaguzi 2020 - kurusha setelite anga za juu - bn900
uchaguzi 2025 - shirikisho la africa mashariki - hima empere.
uchaguzi 2030 - United states of Africa.

sioni sababu ya kuendelea na mfumo wa democrasia ya uchaguzi, tukiri nchi imetushinda tumrudishie mwingereza koloni lake.

Au turudishe mfumo wa machifu, tumjue kiongozi ni nani hasa. aandaliwe toka utotoni.
 
Sometimes its good to be serious, waheshimiwa wetu included!

There is a whole lot that goes into a national id than the price mentioned here! Huyo mpiga picha wa serikalki angeonganisheje vizazi na vifo, upigaji kura, kununua sim cards, kufanya background checks, etc, etc?

Give me a break! I'm sorry to say but waheshimiwa hao na mpigapicha wa serikali have no clue to what they are insinuating, period!
 
Sometimes its good to be serious, waheshimiwa wetu included!

There is a whole lot that goes into a national id than the price mentioned here! Huyo mpiga picha wa serikalki angeonganisheje vizazi na vifo, upigaji kura, kununua sim cards, kufanya background checks, etc, etc?

Give me a break! I'm sorry to say but waheshimiwa hao na mpigapicha wa serikali have no clue to what they are insinuating, period!

It seems you are the one who does not have a clue. This was a question of tendering, they said they wanted to tender-that will have definitely included all the aspects you have raised. Do you want to tell me that Masha's SAGEM has a track record of dealing with all the aspects you have raised? The answer is NO!. This government guys would have teamed up with other experts in the area and saved a lot of tax payers money. By the way, we have RITA which is a government agency dealing with such issues. They could have done the job as well. CCM guys are just looking for money there for fueling their presidential ambitions. Before it was Mungai, then Membe now Masha....this ID thing is a sniff!

Asha
 
Back
Top Bottom